Mchiriku/Singeli(hii ya leo)
Mchiriku sio Singeli usichanganye, Singeli haihusiani kabisa na Mchiriku wala Mnanda ule aliokua anaimba Marehemu Omari Omari RIP,
Singeli ni mziki uliotoholewa kwenye miziki mingine na midundo mingine ya ngoma zetu za asili kwa kuongezewa vionjo vionjo vidogo vya hapa na pale ili kuipa ladha aidha kwa kuzidisha mwendo ya wimbo huo kwa speed kadhaa tena mziki huu ulianza kwa kutumia VLC Media Player baadae wakatumia Virtual DJ kabla ya kuhamishiwa kwenye FL Studio na kuonekana ni bidhaa inayoweza kuingia sokoni yaan mziki unakua wa kawaida unaongeza speed ndio unapata Singeli, zamani huko Kenya walikua wanauita Kapuka ukiondoa Chakacha na Chachacha
huo Mchiriku ni ngoma ya Wazaramo km sijakosea na nina hakika nipo sahihi 100% na ilikua inapigwa kipindi kile na wali wakiwa wanatoka ndio inaletwa hio ngoma pamoja na ngoma ya Mkole inapigwa wanakua km wananema hivi huku wakiwa wamepakwa pakwa ufuta mwili mzima na baada ya hapo wali wale walikua wanaolewa moja kwa moja, kuna ngoma nyingine km Seketure nayo pia ni ya Wazaramo
sasa kidogo naweza nikasema midundo ya Singeli inafanania na ngoma za kule Morogoro labda kidogo Wapogolo, Wakami, Wakutu, Waluguru, Wambunga, Wandamba, Wangulu, Waparakuyo, Wasagara, Wavidunda na Wakaguru ndio midundo yao ya ngoma zikipigwa inakimbia kimbia sana wakiwa wanapiga ngoma yaan ni ngoma za kukimbia kimbia muda wote
Sasa kadri inavyoongezeka muda na miaka kwenda mbele hawa waandaji wa huo mziki (Producer's) wanaongezea ladha wanaongezea na midundo ya ngoma nyingine za asili mfano Lizombe, Sindimba, Ngokwa, Mdundiko, Seketure, Mkole, Mbereko, nq zinginezo nk ili tu ionekane ya tofauti ila Singeli sio Mchiriku wala sio Mnanda