Benson Kigaila, Mzee wa miaka 57 anatumwa kupeleka barua, kwa nini asimpe kazi huyo? Au John Mrema, kapiga debe mpaka mdomo umeenda upande na sauti imekwama, Mbowe hawaoni?
Ha haa! Hata huku kwetu ni kugumu! Wakati nimefulia niko kitaa sina kazi, niliwaomba wakubwa wa huku kwetu, wanitupe hata wilayani kwenye ajira ya kutembelea Land cruiser chakavu; Wakaona ntafaiidi! Wakanitosa.
Nikawaambia hawa ni kwa vile hawajajua historia yangu. Wakati niko chuo mwaka wa kwanza 'tayari' nilikuwa namiliki usafiri wa piki piki. Nilikuwa mwanafunzi pekee aliyekuwa anatembelea piki piki kutoka bwenini kwenda lecture hall: ukiacha wale walemavu ambao walikuwa wamenunuliwa Bajaj na chuo.
By mwaka wa tatu, tayari nilikuwa namiliki gari 'mpya' niliyoinunua Zanzibar mwaka 2008. Na two yrs later nilikuwa nimeshakabidhiwa pick up mpyaa ambayo iliniwezesha kuwa all over the place.
Sana sana niliwashukuru kwa kuninyima nafasi ya kuishi maporini mimi mwana Darisalama.
Kwa kudra za Mwenyezi Mungu, maisha yakasonga mbele na ujenzi wa gorofa unaendelea mdogo mdogo kwa hivi viriziki vya mia mbili, angalau watoto wangu hawatarithi nyumba ya makuti.
Huwa nawashangaa wale wanao ona bila hivi vijinafasi maisha hayatoenda!
Maisha ni lazima yaende. Mlango mmoja ukifungwa mwingine hufunguka.
Napenda kuwadediketia wimbo huu wapambanaji wote waliokosa fursa mbali mbali kuwa, in the end it has made them much stronger!