Mbona walevi wanapata pata hela kuliko wasiokunywa

Mbona walevi wanapata pata hela kuliko wasiokunywa

Me na ex wangu ilikuwa kila siku jioni lazima twende kupata dinner ambayo ilikuwa ni kati ya elfu 12 hadi 15 alafu tunapitia kwenye kigroccery me nakunywa bia tatu yeye tano au zaidi kutegemea tu na siku yenyewe itakavyokuwa tulikuwa tunatumia kati ya elfu 30 hadi 40 kila jioni
Weekend tunakesha bar na tunaamkia guest
Siku kama hizo laki na nusu ilikuwa ni kawaida kuisha
Nilivyokaa na kutathmini hiyo kitu nikataka tubadili mfumo wa maisha kwamba tunachoma hela nyingi sana kwa hali ya maisha yetu ni bora kusave tuwe angalau weekend ndiyo tunatoka na shughuli tumalizie nyumbani badala ya guest elfu30 tunafuata ac

Kweli ikawa hivyo kama baba nilivyoamua
Lakini after kama miezi miwili pashkuna ananiambia hivi mpaka saivi tumesave bei gani mbona hatuna kitu na hatuenjoi tena kama mwanzo
Ni kweli hatukuwa na chochote tulichosave


Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
Dah umenichekesha sna mkuu😁
 
Walevi wengi ni wapiga deal na wahujumu wa Mali ya umma Ili wapate pesa ya kununuliana pombe.

Ulevi ukomeshwe katika utumishi wa umma na sekta binafsi.
Jidanganye 😁
 
katika utafiti wangu mdogo usio rasmi, ukifanya vitu vinavyoweza sababisha uovu zaidi, ni rahisi zaidi kupata pesa nyingi zaidi na kwa haraka kuliko vile vinavyosababisha amani na upendo. Ukiwa mgodini ukatamani kutumia pesa kusaidia wenye huitaji zinapatikana kwa shida kuliko zile za starehe, pia kwenye biashara zote hasa zile haramu. Na pesa hizi mara chache sana zinadumu kusaidia kizazi kijacho.
 
Kumbe kuna ulevi wa kusali tena!
Angalia makanisa yanayojiita ya kilokole , pia angalia aina ya maisha ya waumini wao pia angalia masaa yao ya kazi na masaa yao kusali tofauti yake.
 
Sio kwamba walevi wana bahati,,,,, ni kwamba wanakutana sana maeneo ya starehe kama bar n.k ,,, huko huko kwenye unywaji ndo wanapeana connection kadha wa kadha,,,, binafsi juzi kati January hapa kuna mshikaji tulikutana tu bar story za hapa na pale, kupitia yeye nikauziwa kiwanja na rafiki yake bei ya kutupa kabisa alafu eneo potential sana ,,, hakuna udalali wala nini ! Ni hayo tu ndugu mtoa mada
Mlevi akiwa ana dili fulani, wa kwanza kumkumbuka ni mlevi mwenzake kwa sababau anajua mlevi mwenzake akipata hela watakutana tu na watakunywa wote kuliko mnywa soda anaweza kutokomea mazima!
 
Back
Top Bottom