Ben Saanane
JF-Expert Member
- Jan 18, 2007
- 14,580
- 18,193
Hivi huu utitiri wa thread zinazofanana una tija kweli? Hivi kwani hizo pesa Mbowe anachukua na kukunjia mfukoni tuu?hakuna utaratibu wa receipt
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hivi huu utitiri wa thread zinazofanana una tija kweli? Hivi kwani hizo pesa Mbowe anachukua na kukunjia mfukoni tuu?hakuna utaratibu wa receipt
Mkubwa mbona rahisi sana
utitiri wa ufisadi wa CCM mbona unazidi thread zaidi ya 500 kwanini isingekua thread moja tu?
sembuse hizi chadema tano ama kumi uziite utitiri.
Mkuu,
Two wrongs cant make one right!
Halafu CHADEMA si ndio watatakiwa kulitolea tamko?
Mkuu
kunakitu kinaitwa Transparency mimi hoja yangu ndio ipo hapo.
Je walifuata taratibu za kisheria kukopeshana na kulipana?
Hapa wanatakiwa waonyeshe umahili kwa uwazi ya kwamba wanapo kikopesha chama lazima waweke mambo wazi kumbuka hapo si mambo ya mtu binafsi wala kujitolea ,kama kujitolea wasingetaka kurudishiwa fedha.
Hiyo Tenda ya kudhamini chama waitangaze wazi kama ni tenda ya kutokua na faida ama yenye faida ama ya kujitolea yani kutorudishiwa kabisa fedha.
Na pia jinsi na namna fedha hizo zitakavyorudishwa.
2010 watakapotaka kukodi AIRBUS wawe wa wazi zaidi jinsi ya kupata fedha na kuzirudisha.
Mkamap jina lako linafanana kama vile Mkapa!!!??? Lakini pia linafanana na MiKaPePi (Mkpp) yaani Mizengo Kayanza Peter Pinda....
Lakini pia kwa maelezo yako hapo juu nitakuunga mkono ikiwa utakuja na hoja hiyo hiyo kwa fedha za CCM ambazo kuna uhakika asilimia 100 kwamba zimetoka BoT, kwanza zipo za moja kwa moja toka BoT na zile za kina Jeetu Patel, ambazo alinunua yale magari ya CCM wilaya zote na nyingine toka taasisi za serikali kama TCRA, TPA etc na benki na mashirika yenye hisa za umma kama CRDB bank, Benki ya Posta, NBC, NMB, na kadhalika, ambayo fedha zake zimekwenda CCM, inabidi zifanyiwe uhakiki na zikaguliwe na bila shaka na CHADEMA nayo ikaguliwe na itolewe maelezo kama unavyotaka. Hujakosea kabisa kutoa hoja hii, ila labda jinsi unavyoiweka tu. Lakini pia kama alivyosema mchangiaji mmoja humu, unapaswa kuweka data kama unazo ama kama kuna mtu anakutuma (inaruhusiwa pia) basi mwambie akupe data uweke kwa niaba yake maana anaweza kuwa ni mtu mzima amechoka hana uwezo wa kuingia JF aama anaogopa ama wewe ndio ajira yako. Usitetereke, tekeleza tu wajibu wako lakini jitahidi kuwa makini zaidi
Tina
Maelezo yako mazuri lakini sijaelewa falsafa yako yakufananisha majina na kufanya hoja fanani na kuhusisha Ajira na Hoja.
Mfano :mwanao kama anatabia mbovu na jirani yako akahoji inakuaje mwanao aliyekua kipenzi kwa tabia njema ameanza utukutu huu ,jirani yako akakushauri aisii fuatilia uone chanzo chake.
Lakini wewe badala ya kuchukua hiyo ni changamoto na kujibu hoja ya jirani yako ,wewe unamjibu hivi nenda kwa Juma kwanza ukamhoji mwanae ambaye alishikwa akiiba kuku hapo ndipo uje uniulize kwanini mwanangu amekua mtukutu.
Harafu hapa kumeibuka tabia ukipinga CHADEMA basi wewe ni CCM na umetumwa ama umeajiriwa.kazi kwelikweli
Yaani we acha tu,maanke itasaidia kumkata kimbelembele jirani mchonganishi na mpashkuna.
Mkamap,
Hata hivyo umeongea point,nitarudi baadae nikujibu professionally!
naona mh. Dr slaa yupo nasi hapa, naomba aupe ufafanuzi. je pesa mbowe alizokopesha chadema, alifuta utaratibu wa kawaida? je zilitumika kwa kusudio lilikubalika? kama majibu haya tutayapata, mkamap akubali kuwa anataka kuwafundisha chadema kudhulumu, yaani wamdhulumu mbowe pesa yake.tabia hii ya wizi na dhuluma ni ya ccm.
Mtanzania
Mimi sina ubaya na hizo fedha ,kwenye thread zile niliuliza hilo sikujibiwa watu walikua wanasema udini/ukabila ,nikaona kuna haja ya kuuliza ktk thread mpya.
Tatizo ni kwamba Aliyekua makamu wao WANGWE anasema mgogoro wake na Mbowe ni baada ya kuhoji jinsi malipo yanavyokwenda bila kufuata utaratibu,hayo ndio madai makuu ya wangwe.Mimi nilipendelea wamcrash huyu wangwe kwa kuonyesha taratibu za kukopeshana na kulipana kama zilifuata misingi ya sheria na haki.
Mimi nafikiri si kosa kuhoji taratibu halali kama zilifuata
Mzee wangu kwanza nikushukuru kwa kuwa nasi hapa. Umeonesha mfano ambao natamani wengine wangeuiga. Ni vema umeyaweka haya wazi ambayo yanasomeka kwa sasa na yataendelea kusomeka hapa. Hoja hii imeletwa hapa siku nyingi ingawa inakuwa inaibuliwa kila kukicha na kwa njia tofauti ila lengo likiwa hili.Mkamap, na wote waliochangia thread hii, nimeyaweka haya hadharani siyo kwa nia ya kufunga mjadala, bali wenye kupenda ukweli wanaweza kupokea kutoka hapo bila upotoshaji wa aina yeyote. Pia Kama tulivyoeleza mara baada ya uchaguzi, kuwa Chadema hatuna cha kuficha, tumewapa challenge na vyama vingine viweke hadharani na "sources" zao za "Campaign financing".
Narudia tena leo, kutoa mwito huo. Tutaweza tu kupiga vita ufisadi tukiwa wa wazi wenyewe, ndipo tuone boriti kwenye jicho la jirani.
Mkamap,
In the interest and on behalf of Chadema,swala la mkopo kwa Mbowe na Ndessamburo kama ifuatavyo:-
1) majadiliano ya Mkopo yalianzia kwenye Kamati Kuu, 2005 mara tu baada ya Kamati Kuu,Baraza Kuu kuamua Chadema kuingia kwenye mchakato wa Uchaguzi na kumweka Mgombea Urais. Mgombea yeyote ambaye angeliingia ilikuwa lazima azunguke nchi nzima kujenga chama, kuomba kura, na "kuwatengeneza" wabunge. mzunguko huo na kazi hizo zilihitaji fedha. Hivyo Kamati kwa mujibu wa Katiba ya Chadema, Toleo la 2004( ambayo bado inatumika katika ngazi zote isipokuwa Misingi na Matawi ambako uchaguzi unaendelea kwa mujibu wa Katiba, Toleo la 2007) na ninanukuu " Ibara ya 7.6.15 (g) kuandaa na kutoa mapendekezo kwa Baraza Kuu, Mikakati ya kupata mahitaji ya raslimali za kuendesha kampeni za wagombea wa Chama katika chaguzi za kiserikali". Kwa vile Mapendekezo ya Kamati Kuu yanaenda kwa Baraza Kuu, nayo kwa mujibu wa Katiba ya Chadema, Toleo hilo hilo, Ibara ya 7.6.12(g) nina nukuu "Kuthibitisha mikakti na raslimali za kuendesha kampeni za wagombea wa Chama katika chaguzi za Serikali hususan uchaguzi Mkuu wa Raisi, Wabunge/Wawakilishi na Madiwani". Baraza Kuu ilithibitisha mapendekezo hayo ya Mkopo kutoka kwa Kamati Kuu, nayo kwa mujibu wa Katiba hiyo hiyo Ibara ya 7.6.9 (c) na ninanukuu " kujadili taarifa za Baraza Kuu na kutoa maamuzi na maelekezo kwa utekelezaji".
Hivyo napenda kuthibitisha kuwa taratibu hizo zote za kikatiba zilifuatwa kikamilifu.
2) Baada ya Uchaguzi Mkuu, Chadema ilifanya vikao vyote kuanzia Kamati Kuu, Baraza Kuu hadi Mkutano Mkuu, pamoja na mengine kutathmini zoezi zima la Uchaguzi Mkuu. Taarifa zote ziliwasilishwa kwenye vikao vyote ndiyo maana ndani ya Chadema, kwa kuzingatia Chadema inafanya mambo yake kwa vikao Taarifa za Mkopo ilitolewa, na maelekezo ya namna ya kulipa deni hilo pia yalitolewa ikiwa ni kiasi gani kilipwe kwa mwezi. Taarifa hizi zote zinapatikana kwa Mwanachadema yeyote anayetaka kwenye Kumbukumbu zote za Chadema. Nyaraka zote zikiwemo Audited accounts ziliwasilishwa kwa vikao, ndiyo maana hakuna mgogoro wowote ndani ya Chadema, ukiacha mgogoro unaopandikizwa. Mwenye Taarifa ya mgogoro katika vikao vya Chadema, nina m-"challenge" azimwage hapa kuwasaidia wenzake kuelewa maswala kwa misingi ya uwazi na ukweli.
3) Kabla ya kuwasilisha Kamati Kuu na hatimaye Baraza Kuu na Mkutano Mkuu, Mhe. Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema, alitoa nusu ya fedha zote alizokopesha chama kama "mchango wake binafsi", kwa vile kila mmoja wetu, hasa wabunge wa Chadema kila mmoja alichangia kwa kiwango chake, ambayo siyo ya kulipwa. Kwa kuzingatia hali hiyo Mbowe, alisamehe karibu 250,Millioni, na kubakiza kama deni kwa shs 218 Millioni. Deni hilo pamoja na deni la 118 Millioni za Mhe. Ndessamburo zilipangiwa na vyombo vya maamuzi utaratibu wa kuzilipa kama nilivyoeleza, wastani wa Shs 25 Millioni kwa mwezi kwa madeni yote. Nimeona moja amesema kuwa Grace Kiwelu alikopesha Chadema 100 Millioni. Hakuna ukweli wowote katika hilo. Grace alikuwa amekopesha shs 10 Millioni, na kwa kuwa zilikuwa zililipwa zote katika mwezi wa kwanza. Fedha zote za Mhe. Ndessamburo sasa tumekwisha kuzilipa, na za Mhe. Mbowe zimebaki 43 Millioni. Ni kweli kuwa Chadema imeendelea kukopa wabunge wake kwa nyakati tofauti kwa shughuli zake mbalimbali na zote hizo zimelipwa kama makubaliano yalivyokuwa.
4) Mhe. Mbowe, amelipa fedha zote shs 21 Millioni za Helkopter kama mchango wake katika Kampeni ya Kiteto. Kama nilivyosema, kila kiongozi wa Chadema, na hata wanachadema kimsingi kazi zao, muda wao, magari yao yanathaminishwa na kutambuliwa kama mchango wao kwa chama chao. Huu ni wajibu wa Wanachadema katika kujenga chama chetu. La msingi ni utaratibu wetu wa ndani na mengine ya formula za ndani siyo ya kuweka hadharani, mwenye nia na mapenzi mema anayetaka kuona Chadema inavyofanya kazi afike tu Makao Makuu ataelezwa Chadema inavyofanya kazi, hatuwezi kumwaga Mchele "hadharani", to be polite.
Mkamap, na wote waliochangia thread hii, nimeyaweka haya hadharani siyo kwa nia ya kufunga mjadala, bali wenye kupenda ukweli wanaweza kupokea kutoka hapo bila upotoshaji wa aina yeyote. Pia Kama tulivyoeleza mara baada ya uchaguzi, kuwa Chadema hatuna cha kuficha, tumewapa challenge na vyama vingine viweke hadharani na "sources" zao za "Campaign financing".
Narudia tena leo, kutoa mwito huo. Tutaweza tu kupiga vita ufisadi tukiwa wa wazi wenyewe, ndipo tuone boriti kwenye jicho la jirani.
DR SLAA
Wewe ni mwana demokrasia safi,
Tatizo liliopo ni kwamba mnamuachia huyu jamaa yani CHACHA kupotosha jamii harafu nyie mnakaa kimya naa badala yake mnakuja hapa jf kuongea tofauti.
CHACHA kasema MBOWE na alikua anakidai chama MILION 500. Nawe wasema tofauti .Tatizo nini hasa ??
Kweli Kabisa .....! Huu Nao Ni Ufisadi...!huu Pia Ni Chapa Ya Ufisadi,katika Usanii Wa Aina Yake. Tafadhalini Jadilini Wana-lujna Wa Jf.
mkuu Meja Kumbe Ukishikwa Pabaya Huwa Unakuwa Hivi?,hili Si Lina Mslahi Ya Taifa??mbona Suala La Lowassa Na Rdc Nalo Lilikuwa Sula La Kibiashara Kati Ya Lowassa Na Rdc?mbona Suala La Mzindakaya Na Kukopeshwa Na Bank Lilikuwa Kati Yake Na Bank Kuu??je Haya Hayafananani??mbona Watu Walikuja Juu.tafuta Jibu Lingine Na Usilete Usanii..
Sheikh Yahay Alkishamsema Huu Ni Mwaka Wa Kujua Mengi Yaliyofichwa,na Tutasikia Mengi Tu!
Unataka Tulete Hoja Za Kumtetea Mbowe Tu Au Unataka Zipi?tukubali Na Mambomengine Ambayo Yanaweza Kuwa Ya Msingi.ndio Siasa Hiyo!!
Mie Nataka Kujua Ni Kwasabu Zipi Mbowe Alipi Hiyo Pesa??na Sina Kulinganisha Hili Na Suala La Ndanda Na Mzindakaya Si Kuwatetea Ni Wema Ili Naangalia Uhalisia Wa Mambo Haya.
Lowassa Na Mbowe Washitakiwe Kwa Hili