Mbona watu wengi wanapenda kuhama usiku tu?

Mbona watu wengi wanapenda kuhama usiku tu?

lukelo sakafu

Sasa Unataka Wahame Mchana Uone Mende Na Kunguni Wanavyoserebuka Ktk Vyombo? Usiku Utahisi Tu ILA Hutojua Kitu Chochote!
 
Last edited by a moderator:
Kwasababu za kiusalama, vibaka wakikodolea vitu wanaweza vitamani nakuvifuata nakusababisha usumbufu na madhara yanayoweza kuepukika. Sasa basi ili kuepuka hali hiyo dawa nikuhama usiku.

Vibaka Hawana Formula!
 
unahama mchana huku vibaka wanakodolea macho, hata kabla hujafika unakohamia wao tayari walishaanza kupanga bei ili TV laki3, sofa laki6, friji laki5, mpaka mapazia wanayathaminisha huku we hujui mwisho wa siku unavamiwa ndoto zinatimia
 
Mi nazan wanapenda kuhama usiku kutokana na kukwepa kudiskasiwa na majiran walomzunguka kwa vitu alonavyo iwe vya garama au hata visivyo vya garama maana jamii ilotuzunguka ya kiswahili inapenda kujadili mambo yasowahusu
 
lukelo sakafu

Daah..Mkuu umenikumbusha siku nahamia kwenye nyumba yangu..nimeamka saa 7 usiku na madogo hadi saa 11 nimeshamaliza kufunga mizigo nikaita canter saa mbili tu nimeshaingiza vitu ndani..wife anaandaa chai..nilisema lazima ninywe chai nyumbani kwangu..!!
 
Last edited by a moderator:
mkuu sio kwamba wanaficha kunguni na magodoro yenye ramani za mikojo?

May be,

Lakini pia wanaficha flat screen zao,meza zao za vioo na makabati original wezi wasije wakayaona, Kesho wakawaibia.
Maana usiku ni ngumu kujua mtu kabeba nn
 
Si hami mchana mpaka wife aache kupiga kojo kitandani!
 
Mi nilihama mchana,sijui kwa vile nilikuwa nimekwaza na mwenye nyumba wangu.
 
Nadhani ni uamuzi tu, na may be kila mtu ana sababu yake ya kufanya hivyo
 
lukelo sakafu

Mkuu swali lako linafanana na linalosema "Kwanini wana ndoa wengi hupenda kula tunda la mti wa katikati wa mema na mabaya usiku?" Mengine yanayofanana na hayo ni "Kwanini wagonjwa wengi hufa usiku - tena usiku wa manane? na Kwanini watoto wengi huzaliwa usiku?"

- Sikiliza taarifa za mikesha ya krismas, pasaka na Idd kesho yake utaona wanatoa idadi ya watoto waliozaliwa usiku! Yaani usiku una mambo mengi hata ujambazi na uhalifu mwingi hufanyika usiku.
 
Last edited by a moderator:
Kuepuka majungu " ona kigodoro kimechoka' pia wengi hawatak watu wajue wana vitu gani kupeleka wizi anapoamia
 
Back
Top Bottom