Mbowe akishinda anatakiwa ajiuzulu ndani ya mwaka mmoja

Mbowe akishinda anatakiwa ajiuzulu ndani ya mwaka mmoja

Kabla ya kujiuzulu panga safu nzuri ya uongozi ndani ya chama.

Pangua sekretariate yote, pangua safu ya wakurugenzi makao makuu, kuna wakurugenzi wamejimilikisha ofisi miaka na miaka tunawasikia.

Nenda CHASO tafuta vijana wapya wape majukumu wakipe chama uhai.

Usisahau kutibu majeraha na majeruhi wa uchaguzi yaunganishe makundi.

Kwa kushirikiana na viongozi wakuu, washauri, Kamati Kuu, Baraza Kuu andaeni atakayerithi mikoba yako, sio lazima awe public figure, lkn awe loyal kwa chama, aheshimu viongozi, katiba na wanachama.

Kazi hiyo uifanye ndani ya mwaka mmoja probably baada ya uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge, na Madiwani ni wakati wako mwafaka wa kujiuzulu.

Kama Lissu atakuwa bado mwanachama hai mshirikishe, yeye ni chachu ya mageuzi ndani na nje ya chama lkn si kwa nafasi ya Mkiti.

Kwa hali ya hewa ilivyo sasa usipojiuzulu kwa hiyari tegemea mapinduzi kama ya NCCR ya Mrema na Marando. Usipuuzie.

Mshauri hauawi.
Mkuu mbona nilikuamini sana kwa kuwa na mawazo chanya?

Sasa kwanini wataka Mbowe aendelee kuwa mwenyekiti wa CHADEMA?

Kwasababu Mbowe ameishi na CHADEMA tangia 1992 akiisindikiza CCM hadi leo.

Huoni kuwa umefika wakati wa kupisha kiongozi mwingine ambae atatoa changamoto stahiki kwa CCM?
 
Mkuu Richard, ukifuatilia post zangu mimi ni muumini mzuri tu wa Lissu, tatizo la Lissu hana maadili ya uongozi. Kama ulisikiliza Clubhouse ya juzi siri zote za chama alizisema public.

Ukiangalia kwa makini Mbowe alikuwa kaamua kutogombea alibadili mawazo gafla baada ya kuona jinsi Lissu alivyoingia kwa kumtuhumu na kashifa kibao.

Mbowe atashinda lkn anatakiwa akikabidhi chama mapema kwenye mikono salama kabla mambo hayajaharibika zaidi.
 
Back
Top Bottom