Mbosso anaimba Taarab sio Bongo Fleva, nashangaa sana mwanaume kuimba nyimbo za Mbosso

Mbosso anaimba Taarab sio Bongo Fleva, nashangaa sana mwanaume kuimba nyimbo za Mbosso

Huu muziki wa Mbosso sijawahi kuuelewa, ni taarabu, tena nyingine unakuta Zina matusi ya wazi wazi kabisa
Ila unakuta dume zima linaimba au kufuatisha, halafu linaponda taarabu.
Huu wivu wa kike kijana. Itabidi tukupeleke kwa dudu baya
 
Sasa Mboso Anafanya AfroPop. AfroPop ni muziki ambao ni vionjo vya kiafrika vinavyochanganywa kwenye Muziki wa kimarekani (Pop).

Ushasikia nyimbo ya Fally Ipupa La viest bell? Je ile ni Rhumba? Au Nidja na R Kelly ile ni Rhumba?
Duh😂😂😂
 
Mchiriku/Singeli(hii ya leo)
Mchiriku sio Singeli usichanganye, Singeli haihusiani kabisa na Mchiriku wala Mnanda ule aliokua anaimba Marehemu Omari Omari RIP,

Singeli ni mziki uliotoholewa kwenye miziki mingine na midundo mingine ya ngoma zetu za asili kwa kuongezewa vionjo vionjo vidogo vya hapa na pale ili kuipa ladha aidha kwa kuzidisha mwendo ya wimbo huo kwa speed kadhaa tena mziki huu ulianza kwa kutumia VLC Media Player baadae wakatumia Virtual DJ kabla ya kuhamishiwa kwenye FL Studio na kuonekana ni bidhaa inayoweza kuingia sokoni yaan mziki unakua wa kawaida unaongeza speed ndio unapata Singeli, zamani huko Kenya walikua wanauita Kapuka ukiondoa Chakacha na Chachacha

huo Mchiriku ni ngoma ya Wazaramo km sijakosea na nina hakika nipo sahihi 100% na ilikua inapigwa kipindi kile na wali wakiwa wanatoka ndio inaletwa hio ngoma pamoja na ngoma ya Mkole inapigwa wanakua km wananema hivi huku wakiwa wamepakwa pakwa ufuta mwili mzima na baada ya hapo wali wale walikua wanaolewa moja kwa moja, kuna ngoma nyingine km Seketure nayo pia ni ya Wazaramo

sasa kidogo naweza nikasema midundo ya Singeli inafanania na ngoma za kule Morogoro labda kidogo Wapogolo, Wakami, Wakutu, Waluguru, Wambunga, Wandamba, Wangulu, Waparakuyo, Wasagara, Wavidunda na Wakaguru ndio midundo yao ya ngoma zikipigwa inakimbia kimbia sana wakiwa wanapiga ngoma yaan ni ngoma za kukimbia kimbia muda wote

Sasa kadri inavyoongezeka muda na miaka kwenda mbele hawa waandaji wa huo mziki (Producer's) wanaongezea ladha wanaongezea na midundo ya ngoma nyingine za asili mfano Lizombe, Sindimba, Ngokwa, Mdundiko, Seketure, Mkole, Mbereko, nq zinginezo nk ili tu ionekane ya tofauti ila Singeli sio Mchiriku wala sio Mnanda
 
Huu muziki wa Mbosso sijawahi kuuelewa, ni taarabu, tena nyingine unakuta Zina matusi ya wazi wazi kabisa
Ila unakuta dume zima linaimba au kufuatisha, halafu linaponda taarabu.
Nisikilize nisikilize mpenzi wewe
Mbosso Khan tena
Oh ngayo ngayo ngayo
Matone ya maji hufuata michirizi
Niondoe imani ambayo
Kulilinda penzi ni fundo la irizi
Oh mayo mayo mayo
Shikilia gego nyama ya ufizi
Mie wayo wayo wayo
Ukiniacha wewe nitapata uchizi
Tane tane sikinai yako mahaba
Tupeane hata kwa siku mara saba
Tane tane sikinai yako mahaba
Tupeane hata kwa siku mara saba
I never feel how I feel to you
See a bad man Mbosso Khan confused
Kati ya pesa na wewe tu, choose choose

Note: yuko vizuri dogo acha hizo.
 
Niliwahi kuwaza kama wewe huu uimbaji wa mboso ni taarabu kabisaa,me nilistuka sijawahi kupenda nyimbo zake ingawa hata bongo flava sio mpenzi kivile me ni mpenzi wa rnb na hip hop tu
 
Back
Top Bottom