Mbowe aachiwa huru na wenzake watatu baada ya DPP kuwasilisha hati ya kutotaka kuendelea na kesi

Mbowe aachiwa huru na wenzake watatu baada ya DPP kuwasilisha hati ya kutotaka kuendelea na kesi

Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) Zitto Kabwe amesema kuachiwa huru kwa Mwenyekiti wa @ChademaTz
Mhe. @freemanmbowetz
ni miongoni mwa jitihada zilizokuwa zikifanywa na Taasisi hiyo ili kuimarisha Demokrasia kwa kuzungumza na mamlaka juu ya kushitakiwa kwa Mbowe.

My Take
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣✌✌✌✌
Kila mtu mwenye akili timamu anajua ni jitihada za Tundu Lisu.
 
yeah, yamekugusa eee !!

Sasa ifike pahala kudai katiba mpya isiwe kosa la jinai - nafikiri ujumbe huu uwafikie wana Lumumba wote.
Mimi sio lumumba buku7 wala ufipa buku2
 
Baada ya upande wa Mashtaka kufunga ushahidi wao na kuialika Mahakama kutoa hukumu ndogo na kisha mahakama kuwakuta watuhumiwa na kesi ya kujibu mnamo Februari 18 2022. Leo 04, Machi 2022 ni siku ya watuhumiwa kuanza kujitetea kutokana na tuhuma wanazotuhumiwa nazo.

Awali Mahakama iliwakuta na kesi ya kujibu katika mashtaka 5 kati ya 6 katika kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili.
Hii ina maana gani kisheria? Jaji anasema kuna kesi ya kujibu na DPP anasema hakuna kesi ya kujibu? Nani ni msomi wa sheria na nani ni KIHIYO kati ya hao wawili?
 
Afadhali . Sasa tufuatilie yanayojiri Russia Ukraine vizuri
 
Tulishasema Mbowe ni mwamba, mlikaza fuvu…. ona sasa.!
 
Mimi sio lumumba buku7 wala ufipa buku2
sawa, sasa unafikiri hiyo kesi ilikuwa na uhai kwa taifa letu? wote sisi tumefurahi sababau kesi kwanza ilikuwa inatuabisha kama taifa.

Tufike pahala watanzania tuwe serious na mambo ya msingi na tuachane na mambo haya ya kukomoana yanayotupotezea muda na heshima kama taifa,
 
Mimi kwangu nitaikumbuka kesi hii kwa jinsi ilivyovutia,sidhani kama kuna kesi nyingine ambayo iliwahi kusikilizwa hadharani na kwa uwazi namna ile katika nchi yetu!
Tumeshuhudia jinsi Mawakili walivyochuana,tumeshuhudia jinsi waendesha mashitaki,wapelelezi wa serikali walivyokuwa wanajikanyagakanya na hata kutufanya tujue udhaifu wao.Tumeshuhudia baadhi ya Majaji walivyoikimbia kesi.
Katika hili nilikuwa naomba kesi zote ziwe zinasikilizwa kwa uwazi namna ile ili tujifunze mambo mengi yanayohusu Sheria.
Pongezi zangu ziwaendee Kibatala na Jopo lake!
 
Afadhali . Sasa tufuatilie yanayojiri Russia Ukraine vizuri
Putin kalalamika kasema si vizuri kuendelea kumuwekea vikwazo vya kiuchumi - yeye ana nia njema na Taifa la Ukraine.

Vita baridi achana nayo, tayari imeshaanza kumwingia.
 
Kama ni hivyo Mbowe angeachiwa tangu day 1 alipokamatwa!

Na bado, hata Mbowe alifikiri tatizo ni hilo jibwa lako la burigi ila alipokanyaga waya tu akajikuta ukonga, akabaki anashangaa inakuwaje tena wakati lile jibwa limekufa?

Sent from my SM-T295 using JamiiForums mobile app

Unateseka sana.”
 
Mimi kwangu nitaikumbuka jinsi hii kesi ilivyovutia,sidhani kama kuna kesi nyingine ambayo iliwahi kusikilizwa hadharani na kwa uwazi namna ile katika nchi yetu!
Tumeshuhudia jinsi Mawakili walivyochuana,tumeshuhudia jinsi waendesha mashitaki,wapelelezi wa serikali walivyokuwa wanajikanyagakanya na hata kutufanya tujue udhaifu wao.Tumeshuhudia baadhi ya Majaji walivyoikimbia kesi.
Katika hili nilikuwa naomba kesi zote ziwe zinasikilizwa kwa uwazi namna ile ili tujifunze mambo mengi yanayohusu Sheria.
Pongezi zangu ziwaendee Kibatala na Jopo lake!
Mimi nitapamisi sana pale RAU Madukani kwa Mama P. - pia Mo energy kwa mishikaki
 
Back
Top Bottom