Mbowe aachiwa huru na wenzake watatu baada ya DPP kuwasilisha hati ya kutotaka kuendelea na kesi

Mbowe aachiwa huru na wenzake watatu baada ya DPP kuwasilisha hati ya kutotaka kuendelea na kesi

Kwanza pole kwa misukosuko yote ile uliyo pitia kwa kipindi chote kile ulicho sota gerezani ,umepitia udhalilishaji mkubwa San a katika duru hii ya siasa kwani naamini umepata ukomavu wa kutosha katika harakati zako za kudai demokrasia katika nchi hii ya JMT sasa karibu uraiani

Kazi ni moja tu kudai katiba mpya itakayo tufanya tuyasahau haya yote tunayopitia kwass
 
Muda muafaka kwa mama kusafisha vyombo vya ulinzi na usalama ikiwemo Jwtz, Tiss, Police na Takukuru ambavyo kwa namna moja au nyingine vimeshiriki katika mchakato huo wa kesi Kisha kufeli upelelezi na kubambikiza innocent people kesi hii haipo sawa mama achague viongozi waadilifu vinginevyo watachafua hii Serakali yako tukufu
 
Wale mawakili wa tigo na Airtel wafutwe kazi haraka sn

Sent from my HUAWEI LUA-U22 using JamiiForums mobile app
Yeah..yan hii iwe bampa tu bampa...Wafungue kesi dhidi ya ushahid wa uwongo waliotuhumiwa nao.Fungua kesi dhidi ya TIGO & AIRTEL.
Hiv voda walikwepaje hii skendo kwel watuhumiwa wooye wale hakuna hata mtumiaji wa voda?? A coisedence or plan??
 
Ni Tanzania tu ambako mshtakiwa wa makosa makubwa kama ugaidi anaweza kuachiwa huru eti kwa sababu mkurugenzi wa mashtaka hana nia ya kuendelea na kesi na wewe kama zuzu unashangilia hapa.

Ule ulikuwa ni ujinga na kupotezeana muda na wewe acha kujipendekeza kwa uliowataja hapo juu.
Uhuni MTUPU unaendelea Bongo halafu wenye akili fupi wanasifu eti Maza. Seriously.

Kwa maoni yangu hii kesi hatakiwi kuisha hivi hivi kijuujuu. Kwa serikali kuifuta kuwa hawana nia bado wanayo nafasi ya kuirudisha siku wakiwa na nia na bado inaonyesha ni jinsi gani bado tuna sheria kandamizi za Mkoloni tulizozirithi. Wanasheria watusaidie kwenye hili.

Pia ni wakati sasa hawa watuhumiwa waanze kufunga kesi za madai kwa kuwekwa ndani na kutesa bila sababu ya msingi. Labda hiyo itatoa funzo kwa akina Maza wanaotengeneza matatizo halafu wanajifanya kuyatatua ili wasigiwe.
 
Pamoja na kufutiwa mashitaka naamini Mbowe na Genge lake la kihalifu watakuwa wameshika adbu.
na wamejifunza kuwa ukichezea Amani ya nchi utashughulikiwa kama mbwa koko.

Ushauri wa bure sasa ni bora akalee wajukuu.
aache tabia ya kuajiri wahalifu, wauza madawa, wavuta bangi, majambazi n.k

Sasa tutamfuatilia hadi chooni.
 
Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) Zitto Kabwe amesema kuachiwa huru kwa Mwenyekiti wa @ChademaTz
Mhe. @freemanmbowetz
ni miongoni mwa jitihada zilizokuwa zikifanywa na Taasisi hiyo ili kuimarisha Demokrasia kwa kuzungumza na mamlaka juu ya kushitakiwa kwa Mbowe.

My Take
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣✌✌✌✌
 
Mbowe ameweka rekodi ya kuwa Mkristo wa kwanza kushtakiwa kwa Sheria ya Ugaidi hapa Tanzania.
 
Usiwe kama mtoto mdogo!

Siku zote ccm huwa inawakomesha tu wapinzani wake.

Na hapa wala hata msisgangilie kwamba mmeshinda bali mnapaswa kujilaumu na kujiuliza kwamba inakuwaje ccm inawageuza geuza kama chapati namna hii!?

Sent from my SM-T295 using JamiiForums mobile app
Wewe ulikuwa unaandika kila siku kuwa lazima Mbowe afungwe,

Imekuwaje wewe ccm haujamfunga kama ulivyojiapiza? Na yuko huru sasa?
 
Jaji alisema Kuna kesi ya kujibu, Sasa DPP anaanzaje kufuta kesi wakati ofisi yake ndo ilipeleka kesi mahakamani(walikuwa wanaamini ipo kesi ya kujibu) huu Ni upuuzi maana mbowe kakaa gerezani muda wote hapigi mashine kumba hakuna kesi(haipo ndo maana imefutwa) na Kama ipo kesi ya kujibu kwa Nini DPP afute kesi ambayo jaji amesema ipo kesi ya kujibu?

Na jaji kwanini alisema Kuna kesi ya kujibu? Anajisikiaje kuiondoa kesi hiyo mahakamani isijibiwe?

DPP vs Jaji
nani anaemuona mwenzie fala?
 
Kingai na Urio wanapatikana wapi mda huu kuna mwenye taarifa ya wapi walipo?
 
Back
Top Bottom