Habari za wakati huu kaka na dada zangu wote wa humu JamiiForums.
Ndugu zangu Watanzania;
Nini mantiki na chanzo kikuu cha kasumba hii ya wapangaji wengi kupenda kuhamia eneo la makazi mapya muda wa usiku/giza?
Kwa ambao hamnijui, mimi nimekaa sana uswahilini. Nimeishi Kurasini, Keko pamoja na Mbagala. Hii tabia ninaijua kwa kipindi kirefu tu na nina uhakika nitapata majibu humu kwa wadau.
Unakuta mtu amepanga vitu vyake kuanzia asubuhi mpaka mchana amemaliza. Baada ya kumaliza anakuwa hana shughuli nyingine zaidi ya kuondoka, lakini yeye haondoki.
Ikifika saa moja giza limeingia ndio unaona canter, pick-up, kirikuu au Fuso hiiiilooooo ndio linaingia na wanaanza kubeba makabati, magodoro, viti, masufuria wanaanza kuingiza katika gari tayari kwa kuhama. Why this?
Kwani kuna tatizo gani mtu akihama jua likiwa bado linawaka. Nilijaribu kufanya utafiti kidogo kwa baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki ambao ni wamama na wababa watu wazima wakaniambia kwamba, ukiwa unahamia nyumbani kwako ulipojenga hiyo ni ruksa kuhamia jua likiwa linawaka lakini ukiwa unahamia katika nyumba ya kupanga, hususan yenye wapangaji wengi, basi ni vema ukahamia giza likiwa limeingia.
Je, nini chanzo na mantiki ya kasumba hii?
NB: Kuna makala moja tamu kuhusu MOSSAD nitaiweka soon kule Jamii Intelligence.
USISAHAU:
ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.