Mbona watu wengi wanapenda kuhama usiku tu?

Mbona watu wengi wanapenda kuhama usiku tu?

lukelo sakafu

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2015
Posts
2,938
Reaction score
517
Wakuu,

Nina hoja fupi hapa, hivi mbona wakazi wengi wa Dar es salaam na miji mingine wanapenda kuhama usiku usiku tu? Mtu anatoka Keko anahamia Mbagala lazima atahamisha vitu usiku tu. Hivi kunani hapa? Wanaficha nini? Kwanini wasihame mchana au asubuhi?

Wakuu karibuni hapa mtujuze
 
lukelo sakafu

Mi nilihama mchana, ukiona wanahama ucku kawaulize nadhan watakupa jibu muafaka vngnevyo utatulalizimisha kuwabetia majibu yao km si kuwasemea
 
Last edited by a moderator:
Ni muda mzuri,kusitiri Mali zao,ili si kila mtu ajue Fulani anamiliki nini na nini.

Ila si wote wengine wengi tu sikuhizi wanahama mchana
 
Lukelo Sakafu umepatia, ni hivyo viumbe Kunguni ndo tatizo
 
Kwasababu za kiusalama, vibaka wakikodolea vitu wanaweza vitamani nakuvifuata nakusababisha usumbufu na madhara yanayoweza kuepukika. Sasa basi ili kuepuka hali hiyo dawa nikuhama usiku.
 
Wanaogopa nyumba ndogo za mtaa wanaohama zisijue kama buzi limekata kamba. maana wakijua watakufuata kudai hela ya matunzo na kodi ya nyumba
 
Back
Top Bottom