Mbowe acha kutetea watu wapumbavu

Mbowe acha kutetea watu wapumbavu

Unadhani mimi ni wa siasa nyepesi za usukuma nansukuma gang boss? Tazama hii id vizuri, kisha waulize wenzio hapo Lumumba watakupa maelezo ya kutosha.
Kama mwanasiasa ndio wewe wanakutengemea basi kwa taarifa yako huna uwezo wowote. Nimekuuliza kati ya Lema na Mbowe nani anafaa? Unaruka ruka tu.
 
Wabongo ni taifa la wapumbavu

Leo hii Mbowe alianza kutumia pesa za baba yake kujenga chama miaka ya 2000 leo ndiye anaitwa mlamba asali?

Mbowe mwaka 2005 alikodi helicopter kuzunguka nchi mzima wakati chama hakina hata ruzuku leo watu wanasema kalamba asali?

Aisee Mbowe kavunjiwa club yake kwa sababu ya kupigania wapumbavu

Account zake zikafungiwa kisa wapuuzi

Halafu mwisho akafungwa sababu ya wapuuzi na kupewa kesi ya ugaidi!! Shame

Mbowe toka mwaka 2000 mpaka leo miaka 23 kashatumia pesa kiasi gani toka mfukoni mwake?

Mbowe angekuwa mlamba asali Basi angeilamba kwenye utawala wa Magufuli ambaye aliwanunua wabunge 19, Kafulila na wenzie wote walipewa ubunge na uwaziri!! Lakini pamoja na kuwekewa dau la billion 5 na Magufuli akiuze chama ili aweke mwenyekiti mamluki kama ilivyo kwa vyama vyote vingine vya upinzani alikataa na kuendelea kupigania wapumbavu.

Msimamo wa Mbowe upo wazi kabisa anataka Katiba mpya, Tume huru ya uchaguzi, My control Mfumuko wa bei, Nchi kutokopa ovyo, Uhuru wa vyombo vya habari, Kushughulikia Deni la taifa!!!

Wabongo wanataka siasa za majitaka za kutukana siasa hizo hazina nafasi Dunia nzima siasa za Sasa ni hoja !!!

Pia watanzania wengi wameanza kufatilia siasa za upinzania miaka ya utawala wa Magufuli.

Nchi hii ina watu wapumbavu Sana nashauri Mbowe aachane na kutetea wapuuzi
Mods mnaachaje Uzi wenye kichwa Cha habari Cha lugha ya kuudhi Kwa matusi? Mna maslahi gani?
 
Kama mwanasiasa ndio wewe wanakutengemea basi kwa taarifa yako huna uwezo wowote. Nimekuuliza kati ya Lema na Mbowe nani anafaa? Unaruka ruka tu.

Hakuna anayefaa, inaonekana ndio umeanza kujua siasa sasa, hii ndio iliyopelekea ulete ule utoto wako wa sukuma gang. Na ndio maana unawajua wanasiasa wawili tu, Mbowe na Lema.
 
Hakuna anayefaa, inaonekana ndio umeanza kujua siasa sasa, hii ndio iliyopelekea ulete ule utoto wako wa sukuma gang. Na ndio maana unawajua wanasiasa wawili tu, Mbowe na Lema.
Haya tutajie badala ya mbowe mnataka awekwe nani? Mnyika, Lissu au mmoja wa covid-19?
Hebu toa ya moyoni mdogo wangu.
 
Huhitaji kupanick labda kama unafaidika binafsi na Mbowe. Ni kweli Mbowe amefanya mazuri ndani ya CDM, lakini kwa sasa amefika mwisho na anaanza kuharibu mazuri yake yote. Kwa taarifa yako Mbowe amefaidika sana na CDM kuliko alichotoa, japo ni kweli pesa zake zilisaidia sana kwenye ujenzi wa chama hapo awali.

Lakini kwa kiwango kikubwa Mbowe ameshindwa kuibadilisha Cdm hasa upande wa miundombinu kama ofisi nk. CDM sio chama cha kukosa ofisi yenye hadhi ya chama hicho, na ofisi 1 kila mkoa. Tukubaliane tu kwa sasa Mbowe ameshafikia mwisho wake. Tunakuomba umshauri kiroho safi kuwa akae pembeni maana sisi wafuasi wake hatuna imani naye. Huko CCM ndio kuna tabia ya kufumbiana macho kwa kiongozi akichemsha.
[emoji848][emoji848][emoji848]
 
Haya tutajie badala ya mbowe mnataka awekwe nani? Mnyika, Lissu au mmoja wa covid-19?
Hebu toa ya moyoni mdogo wangu.

Sikuanza juzi kusema Mbowe hafai, toka ampokee yule mzee muhuni wa siasa Lowassa, nilisema hapana. Nafasi ya uenyekiti ni sahihi kupewa Heche, na Lisu Makamu. Hao COVID-19 wakae na Mbowe wamalizane.
 
Mbowe ni kiongozi yuko sahihi kutoa mwelekeo wa chama chake kwa misingi ya maridhiano, angalau CDM mnaweza kuitikisa CCM ili mradi mwende nayo kisayansi siyo kimabavu hamtaiweza zaidi ya kuishia kukimbilia nje ya nchi uhamishoni.
 
Sikuanza juzi kusema Mbowe hafai, toka ampokee yule mzee muhuni wa siasa Lowassa, nilisema hapana. Nafasi ya uenyekiti ni sahihi kupewa Heche, na Lisu Makamu. Hao COVID-19 wakae na Mbowe wamalizane.
Kwahiyo wewe ni timu heche!!! Sasa kwaakili hiyo ndiyo unajitapa mwanasiasa mbobevu. Nakusihi uachane na siasa maana unamihemko mizito sana.
 
Mbowe ni kiongozi yuko sahihi kutoa mwelekeo wa chama chake kwa misingi ya maridhiano, angalau CDM mnaweza kuitikisa CCM ili mradi mwende nayo kisayansi siyo kimabavu hamtaiweza zaidi ya kuishia nje ya nchi uhamishoni.

Hakuna anayetaka maridhiano ya kitapeli. Kiongozi anayeendekeza maridhiano ya kitapeli hatumuelewi. CCM hawana mabavu yoyote zaidi ya kutegemea mbeleko ya vyombo vya dola. Kama Mbowe anataka maridhiano na ccm, afanye maridhiano hayo kimpango wake.
 
Kwahiyo wewe ni timu heche!!! Sasa kwaakili hiyo ndiyo unajitapa mwanasiasa mbobevu. Nakusihi uachane na siasa maana unamihemko mizito sana.

Yaani hapa ndio utajua umeingia penyewe, lazima ukae babu. Kama hata wasukuma wamegoma kufuata maagizo yenu kundi haramu la sukuma gang, basi utajua hujui.
 
Wale wasukuma uliokuwa unawatambia jana naona leo wamegoma kufuta matamanio yako. Hakika leo wasukuma wameamua kujitenga na kiongozi muovu na wamejitokeza kwa wingi.
Unaujua uhalisia wa kilichotokea pale Furahisha,uzuri nilikuwepo Live kwakuwa mimi nipo hapa hapa Mwanza. Endelea kulumbana na Makamanda wenzio huku ukimtolea povu M/Kiti.Hii ndiyo Mwanza na nilikutahadharisha haitowaacheni salama.Vipi kuna nani alifunua mdomo wake kutamka hata neno Sukuma Gang?
 
Mwandishi unachomaanisha mbowe asipiganie wapumbavu ni kwa sababu ya mapokezi kiduchu leo?
 
Back
Top Bottom