Nimesoma comments nyingi humu sijaona hata mmoja kati yenu aliyejiuliza kwanini Mbowe amefanya mkutano wa uchaguzi wa aina hiyo, wote mnabwabwaja tu!.
Video yenyewe iliyowekwa hapo ni kipande kifupi, kisicho na maelezo yoyote kabla nini kilisababisha Mbowe akaamua kufanya uchaguzi wa aina hiyo.
Mihemko tu imewatawala wengi wenu kuanza kumponda Mbowe, kama vile mna stress za maisha yenu mnaamua kummalizia yeye, pambaneni na hali zenu.
Mngekuwa na akili zinazofanya kazi mngejiuliza kwanini Mbowe amefanya hivi, mkipata jibu lisilowaridhisha ndio muanze kumpinga, sio mnakurupushwa na mleta mada mnajaa wazima kama samaki ķwenye nyavu!
Nyie ndio GT's!.
Hamjiulizi sasa hizi Chadema wanafanya chaguzi za kanda, huo uchaguzi wa Handeni ni wa kanda? kijiji, kata, au mtaa? muda wake ulishapita au bado? kama muda ulipita bila uchaguzi kufanyika mlitaka paachwe hivyo hivyo? au waendelee kuvuta muda kujiandaa kwa uchaguzi na kutumia resources za chama?
Muwe mnajiuliza sababu ya jambo, sio kukurupuka tu kwa makelele ya hasira.