Mbosso anaimba Taarab sio Bongo Fleva, nashangaa sana mwanaume kuimba nyimbo za Mbosso

Mbosso anaimba Taarab sio Bongo Fleva, nashangaa sana mwanaume kuimba nyimbo za Mbosso

Kila mahadhi ya Pwani ni taarabu kaka? ina maana utaniambia The Mashrooms wanaimba taarabu pia? Siri yangu ya Jay Dee ile ni taarabu? Nataka kuwa nawewe ya kina Berry Black nayo ni Taarabu?
Mzee nimesema kila mahadhi ya pwani ni taarabu? Hapana

Sijui namna nzuri ya kukuelezea ila Mbosso kwa jinsi anavyopandisha sauti (vocal vibrato/majonzi), na mashairi ya vijembe au mahaba yanafanya nyimbo zake kuwa kama Taarab

Sijui kama unamsikiliza au unabisha tu...kajaribu kutafuta nyimbo kama Hodari, Nadekezwa, Tamba, Yalah, au sitaki kama unafahamu muziki basi utaona Kuna mfanano mkubwa na taarabu
 
Hivyo vikarolaiti vyenu,
nitavipiga marufuku hapa ,

mimi nina rangi yangu,
sina uso wa vibaka,
Mimi nina rangi yangu,
nakopa bado nalipa aaah,

Bandika bandika mmi ,
nabandua tumependana wawili, wewe unajichomeka ,
hakutaki pesa mbili ,
hunijui takataka ,
bandika bandika ,
mm nabandua aah aaaaah, tuulikaaa aaah ,
Naam ni mashairi ya Taarab haya, sijui kwa nini watu wanabisha su kukasirika
 
Huu muziki wa Mbosso sijawahi kuuelewa, ni taarabu, tena nyingine unakuta Zina matusi ya wazi wazi kabisa
Ila unakuta dume zima linaimba au kufuatisha, halafu linaponda taarabu.
Sasa usichokijua Taarabu ndio Mdundo wa Taifa

kabla ya Mchiriku, kabla ya Mnanda kabla ya Muziki wa Dansi kupata soko Tanzania wakina Ali Choki na Mwijuma Muumini na wengineo FM Academia mziki uliokua una trend enzi zetu ni muziki wa Taarabu na ndio zao la miziki mingine yote unayoisikia sasa hivi mpaka Kwaya na miziki ya Injili na Qaswida unazozisikia zina mahazi fulani ya Taarabu ndani yake vile vionjo ila ni ile Old Taarabu ya zamani kabisa sio hii Modern ambayo sasa imewekwa kando, mziki singeli wanajaribu kuifanyia modifications miziki ile ya Taarabu ila wanachokosea ni kufanya modernization iliyopitiliza naa uimbaji uliokosa mpangilio sababu ya kuimba matusi yasiyokua na afya kwa msikilizaji wakihisi ya kwamba ndio mziki utapendwa zaidi ukijaa matusi

Bongo fleva ni mziki uliochipukia miaka ya 1990 baada ya Mziki wa Dansi ambao ulitanguliwa na mziki wa Taarabu za wakina Nasima Kidogo na Khadija Koppa bila kumsahau Marehemu Bibi Kidude RIP,

sasa unaposema Mbosso anaimba Taarabu maana yake anaimba mziki namba 1 wa Tanzania ambao ndio mdundo wa Taifa hili kwa maana hio anatakiwa apewe sifa sio kubezwa na kuonekana anaimba kitu ambacho hakifahi sio sahihi km umeona anaimba Taarabu ilitakiwa umpe heshima tena heshima haswa
 
Mzee nimesema kila mahadhi ya pwani ni taarabu? Hapana

Sijui namna nzuri ya kukuelezea ila Mbosso kwa jinsi anavyopandisha sauti (vocal vibrato/majonzi), na mashairi ya vijembe au mahaba yanafanya nyimbo zake kuwa kama Taarab

Sijui kama unamsikiliza au unabisha tu...kajaribu kutafuta nyimbo kama Hodari, Nadekezwa, Tamba, Yalah, au sitaki kama unafahamu muziki basi utaona Kuna mfanano mkubwa na taarabu
Kaka, Taarabu ni sehemu ndogo tu ya Muziki wa Pwani. Muziki wa Pwani unahusisha Sub Genres kama Benga, Chakacha, Mchiriku/Singeli(hii ya leo) na Taarabu.

So, Mboso ana vionjo vya Pwani kwenye muziki wake, and you wrong to term it specifically taarabu. Sababu uimbaji wa kuvuta na kupandisha sauti na kuiremba (vocal ornamentation) na kuimba kwa mafumbo haiko kwenye taarabu bali muziki wote wa Pwani ndio asili yake.
 
Sasa usichokijua Taarabu ndio Mdundo wa Taifa

kabla ya Mchiriku, kabla ya Mnanda kabla ya Muziki wa Dansi kupata soko Tanzania wakina Ali Choki na Mwijuma Muumini na wengineo FM Academia mziki uliokua una trend enzi zetu ni muziki wa Taarabu na ndio zao la miziki mingine yote unayoisikia sasa hivi mpaka Kwaya na miziki ya Injili na Qaswida unazozisikia zina mahazi fulani ya Taarabu ndani yake vile vionjo ila ni ile Old Taarabu ya zamani kabisa sio hii Modern ambayo sasa imewekwa kando, mziki singeli wanajaribu kuifanyia modifications miziki ile ya Taarabu ila wanachokosea ni kufanya modernization iliyopitiliza naa uimbaji uliokosa mpangilio sababu ya kuimba matusi yasiyokua na afya kwa msikilizaji wakihisi ya kwamba ndio mziki utapendwa zaidi ukijaa matusi
Hakuna mdundo wa taifa Tanzania na ni ngumu kuwa na mdundo wa taifa kwa sababu za kijiografia. Tuna makundi kimaeneo karibu 6 kimuziki ambayo hayafanani kabisa kimidundo, kiushawishi na lengo la kimuziki.

Huo muziki wa Pwani unaousema, ukifika Morogoro tu wenyeji hawauelewi, ukifika dodoma, singida sio wao, ukifika Shinyanga, Tabora, Mwanza Geita wanaona ni kelele tu. Ukienda kaskazini kule haukisi mambo yao.

So, Tanzania hakuna mdundo wa Taifa, jiografia inatukataa.
 
Kaka, Taarabu ni sehemu ndogo tu ya Muziki wa Pwani. Muziki wa Pwani unahusisha Sub Genres kama Benga, Chakacha, Mchiriku/Singeli(hii ya leo) na Taarabu.

So, Mboso ana vionjo vya Pwani kwenye muziki wake, and you wrong to term it specifically taarabu. Sababu uimbaji wa kuvuta na kupandisha sauti na kuiremba (vocal ornamentation) na kuimba kwa mafumbo haiko kwenye taarabu bali muziki wote wa Pwani ndio asili yake.
Kaka sijasema kila muziki wa Pwani ni taarabu
Na taarab nayo Ina gernes zake, kwa jinsia anavyoimba Mbosso muziki wake una distinctive characters za taarabu, sema kwa sababu ameshatambulishwa na anafanya kazi na watu wa Bongo Fleva ndio basi watu wanaona ni Bongofleva
 
Usisikilize nyimbo za Mbosso kama hauna mpenzi wala mapenzi huyajui utapata dipuresheni bure km hivi mtoa mada,,, sipo single
😂😂Dah, sipo single jamani, sema kila mtu ana ladha yake ya muziki.
Sorry kama nimemponda kipenzi chako
 
Wanaopenda mziki, wanasikiliza na kuburudika kwa vyombo vinavyopigwa(akisikia tarumbeta, solo, base, rhythm, japo ni computerized). Hayo maneno watu hawajali.
 
Ndio nikiusikia naujua
Sasa Mboso Anafanya AfroPop. AfroPop ni muziki ambao ni vionjo vya kiafrika vinavyochanganywa kwenye Muziki wa kimarekani (Pop).

Ushasikia nyimbo ya Fally Ipupa La viest bell? Je ile ni Rhumba? Au Nidja na R Kelly ile ni Rhumba?
 
Back
Top Bottom