Mbowe ahusishwa na UFISADI wa kuimaliza NSSF

Mbowe ahusishwa na UFISADI wa kuimaliza NSSF

Wafanya biashara makini na wenye uwezo wa kuendesha biashara zao, hukopa na hulipa na kukopa tena na kurudisha. Lakini mfanya biashara Mbowe hilo kashindwa, yaani kashindwa kuongoza biashara ataweza kuongoza watu million 40?
Nilijuatu tu tangu mwanzo kwamba lengo lako ni kuhoji uwezo wa Mbowe kama kiongozi. Eti kashindwa kuongoza biashara ataweza kuongoza watu milioni 40? My foot! Uzumbukuku tu. Kama Mbowe angekuwa kiongozi aliyeshindwa tusingekuwa tunamwongelea hapa JF. Mbona hujaleta mada ya Lipumba au Mrema kama viongozi? Kwa sababu hawa ni dhahiri wameshindwa. Lakini hatupotezi muda wetu kuwajadilia. Lakini Mbowe anawakuna wote wale wanaotetea mafisadi.
 
Kuna mmoja humu alisema anadaiwa Million 15 tu, pamoja na riba zinakuwa 80 na kazilipa. Kumbe alikuwa anachakachuwa ukweli ni
[FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]*Adaiwa milioni 1200, hataki kulipa".

Hiyvo naona ni vingi kuliko vijisenti.

[/FONT]
 
Hii si mada ya Rostam na Kikwete. Hii ni mada ya Mbowe na Mkewe kukopa na kuvinjari kulipa, tena fedha za akiba ya uzeeni, wenzako juu huko wamesema ni kweli kakopa kupitia kampuni anyoimiliki yeye na mkewe MHL, na kweli bado analeta utata katika kulipa, si kwa sababu hana pesa, kwani tumesikia juzi-juzi wabunge wamepewa donge nono tu, tena yeye kwa kuwa ni Kiongozi wa upinzani (au Chadema) bungeni, ina maada ana visenti vya ziada vya marupu-rupu, si alipe tu akiba zetu?
You know what ? Do your damnest. Sisi tunaendelea kusonga mbele mpaka kieleweke! Kama mnadhani mna uwezo wa kumwangusha Mbowe basi ninyi ni kama wale fisi wanaomfuata binadamu wakifikiria kuwa mkono wake utadondoka karibuni wapate mlo.
 
Wafanya biashara makini na wenye uwezo wa kuendesha biashara zao, hukopa na hulipa na kukopa tena na kurudisha. Lakini mfanya biashara Mbowe hilo kashindwa, yaani kashindwa kuongoza biashara ataweza kuongoza watu million 40?

Kama mkopeshaji kalala hadai deni katika biashara hutakiwi kuhangaika kumlipa....biashara nzuri ni ile unayotumia pesa za wengine..ndio maana makampuni yana Credit controllers na wala hayana Debt Controllers .Sasa toka 1990 haoCredit controllers wa NPF walikuwa wapi?
 
Mbowe ana akili sana. Anajua ni vigogo wangapi wana mikopo zaidi yake na hawajalipa. Afterall anadaiwa riba tu! Ila kama kiongozi wetu inabidi afafanue hili tumwelewe
 
Hivi hapo anachafuliwa? au?

Kukopa fedha zetu za akiba ya uzeeni halafu asilipe halafu useme anachafuliwa? unashangaza kweli kweli. Naona hapo tope kajisiriba mwenyewe na mnaomtetea mnazidi kulitapakaza!

Kukopa pesa na kushindwa kulipa ni kitu ambacho huwa kinatokea. Lakini cha kujiuliza hapo ni kwamba je njia au taratibu zinazo julikana kisheria ndizo zilizo tumika kumpa bw. Mbowe mkopo? na je taratibu hizo pia zinatumika kurudisha (loan recovery) mkopo?
Lakini kwa vyovyote vile mbowe hawezi kuwa sawa kuifisidi nchi kama anavyofanya Rostam, Lowassa na Kikwete.
 
Ahh basi kwa madeni makubwa hivyo napata picha kamili... Labda anafikiri kwa kuwa Rais wa nchi ataweza kulimaliza deni. Asilaumiwe jamani kwa mihangaiko ya kila namna anayoifanya katika kutafuta upenyo wa kuingia ikulu hali ya kuwa uchaguzi 2015 sio leo wala kesho...

Ninavyofahamu mimi amebakiza kulipa interest tu Principal amount alilipa,Tusi weke ushabiki,NSSF wanakopesha miradi mbalimbali ukiwa na writeup nzuri unapata pesa,mashirika na taasisi mbalimbali huwa zinakopa huko,fanya uchunguzi wa kina utaona mengi kwa kuwa Mbowe ni mwanasiasa basi akifanya chochote ni habari.
 
hoja ni kuwa kampuni ya mbowe ilikopa mkopo nssf kwa uwazi; na ikalipa mkopo huo kwa uwazi-japokuwa riba ilivyotakikana kwa mujibu wa mkatapa haijalipwa timilifu. Unkiangalia kimsingi deni la million 15 (1993) lilishalipwa (kwa mikupuo mitatu million 3, million 12, million 50) sasa kama bado anadaiwa tu kwa mujibu wa mkata riba ya deni; huko ni kumkamua mtu hadi damu kitu ambacho hakifai kabisa. Hapa Riba ndo mgogoro na inataka kutumiwa KISIASA!!! Lakini kwa ukweli kampuni ilijitahidi kulipa kadri ilivyoweza. Madeni ya namna hii ndo nchi changa huwa inayakataa kulipa nchi tajiri kwa kuwa RIBA ni kandamizi!!!
 
Maandiko matakatifu katika Biblia yanasema ASIYEMWAMINIFU KATIKA LILILO DOGO HAWEZI KUWA MWAMINIFU KATIKA LILILO KUBWA. Kama amekosa uaminifu katika kulipa deni lililo dogo hawezi kuwa mwaminifu hata akipewa madaraka makubwa katika nchi. Hapa inamaanisha kwamba Mbowe ni tapeli. Anaposema kampuni yake ndiyo inadaiwa si yeye ni utapeli. Siku ya mwisho kampuni yake inapolipa dividends ni yeye ananufaika. Sasa anatuambia hahusiki ki vipi. Huyu naye ni TAPELI NA FISADI PAPA! Tusiwaonee haya kuwaambia ukweli kwa vile tu ni wachama cha vuguvugu la mabadiliko.
 
attachment.php

Ndugu Freeman Mbowe akiwa na mkewe ambaye ni binti wa aliyekuwa gavana wa BOT enzi hizooo na pia mwanzilishi wa Chama kikuu cha upinzani Tanzania CHADEMA ndugu EDWIN MTEI

Huyu ni rais wetu mtarajiwa in October 2015

Sasa nauliza je alimaliza Masomo yake kule Hull University?

Na je alishalipa deni lake alilokuwa anadaiwa na NSSF?

Je ali declare mali zake hadharani au?
 
Attachments

  • mbowe wife.jpg
    mbowe wife.jpg
    293.5 KB · Views: 635
What is the deni got to do with urais wake? elezea na madeni ya walioko madarakani sasa, tuone nani zaidi.Acha kuleta hoja za kuchafuana hapa.
 
What is the deni got to do with urais wake? elezea na madeni ya walioko madarakani sasa, tuone nani zaidi.Acha kuleta hoja za kuchafuana hapa.

Waliopo madarakani wote wana madeni na wengi wao wana njaa

sasa kuna ubaya gani tukajua hali ya mfuko wa rais wetu mtarajiwa?

je vipi alimaliza masomo kule UK?
 
attachment.php

Ndugu Freeman Mbowe akiwa na mkewe ambaye ni binti wa aliyekuwa gavana wa BOT enzi hizooo na pia mwanzilishi wa Chama kikuu cha upinzani Tanzania CHADEMA ndugu EDWIN MTEI

Huyu ni rais wetu mtarajiwa in October 2015

Sasa nauliza je alimaliza Masomo yake kule Hull University?

Na je alishalipa deni lake alilokuwa anadaiwa na NSSF?

Je ali declare mali zake hadharani au?
2015 presidaa and festi ledi discussing issues of tribal importance
 
attachment.php

Ndugu Freeman Mbowe akiwa na mkewe ambaye ni binti wa aliyekuwa gavana wa BOT enzi hizooo na pia mwanzilishi wa Chama kikuu cha upinzani Tanzania CHADEMA ndugu EDWIN MTEI

Huyu ni rais wetu mtarajiwa in October 2015

Sasa nauliza je alimaliza Masomo yake kule Hull University?

Na je alishalipa deni lake alilokuwa anadaiwa na NSSF?

Je ali declare mali zake hadharani au?

Kajipange upya. Huyu si mke wa Freeman Mbowe!
 
Kamanda atajitokeza tuu na mwamini aje kujibu maswali yanayomhusu
 
Back
Top Bottom