Kiukweli, fitina za kisiasa popote pale haziepukiki....
Lakini CCM na serikali wanayoingoza wameshavuka kwenye viwango vya fitina sasa wanatumia nguvu kulazimisha mambo kwa kuvunja sheria na katiba waziwazi na hivyo kuuvuruga uchaguzi huu na kuvuruga amani kabisa ya nchi yetu nzuri....
Katika hili mtu anaweza kujiuliza; Hivi Tundu Lissu aenguliwe kwa sababu zipi hasa za kisheria....??
Mimi bwana, sijaona vigezo vya kisheria wala kimaadili vitanavyoweza kutumika kumuengua....
Hakuna, hakuna, hakuna...!!!
Mpango ambao ulisukika na kuonekana uta - work out ni huu wa kutumia kesi kwa kushirikiana na NEC...
Bahati njema ni kuwa, umegundulika mapema na unaweza kudhibitiwa kirahisi tu....
Mimi nina hakika, kuwa, Tundu Lissu mpaka sasa ni mgombea halali wa Urais kwa tiketi ya CHADEMA, na hakuna wa kumzuia....
Mwamuzi atakuwa BALLOT BOX siyo maamuzi ya mezani...