Mbona watu wengi wanapenda kuhama usiku tu?

Mbona watu wengi wanapenda kuhama usiku tu?

We mtoa mada ivi unajua ugumu wa kumhamisha kunguni bila kuonekana?
 
Nimewauliza wadada fulani swali hili; mmoja akadakia kwa kudai hataki watu waone vitu anavyomiliki.

Wakuu hii sababu inatosha kweli hadi mtu ahame usiku mwingi?
 
1. Kutopenda kuchunguzwa vitu anavyomiliki muhusika kwa sehem anako hamia au alipokuwepo.
2. Kutopenda kujulikana anahama(wengi wasimuone)
3. Nafasi(wengi wa watu huwa free wakati wa usiku hivyo ndo muda wakufanya mambo ya ziada kama kuhama)
4. Unafuu wa nauli na upatikanaji wa usafiri(Muda wa usiku ndo muda ambao madereva wa vi lory au kirikuu ni wepesi kukubali bei yotote ili mradi siku isipite bure ukitofautisha na wakati mwingine kama asubuh au mchana .
5.Kuficha baadhi ya siri zake(Wengine huwa na madoro machafu au mambo hata ya kishirikiana hivyo hapendi vionekane)
6. Mozoea (Baada ya hayo yote basi hata kama mtu hana hizo sababu hujikuta nae kuangukia katika mazoea haya bila hata sababu maalumu)
 
We' utakuwa mzoefu wa kuhama hama....[emoji28][emoji28]
 
Inavyoaminika mitaani:
Wanaohama usiku wengi ni wanaoishi nyumba za kupanga. Wanaohama mchana wengi ni wale wanaohamia kwenye nyumba zao mpya. Anatoka mchana kweupe ili mumuulize, unakwenda wapi? "Nahamia kwangu 😀" atakujibu.
😂😂
 
Habari za wakati huu kaka na dada zangu wote wa humu JamiiForums.

Ndugu zangu Watanzania;

Nini mantiki na chanzo kikuu cha kasumba hii ya wapangaji wengi kupenda kuhamia eneo la makazi mapya muda wa usiku/giza?

images (6).jpg

Kwa ambao hamnijui, mimi nimekaa sana uswahilini. Nimeishi Kurasini, Keko pamoja na Mbagala. Hii tabia ninaijua kwa kipindi kirefu tu na nina uhakika nitapata majibu humu kwa wadau.

Unakuta mtu amepanga vitu vyake kuanzia asubuhi mpaka mchana amemaliza. Baada ya kumaliza anakuwa hana shughuli nyingine zaidi ya kuondoka, lakini yeye haondoki.

Ikifika saa moja giza limeingia ndio unaona canter, pick-up, kirikuu au Fuso hiiiilooooo ndio linaingia na wanaanza kubeba makabati, magodoro, viti, masufuria wanaanza kuingiza katika gari tayari kwa kuhama. Why this?

Kwani kuna tatizo gani mtu akihama jua likiwa bado linawaka. Nilijaribu kufanya utafiti kidogo kwa baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki ambao ni wamama na wababa watu wazima wakaniambia kwamba, ukiwa unahamia nyumbani kwako ulipojenga hiyo ni ruksa kuhamia jua likiwa linawaka lakini ukiwa unahamia katika nyumba ya kupanga, hususan yenye wapangaji wengi, basi ni vema ukahamia giza likiwa limeingia.

Je, nini chanzo na mantiki ya kasumba hii?

NB: Kuna makala moja tamu kuhusu MOSSAD nitaiweka soon kule Jamii Intelligence.

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
Zaidi ya kukwepa aibu ya vyombo vilivyo chakaa ..labda na kuhofia kijicho na husda

Watu hawapendi kuonesha vyombo vya ndani
Hasa magodoro yaliyo chakaa.

Wengine hawapendi kuonesha assets zao za ndani kama wanazo kuhofia husda
 
Back
Top Bottom