Wadau, baada ya kipindi cha Maswali na Majibu, kulikuwa na miongozi ya Wabunge kwa Naibu Spika. Moja ya hoja zilizojitokeza ni madai ya Lissu kuwa Wabunge wa CCM wanachukua fedha kutoka kwenye mifuko ya jamii. Hata hivyo, waziri Gaudensia Kabaka alisema kuwa si kweli kuwa wabunge wanaenda kuchukua fedha kwenye mifuko ya kijamii na kuweka mfukoni mwao bali wanaomba fedha kwenye mifuko hiyo kwa ajili ya maendeleo kwenye majimbo yao. Alisema kuwa ni wabunge wa CCM ndio wanaojitokeza kuomba kwa ajili ya majimbo yao jambo ambalo amesema kuwa ni jema. Anawashangaa wabunge wa upinzani kulalamika kuwa wabunge wa CCM wanaomba fedha kwenye mifuko yao ilhali wao hakuna anayewazuia kuomba.
Kibaya zaidi waziri Kabaka alisema ni pale Mbunge ambaye anajitokeza kuomba fedha kwenye mifuko hiyo na akakaa na deni kwa muda mrefu hali inayomfanya awe kwenye risk ya kukamatwa na kufunguliwa mashtaka. Alisema kuwa kuna kiongozi mmoja wa upinzani ambaye amekpa fedha nyingi NSSF na mpaka sasa anakwepa kulipa. Katika majibu ya nyongeza, Waziri wa TAMISEMI, HAWA GHASIA alimtaka mtu huyo kuwa ni Freeman Mbowe, Kiongozi wa Kambi ya Upinzani ambaye alitumia mamlaka yake kama KUB kukopa kiasi kikubwa cha fedha (kiwango hakikubainishwa) na mpaka sasa hajalipa na haoneshi nia ya kulipa hivyo kujiweka kwenye uwezekano mkubwa wa kukamatwa