Mbowe aachiwa huru na wenzake watatu baada ya DPP kuwasilisha hati ya kutotaka kuendelea na kesi

Mbowe aachiwa huru na wenzake watatu baada ya DPP kuwasilisha hati ya kutotaka kuendelea na kesi

Putin kalalamika kasema si vizuri kuendelea kumuwekea vikwazo vya kiuchumi - yeye ana nia njema na Taifa la Ukraine.

Vita baridi achana nayo, tayari imeshaanza kumwingia.
Bado mpaka atapikee..
 
Sasa hii imeletwa na people's power au religious leaders' power? Au people's power kupitia religious leaders' power? Je, sio kutokana na external influence/ pressure wakati wa safari ya Rais huko ughaibuni na kuja kudanganyia viongozi wa dini ambao waliwapanga wenyewe!?
muft walimsema vibaya lakini ndiyo aliyeleta matokeohayo bila muft kuomba ikulu mbowe angeozea jela
 
sawa, sasa unafikiri hiyo kesi ilikuwa na uhai kwa taifa letu? wote sisi tumefurahi sababau kesi kwanza ilikuwa inatuabisha kama taifa.

Tufike pahala watanzania tuwe serious na mambo ya msingi na tuachane na mambo haya ya kukomoana yanayotupotezea muda na heshima kama taifa,
Nadhan maelezo yako yanaji contradict nika learn kama unamtuhum mbowe kama ni gaid kitu ambacho si kwel.
 
muft walimsema vibaya lakini ndiyo aliyeleta matokeohayo bila muft kuomba ikulu mbowe angeozea jela
Mufti ni mbwa tu hana mchango wowote kwenye hili.Kwakifupi serikal imetengeneza haya maigizo iliwaonekane kama akina mbowe wameomba msamaha
 
Mungu wa mbinguni awabariki nyote.

Leo kuna Ibada ya Njia Ya Msalaba aliyopitia Bwana wetu Yesu Kristo kuelekea kwenye ukombozi wa Wana wa Mungu.

Ni imani yangu Simon wa Kirene atatuongoza!

Updates;

Nawatakia Chadema wote Ibada njema ya Njia ya Msalaba.

Mungu ni MWEMA wakati wote.

Jumaa kareem.

The End.
Toa unafiki wako hapa .
 
Baada ya upande wa Mashtaka kufunga ushahidi wao na kuialika Mahakama kutoa hukumu ndogo na kisha mahakama kuwakuta watuhumiwa na kesi ya kujibu mnamo Februari 18 2022. Leo 04, Machi 2022 ni siku ya watuhumiwa kuanza kujitetea kutokana na tuhuma wanazotuhumiwa nazo.

Awali Mahakama iliwakuta na kesi ya kujibu katika mashtaka 5 kati ya 6 katika kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili.

Kujua kesi ilipoishia fungua kiunganishi hiki:Mbowe na Wenzake 3 wakutwa na kesi ya kujibu. Kesi imeahirishwa hadi Machi 04, 2022 watuhumiwa kuanza kujitetea


=========

UPDATES

Jaji anaingia Mahakamani Muda huu Saa 4 na Dakika 52

Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Jamuhuri Dhidi ya Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe inatajwa hapa Mahakamani Muda huu

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Ikupendeze naitwa Robert Kidando Wakili wa Serikali Mwandamizi nipo na

Pius Hilla
Abdallah Chavula
Jenitreza Kitali
Nassoro Katuga
Esther Martin
Ignasi Mwinuka
Mawakili Wa Serikali Waandamizi Tulimanywa Majige
Wakili wa Serikali

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Ikupendeza naitwa Peter Kibatala nipo Pamoja na

Paul Kisabo
Sisty Aloyce
Gaston Garubindi
Iddi Msawanga
Evaresta Kisanga
Maria Mushi
Nashon Nkungu
John Mallya
Jeremiah Mtobesya
Fredrick Kihwelo
Dickson Matata Ni hayo tu mh Jaji.

Jaji: Shauri lilikuwa lina kuja kwa Utetezi, Je Mnazo habari zozote za Wateja wenu?

Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji ni kweli Kwamba Shauri lilikuwa limepangwa kwa ajili ya Utetezi Kwa Upande wangu tulifanya Maandalizi Mazuri Mimi John Malya, Dickson Matata, Fredrick Kihwelo na

Kibatala: wengine Juzi na Jana tulikuwa Ukonga na Segerea. Tulionana nao wakiwa na Bashasha kabisa, Kwamba Leo tunaendelea na Utetezi Lakini Leo Asubuhi tumepata Taarifa Kutoka Kwa Askari Magereza Kwamba Mbowe amepata Matatizo ya Ki Afya. Kwa hiyo hatuwezi Kuendelea,

Hivyo, Tunaweza Kupanga Kuendelea Jumatatu

Jaji: Jumatatu itakuwa Tarehe ngapi

Wakili Peter Kibatala: Tarehe 07 March 2022

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Shauri limekuja kwa ajili ya Utetezi, na tumewasikia Wenzetu Maombi Waliyo Wasilisha Sasa tusingependa Kujibu Hoja hiyo, Kwa sababu na sisi tuna Maombi Mengine Kwa hiyo Kujibu Hoja hiyo haitokuwa na Maana sana

Mheshimiwa Jaji tunaomba Moja la Kufanya Mbele ya Mahakama yako Na Ombi hili Mheshimiwa Jaji ni kwamba Mkurugenzi Wa Mashitaka (DPP) kwa niaba ya Jamhuri anaomba Kuwasilisha Taarifa ya Kutokuwa na Nia na Kuendelea na Shauri hili

Na Taarifa hiyo tunaitoa Chini ya Kifungu cha 91(1) kwa Sheria ya Mwenendo Wa Makosa ya Jinai

Jeremiah Mtobesya: Tumesikia Taarifa ya Notes hiyo kutoka kwa Mkurugenzi Wa Mashtaka, na Kwa Bahati Mbaya hatuwezi Kusema lolote zaidi ya Kusema tunaichia Mahakama, sababu Kifungu Kinatoa Maelezo Yote Kwamba Baada ya Kusema hivyo tunaichia Mahakama dhidi ya Amri zake za Mwisho

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Taarifa Hii tunaiwasilisha kwa Njia ya Maandishi, Kwa Maombi hayo ya Kifungu cha 91(1) tunaomba Kuondoa Mashitaka Yote dhidi ya Washitakiwa Wote Sababu zote zipo katika Noel Prosecui ambayo tumeiwasilisha

Wakili wa Serikali Robert Kidando: anapeleka Nyaraka Mbele ya Karani wa Jaji, na Karani anampatia Jaji

Jaji: Je umezungumza kwa niaba ya Defense Wote..?

Jeremiah Mtobesya: Mheshimiwa Jaji naomba kila Mmoja aseme

John Malya: Mheshimiwa Jaji notes iliyotolewa inayushuka Mikono wote, pamoja na Kujiandaa kwa ajili ya Kujitetea, Mikono yetu imefungwa na hatuwezi Kusema lolote, Tulitaka sana Warudishe Gharama zetu na Mengine lakini wacha Tusubiri Maamuzi ya Mahakama

Fredrick Kihwelo: Kwa niaba ya Mshtakiwa wa tatu Tumesikia Taarifa iliyotolewa, Tunaichia Mahakama iweze Kutoa Amri

Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Na sisi tunaichia Mahakama, Sheria inajielezea wazi.. Mahakama ipo Kimya Kidogo na Jaji Bado anaandika

Kule Nje ni Kelele za Shangwe na Fifijo watu Wanaimba, Imebidi Mahakama Kufunga Vioo Vya Madirisha ili Kuzuia Kelele Kuingia Mahakamani, Wewe furaha yako ni Kiwango gani? Onyesha emoji ya furaha hapa Chini.. Au picha yako ukiwa na furaha kubwa..

Jaji: Baada ya Mahakama Kusikiliza Hoja iliyoletwa na Wakili Mwandamizi wa Serikali Kwamba Mkurugenzi wa Mashtaka hana nia ya Kuendelea na Kesi, na Upande wa Pili wakaridhia

Mahakama inasema Shauri hili lililo kuwa linawakabili Washitakiwa Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe inatajwa nakiondosha Mahakamani na Washitakiwa Wanaachiwa huru bila Masharti, sababu Kuna Vielelezo vililetwa Mahakamani, naandaa Amri ya Kuviachia

Jaji: Na hivyo naelekeza Mkuu wa Magereza Kuwaachiwa Mara Moja, Leo na si Vinginevyo Natoa Amri Jaji anatoka Mahakamani Mahakama inaridima Kwa Shangwe.

=======
Freeman Aikael Mbowe na wenzake watatu, wameaachiwa huru leo, na Mahakama kuu Divisheni ya makosa ya uhujumu uchumi na Rushwa, Baada ya DPP Kuwasilisha hati ya kutokuwa na nia ya kuendelea na shauri hilo, leo 4.3.2022. Hivyo, Freeman Aikaeli Mbowe

Mungu ni mwema mnoo tena nyakati zote na jina lake lihimidiwe. Kwa upande mwingine, hata kama ni kwa kuchelewa, huku ni kuonyesha ukomavu wa hali ya juu wa Rais Samia. Wewe sasa unaingia kundi la viongozi wasioamini katika kukomaza shingo bila tija. Ni personal sacrifice Rais anafanya kwa sababu ni kinyume na matamshi yake BBC. Tulijua Rais alidanganywa. Hongera kwa wapenda nchi yetu, wapenda demokrasia wote na watu wote wakweli. Sasa Rais Samia tuko nyuma yako na usituangushe tena katika Masuala sensitive kama haya. Itoshe kusema CHADEMA ni kubwa sana kuliko tunavyodhani. Lazima kukaa nayo kwa hekima zaidi. Kazi iendelee na Mh Mbowe karibu mno kijenge Tanzania mpya.
 
Usiwe kama mtoto mdogo!

Siku zote ccm huwa inawakomesha tu wapinzani wake.

Na hapa wala hata msisgangilie kwamba mmeshinda bali mnapaswa kujilaumu na kujiuliza kwamba inakuwaje ccm inawageuza geuza kama chapati namna hii!?

Sent from my SM-T295 using JamiiForums mobile app

Kwahiyo vyombo vya dola ndio CCM?
 
Hakuna mtu nilikuwa namsubiri kwa hamu kwenye hii kesi aabike humu ndani kama Crimea, maana alikuwa ananichefua mno na akili zake mbovu..!

anyways, Namshukuru Bwana Yesu Leo nimetoa chozi la furaha..!
 
Bavicha nyie ni vichwa maji kweli kweli[emoji23][emoji23][emoji23]

Mtu wenu anasota gerezani mwaka mzima alafu walewale watesi wake wanakuja kusema aahh hatuna nia na kuendelea na kesi alafu nyie mnaanza kushangilia? Kama si uzuzu ni nini?

Sent from my SM-T295 using JamiiForums mobile app
Kwa hiyo all these days unafurahia wengine kuteseka kwa sababu tu mna uwezo wa kutesa watu kwa kutumia madaraka mliyopewa!!!! Mungu atawalaani wote.
 
Hakuna mtu nilikuwa namsubiri kwa hamu kwenye hii kesi aabike humu ndani kama Crimea, maana alikuwa ananichefua mno na akili zake mbovu..!

anyways, Namshukuru Bwana Yesu Leo nimetoa chozi la furaha..!
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Mkuu, kwani mimi nmeaibikaje labda?

Sent from my SM-T295 using JamiiForums mobile app
 
Hakuna mtu nilikuwa namsubiri kwa hamu kwenye hii kesi aabike humu ndani kama Crimea, maana alikuwa ananichefua mno na akili zake mbovu..!

anyways, Namshukuru Bwana Yesu Leo nimetoa chozi la furaha..!
anyways, Namshukuru Bwana Yesu Leo nimetoa chozi la furaha..![emoji1533][emoji1534]
 
Sasa baraza kuu likakutane ASAP wakamalizie kile kiporo cha wale wanawake 19, nako mbivu na mbichi zijulikane.
 
Back
Top Bottom