Mbona wanawake wakijiweza kidogo tu kiuchumi wakalingana na wanaume wanakuwa na dharau?

Mbona wanawake wakijiweza kidogo tu kiuchumi wakalingana na wanaume wanakuwa na dharau?

Habari za saivi ndugu zangu.

Dhumuni la kuleta hii mada hapa ni ili kupata msaada wa kimawazo kuhusu binti mmoja tuliodumu kwenye mahusiano kwa miaka minne.

Kipindi tunaanza tulikuwa tukipendana, tulikuwa mkoa mmoja naye mkoa mwingine ila kila akitaka fanya jambo lazima anishirikishe. Akawa anatunza pesa, namtunzia hadi ikafika milioni 1, alikuwa ananiamini sana kweli ikafika kipindi akaihitaji nikampatia akasema afungue kijiduka cha nguo.

Akafungua biashara ikawa inaenda ananiagiza nimchukulie mzigo mjini, nachukua namtumia.

Sasa mwaka huu shida imekuja amekuwa kama hana muda na mimi, ukimwambia ichi anakuja juu sana. Kawa mtu wa kujionesha kwingi, mtandaoni ana marafiki wengi sana wa kiume.

Ikawa kila siku sijui anaenda wapi, anajipost yupo na boda wake wanajisnap. Namuuliza watu wanaojua tuko kwenye mahusino wanakuchukiliaje wewe na huyo kijana akajibu "HAKUNA ANAENILISHA HUYU NI KAMA NDUGU YANGU"!

Nikapotezea maisha yakaenda, akawa mtu wa visirani sana.

Ukimwambia kitu hajali, sasa nipo nafikiria nimuache tu maisha yake maana kwa hali yake ya sasa IMENISHINDA.

Naombeni msaada wa mawazo ndugu zangu.
Hao viumbe wewe wasikie tu kwenye redio.
Kuna pasta mmoja maarufu Sana hapo Burundi alimnunulia mke wake gari ya gharama Tena toka dukani, huku mke huyo huyo ambaye jamaa anapenda Sana kujitangaza naye akawa analiwa na sekretari wa huyo pasta uchwara mpaka amezaa naye. Ukifunguamitandao ya kijamii utamuona huyo pasta michongo anavyo weweseka utadhani Ni bundi wakati wa kiangazi.
Kifupi ukimtangaza Sana mkeo ujue Kuna watu Tena wakaribu watapenda kumuonja.
Hata hicvyo inasemekana pasta Hana zile nguvu pendwa za wanaume wa Dar. Akipigwa ngumi moja tu wiki mbili au tatu haamki.
 
Mi huwa naamini wanawake hawana uhitaji wa kuwa na mwanaume ila wanahitaji tu ile mali anayomiliki mwanaume.....ndio maana mwanaume kama huna kitu ni ngumu sana kupata mke, mwanamke akipata mali yake mwenyewe anakuwa hana kabisa uhitaji wa mume na ikitokea ukampata mke wa namna hiyo jiandae kunyanyaswa tu.
Mstari wa kwanza umemaliza kila kitu
 
Dah.
bro wew ni CLONE yangu kabisa. mim yamenikuta ayo kuna mwanamke nilikuwa nae kimahusiano akanibwaga sasa anatoka na kigogo wa benki moja mjin. dem kawezeshwa anakipato kikubwa kunizid mim bas ananitambia mitandaoni alaf anadharau sio poa adi mtindo wa kuongea amebadiri anaongea kama sepetu
Pole sana kaka! Dah
 
Hao viumbe wewe wasikie tu kwenye redio.
Kuna pasta mmoja maarufu Sana hapo Burundi alimnunulia mke wake gari ya gharama Tena toka dukani, huku mke huyo huyo ambaye jamaa anapenda Sana kujitangaza naye akawa analiwa na sekretari wa huyo pasta uchwara mpaka amezaa naye. Ukifunguamitandao ya kijamii utamuona huyo pasta michongo anavyo weweseka utadhani Ni bundi wakati wa kiangazi.
Kifupi ukimtangaza Sana mkeo ujue Kuna watu Tena wakaribu watapenda kumuonja.
Hata hicvyo inasemekana pasta Hana zile nguvu pendwa za wanaume wa Dar. Akipigwa ngumi moja tu wiki mbili au tatu haamki.
Pastor hana nguvu za kiume?
 
waislam wakisema wanawake ni wakukaa tu ndani na kulea familia.mnawaona waislam wakandamizaji.Mungu aliyaona haya.
Huyo ameumbwa kupewa tu.
Alianza kujipa mwenyewe umekwisha
Mkuu hakika nmekuelewa
 
Back
Top Bottom