Mbowe akishinda anatakiwa ajiuzulu ndani ya mwaka mmoja

Quinine

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
22,227
Reaction score
49,628
Kabla ya kujiuzulu panga safu nzuri ya uongozi ndani ya chama.

Pangua sekretariate yote, pangua safu ya wakurugenzi makao makuu, kuna wakurugenzi wamejimilikisha ofisi miaka na miaka tunawasikia.

Nenda CHASO tafuta vijana wapya wape majukumu wakipe chama uhai.

Usisahau kutibu majeraha na majeruhi wa uchaguzi yaunganishe makundi.

Kwa kushirikiana na viongozi wakuu, washauri, Kamati Kuu, Baraza Kuu andaeni atakayerithi mikoba yako, sio lazima awe public figure, lkn awe loyal kwa chama, aheshimu viongozi, katiba na wanachama.

Kazi hiyo uifanye ndani ya mwaka mmoja probably baada ya uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge, na Madiwani ni wakati wako mwafaka wa kujiuzulu.

Kama Lissu atakuwa bado mwanachama hai mshirikishe, yeye ni chachu ya mageuzi ndani na nje ya chama lkn si kwa nafasi ya Mkiti.

Kwa hali ya hewa ilivyo sasa usipojiuzulu kwa hiyari tegemea mapinduzi kama ya NCCR ya Mrema na Marando. Usipuuzie.

Mshauri hauawi.
 
Tatizo lake ni mbinafsi na mkabila
FREEMAN AIKAEL MUSEVEN MUGABE MBOWE.
 
Umetumwa hatumtaki
 
Mkuu
Ni vyema ukapiga tafakuri ya muda kabla ya kupost. Maana kila unacholeta ni BOKO tupu.
 
Mbowe angekaa tu pembeni apumzike.

Kama miaka 20 haijamtosha sembuse mwaka mmoja.
 
Na akimfukuza Lissu itasaidia sana.
 
yaani apoteze rasilimali za chama na muda wa wajumbe ili aje awe mwenyekiti wa mwaka mmoja?

Cha msingi anachopaswa kusikiliza ni kuwa Wanachadema wanaona muda alioongoza umetosha na wananchi waliowengi wanamkataa. Kung'ang'ania kwake kunapunguza momentum ya kisiasa ya chama, apumzike tu!
 
Mkuu
Ni vyema ukapiga tafakuri ya muda kabla ya kupost. Maana kila unacholeta ni BOKO tupu.
Unataka nipost unachokipenda, watasoma wanaopenda maboko yangu after all sijaku tag uje kusoma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…