Mtu Wa Aina Hii Ndio Aje Kuwa Rais Jamani? Mbona Nchi Hii Itakuwa Imekwisha Mpaka Hapo Atakapokuwa Wamepatikana Viongozi Wa Kweli,awamu Ya Tatu Wameharibu Ya Nne Pia Na Hao Ambao Tungetarajia Waje Watuwekee Nchi Sawa Ndio Hawa
mi hapa sijui nisemeje? kama DR. Slaa alivyojitokeza kukanusha huyu naye aje.....!
Ndio maana wa Chadema wanaukimbia Uraisi ,hapa mlikuwa mnasifu moshi kumbe ndani kuna cheche , vishindo vya Mbowe sasa basi ,amemwagiwa maji ya barafu ,daha ukiziba huku kunatoboka kule ,wamebaki wanaume wa kazi wanangangari wazee wa shwa shwa shwa ,mapangaaa shwa shwa shwa ,ipo kazi nasema ipo kazi kwa sababu hivi sasa njia ni moja tu ,iungeni mkono CUF bila ya kusita hakuna Chadema hakuna TLP ,na ndio ukweli mnauona huu ,usingoje kushikwa mkono ,tunataka kuingoa CCM kwa kishindo ,hivyo TLP CHADEMA na wengineo elekezeni nguvu zenu kuipa sapoti CUF katika ngazi ya Uraisi ,Lipumba he is a man to be na anastahili kwa kuwa kila sifa ambazo ni kigezo cha Urais anazo ,sisemi kuwa hao wengine hawafai ,hapana CCM ameshawaona na kuwavuruga ,wameitafuta kwa kila njia CUF lakini wameshindwa ,tena wameshindwa vibaya sana katika harakati za kuikwamisha CUF ,kila wanapojaribu wanakutana na kizingiti na hua ndio mwisho wao ,inawabidi wajipange upya mwisho wameona wahamie kwa Chadema na TLP na wengine ,Chama Cha Wananchi CUF kitawaongoza WaTanzania pale wanapopataka hilo halina mjadala.
Mbowe hotel yadaiwa bilioni 58.7/- za NSSF
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
MBOWE Hotel Ltd ni miongoni mwa wakopaji wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), ambao hawatekelezi masharti ya mikopo na kusababisha malimbikizo ya deni la jumla ya sh. bilioni 58.757.
Akitangaza taarifa ukaguzi, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh, alisema deni hilo limesababishwa na wakopaji kumi.
Kwa mujibu wa ukaguzi wa CAG, wakopaji hao ni Mbowe Hotel Ltd ambaye Machi 10, 1990 alikopa NSSF sh. milioni 7.5, lakini alishindwa kulipa deni na kusababisha limbikizo la riba ya sh. 229,898,516.
Alisema hadi Juni 30, 2008, deni la riba kwa hoteli hiyo lilifikia sh. 237,398,516. Wadaiwa wengine ni New Kilimanjaro Bazaar, ambaye kati ya mwaka 1990,1991 na 1992 alikopa jumla ya sh. 99,445,000.
Utouh alisema kuwa riba ya mkopaji huyo ilifikia sh. milioni 750.849 ambapo jumla ya riba na deni imefikia sh. milioni 850.294. Wakopaji wengine ni Kagera Sugar Company Ltd, ambayo Februari 11, 2003 ilikopa sh. milioni 12 na riba ya deni hilo ni sh. bilioni 5.624, ambapo pamoja na deni ni sh. bilioni 17.624.
Kampuni zingine zinazodaiwa na kiwango cha fedha kwenye mabano, ni General Tyre East Africa (sh. 13,502,430,000), KATANI LTD (sh. 5,090,220,000), Continental Ventures (sh. 4,963,822,411).
Wengine ni EMUNIO Tanzania Limited (sh. 1,770,089,625), Kiwira Coal & Power Company Limited (sh. 8,967,450,000) na Tanzania Portland Cement Company (sh. 5,751,799,404).
Wakati huo huo Utouh amemsafisha Spika wa Bunge, Samuel Sitta, kwamba madai kuwa alitumia vibaya fedha za serikali kwa ajili ya matibabu hazikuwa sahihi, kwa kuwa ukaguzi ulionyesha malipo yote yalifanyika halali.
Wazo:
Ninachoweza kusema nikuwa wakati mwingine siasa inaweka pazia katika reason. I can't wait kwa Mbowe kuwapiga mkwara Uhuru na kuwataka waiombe radhi MH. Kwa upande mwingine, katika hali hii ngumu ya kiuchumi na tukifuata mfano wa wakuu wa ubepari je haiwezekani kufanya settlement na makampuni yanayohusika ili hatimaye hii taarifa (ambayo ilikuwemo tangu ripoti ya 2006!) isirudiwe tena 2008/2009? On the other hand, mtu kakopa milioni 9 riba inakuja kufikia milioni 230! Huu siyo wazimu, hata kamamimi wallahi silipi! Yamekuwa mambo ya kina Merchant of Venice!?
- Kwamba Hoteli ya Mbowe inadaiwa hilo halina utata.
- Kwamba gazeti limeandika inadaiwa bilioni 58 (jumla ya madeni ya wengine wote) ni msingi mzuri wa kulifungulia mashtaka na kulitaka lilipe na kuomba radhi kwenye ukurasa wa mbele!
- Kwamba, ingawa mtu yeyote akisoma kwa haraka anaweza kuona kuwa kati ya wakopaji wote 10 wanaodaiwa madeni hayo makubwa, la Mbowe ndilo la kiwango cha chini zaidi (milioni 230 hivi); so kwanini habari ni ya mbowe badala ya Bazaar (anayedaiwa milioni 800, au Kiwira inayodaiwa karibu bilioni 9!?)
Kama 'Dr' Masau alivyokuwa anadaiwa...dawa ya deni Mbowe alipe tuuu
Wadau mimi ni an apologetic CCM member but this is a STUPID piece of news,Mbowe hotel yadaiwa bilioni 58.7/- za NSSF

Sorry bado sijajua hili ni gazeti gani. Can someone tell me?
dawa ya deni kulipa