Mbowe ahusishwa na UFISADI wa kuimaliza NSSF

Mzee wa Rula,
Hilo jungu lako lina kaukweli kidogo. Habari hizi ziliripotiwa katika gazeti moja la Bongo zikitolewa na NSSF. Baada ya gazeti kubaini ukweli ilibidi wamwombe Mbowe msamaha. Ndio maana zimebaki habari za kibarazani.
 
Ungewauliza huko huko kibarazani wakupe ripoti kamili kabla ya kukimbilia hapa JF.

Msome mwenzio MsandoAlberto kajibu nini. Kwani hapa si barazani? Kama hujafanya ujasusi vizuri ngoja nikujuze, na hiki ni kibaraza cha porojo kama vingine tu. Bisha na hilo pia.
 
Msome mwenzio MsandoAlberto kajibu nini. Kwani hapa si barazani? Kama hujafanya ujasusi vizuri ngoja nikujuze, na hiki ni kibaraza cha porojo kama vingine tu. Bisha na hilo pia.
MsandoAlberto ni mwuungana. Mimi sina subira na the likes of you. Nakupa hapo hapo.
 

Ahsante sana nimekupata, jee kama hajalipa mkopo? Credibility bado ina kuwepo? Au ndio inakuwa kama Serikali ya Tanzania kwa NBC kama ulivyo elezea hapo juu?
 
Search kwenye archives za JF, utakuta thread zaidi ya mbili on this issue. Unanikausha maji mwilini.

Mbowe Hotels Limited ina wanahisa na Freeman Aikael Mbowe ni mmoja wa hao wanahisa.
 
MsandoAlberto ni mwuungana. Mimi sina subira na the likes of you. Nakupa hapo hapo.

Hujajibu swali hata moja na sijaona ulichonipa hapo hapo, pumba? Au utumbo? Jibu swali, na hapo juu kuna ka swali ka ziada, au huwa huzi-jasusi hizi post, unajisemea tu?
 
For the record, deni lilikuwa Mil 15, Mbowe Hotel Ltd imelipa Mil 80 ikiwa ni deni na riba yake. Huyo aliyekwambia MHL ilikopa mamilioni muulize ni mamilioni kama ya kagoda, epa, deepgreen au?
 
Search kwenye archives za JF, utakuta thread zaidi ya mbili on this issue. Unanikausha maji mwilini.

Mbowe Hotels Limited ina wanahisa na Freeman Aikael Mbowe ni mmoja wa hao wanahisa.

Ni mmoja wao au ndio major share holder na wengine ni mkewe na wanawe? Sema kweli bana!
 
For the record, deni lilikuwa Mil 15, Mbowe Hotel Ltd imelipa Mil 80 ikiwa ni deni na riba yake. Huyo aliyekwambia MHL ilikopa mamilioni muulize ni mamilioni kama ya kagoda, epa, deepgreen au?

Kwa hiyo kamaliza deni lote na sasa hadaiwi?
 
JF (Jukwaa la Siasa) sio kibaraza la porojo. Huwezi kufanya porojo na shida za watanzania. Lazima ufike mahali ujitambue na utoe mchango wako kwa taifa hili. Hata kama wewe si mwanaCDM. Toa hoja zinazojenga chama chako. Porojo na hadithi wakati sasa hivi kuna mtoto amelala bila kula chochote au amekunywa uji sio sahihi. Jaribu kufikiria tena matendo na maneno yako yanamsaidiaje mtoto huyo!
 
Msando, na hiyo nyumba iliyowekwa dhamana ilikuwa ni ya MHL?
 
yakheeeee hiloo baraza la ghahawa au la miraaaaaaaaaaa shekhe?
 
Mzushi, mzandiki, mchochezi, mchonganishi..........waliokutuma waambie wajibu hoja zinazowatafuna kanda ya ziwa.
 
Watoto wake sio wanahisa, Dr. Lilian Ndefumiro Mbowe ni mwanahisa pia. Hakuna anayekataa kwamba Freeman Mbowe ni mwanahisa. Hakuna anayesema MHL haikukopa. Soma majibu yangu utaelewa kama uwezo huo unao. Mgogoro wa kiasi gani kimelipwa na kiasi gani kilipwe haujaisha. Ila sheria iko wazi kama mtu ameshindwa kulipa deni unauza dhamana iliyotolewa. Wasipofikia muafaka ndicho kitakachofanyika. Kwa heri. Utaniambukiza ujinga kamanda.
 

Samahani kama unaogopa ujinga, lakini, kumbe ni kweli ni Mbowe tena leo nimepata mpya kutoka kwako, na Mkewe, na deni bado wanadaiwa.

Duhh, ingekuwa hujaaga ningekuuliza hivi huyu Mbowe hana ndugu? Hata hiyo MHL iwe kwa jina lake na mkewe tu? Si ilikuwa ya urithi hiyo? Sasa warithi wenzake mbona hawamo?
 
Ni kweli Mbowe anadaiwa, jamaa ni mfanyabiashara na kukopa ni sifa ya mfanyabiashara makini. Serikali yetu imekopa benki za nje na ndani na huku ni kuweka kikwazo kwa wakopaji wadogo na wa kati. Mbowe ana shauri linaloendelea katika mamlaka ya nssf na biashara nadhani ni kuhusu riba. Tafadhari usipende kusikiliza mambo yatakayokufanya kuwa mseng....enyaji.
Nadhani unapaswa ujue kuwa kufanya biashara kikamilifu na kwa tija inakupasa ukope
 
Halafu tunalalamika akiba za wazee hazilipwi kwa wakati, wakati kina Mbowe na familia zao wanakopa akiba zetu za uzeeni halafu hawataki kulipa, eti biashara haikwenda vizuri! Juzi tu kazowa kitita kisichopunguwa million 90 bungeni, kwa nini asilipe deni lake na mkewe, ili ahakikishe akiba zetu za uzeeni haziendi mrama?

Leo tuna kauli ya kusema hawa ndio viongozi wanaofichuwa ufisadi? Hata haya hatuna!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…