Mbowe aligombeaje urais mwaka 2005 kama hana degree?

Kigezo cha elimu rasmi chochote (vyeti) utakachoweka kimsingi kitakuwa unfair, unconstitutional, undemocratic and a logical fallacy, appeal to authority.

Watanzania wengi hawaelewi hoja hii, ndiyo maana wanalalamikia hata sifa za kielimu za kuwa mbunge kuwa ndogo sana. Hawaelewi kuwa mbunge mtihani wake si wa darasani, ni wa kuwashawishi wananchi, ambao ni mgumu kuliko wa darasani.

Mnaliangalia tatizo kutoka upande mbaya. Hatuongezi ufanisi wa uongozi wa nchi kwa kudai vyeti fulani kutoka kwa viongozi. Tunaongeza ufanisi wa uongozi wa nchi kwa kuongeza elimu kwa wapiga kura wote.

Kwa sababu, ukiongeza vigezo vya elimu vya viongozi tu, wakati wapiga kura hawana elimu, viongozi wataona wananchi hawawezi kuwawajibisha. Watafanywa wanavyotaka.

Kwani baraza la mawaziri la sasa lina uhaba wa wasomi (kwa maana ya vyeti vikubwa)? Halina. Lakini kila ukisoma ripoti za CAG unaona madudu yanayotoka humo?

Hayo madudu ni kwa sababu viongozi hawana elimu ya vyeti?

La hasha. Ukiangalia elimu ya vyeti tuma ma Ph.D kibao, masters kibao. Wenye bachelor ndio wanaonekana hawajasoma.

Madudu hayo ni kwa sababu wananchi hawana elimu, hawana ufuatiliaji.

Ndiyo maana waliosoma sana hiyo elimu rasmi na kutupa mifumo ya elimu rasmi na demokrasia (nchi kama US na UK)hawana kigezo hicho.

Ukishaweka chujio la kwamba mtu asiye na cheti fulani hawezi kuwa rais, umeshavunja haki za msingi, za kidemokrasia za kikatiba za raia kupigiwa kura.

Wape wagombea wenye degeree na wasio na degree nafasi za kugombea urais, halafu wananchi wachague wenyewe wanamtaka nani.

Usijipe umuhimu wa kuwachagulia wananchi kuwa mwenye degree ndiye anawafaa.

Unaweza kutukosesha Lula da Silva wetu, John Major wetu au Harry Truman wetu.

Maana nzima ya demokrasia ni kuwaachia wananchi wachague kiongozi wao. Ukishaanza kuweka vigezo vigezo artificial kama vya vyeti ndiyo mwanzo wa kuwachagulia watu mgombea wako tu.

Yani unaweza kuweka vigezo kumuondoa mgomnea fulani wanayemtaka wananchi, ukamuweka mgombea wako unayemtaka wewe.

Ndiyo Kikwete alivyomtoa Sitta hivyo na kumuweka Anna Makinda Uspika kwa kigezo cha "safari hii tunamtaka mwanamke".

Ndiyo CCM walivyomkata Lowassa hivyo kwa kigwzo cha "safari hii tunataka wagombea vijana zaidi".
 
Mkatae Msukuma na wenzake kwa sababu ni wajinga, si kwa sababu hawana degree.

Kwa sababu, hata Nape ni mjinga lakini degree anayo.

Sasa utasema unakubali ujinga wa Nape lakini hukubali ujinga wa Msukuma kwa sababu Nape ana degree?

Unamhukumu mtu kwa hoja zake au kwa kuangalia kama ana degree?

Unajua watu wanaopiga hela vibaya sana nchi hii kwenye rushwa ni wenye degrees, tena nyingi tu?
 
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haijataja moja kwa moja kiwango maalum cha elimu kama sifa ya kugombea urais.

Hata hivyo, sifa za elimu zinaweza kuwekwa na Tume ya Uchaguzi au kupitia sheria nyingine zinazohusiana na uchaguzi au chama cha siasa husika.

Katika Ibara ya 39 ya Katiba, sifa zinazotajwa zaidi ni kuhusu uraia, umri, uadilifu, na uanachama wa chama cha siasa, lakini hakuna kipengele kinachotaja moja kwa moja kiwango cha elimu.
 
Elimu ipo,ikamfanya mrema kutafuta digrii mitandaoni
 
Hivi ni kweli Mbowe (Mboe) alipata zero form 6?. Au Huwa ni propaganda tu.?.

..it is 50 / 50.

..kuna wanaosema Mboe / Mboye alipata zero, na wengine wanasema si kweli.

..sawa na Mama Abduli. Wako wanaosema alipata zero form 4.

..Wengine wanakanusha wanasema Mama Abduli " hakufaulu " au " hakufanya vizuri " form 4.

Cc Gagnija
 
Kasome tena Katiba mkuu, takwa la kuwa na degree ni la vyama siyo la Kikatiba,
Katiba inataka ujue kusoma na kuandika Kiswahili ama Kingereza ama vyote
 
ndozao ccm wanataka RAIS awe na digrii lakini msimamia maendeleo nchini ambaye ni diwani anatakiwa kujua kusoma na kuandika tu(awe mjinga)
Atawezaje kuibiwa bila yeyekujua,au kurubuniwa ashiriki wizi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…