Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Kigezo cha elimu rasmi chochote (vyeti) utakachoweka kimsingi kitakuwa unfair, unconstitutional, undemocratic and a logical fallacy, appeal to authority.Kwanza sijasema kiwekwe kigezo cha degree au kwamba degree ni muhimu zaidi, nimesmea "elimu rasmi", Inaweza kuwa kidato cha nne, cha sita, diploma, certificate n.k, Inaweza pia kuwa ni equivalency.
Pili hata kama kigezo kingekuwa ni degree na taifa halina watu wengi wenye degree sio lazima kiwe undemocratic au unconstitutional kwa sababu hao watu wasio na degree wenyewe wanaweza kwa wingi wao wakaamua hicho ni kigezo muhimu kwa kiongozi kwa maslahi ya wote.
Watanzania wengi hawaelewi hoja hii, ndiyo maana wanalalamikia hata sifa za kielimu za kuwa mbunge kuwa ndogo sana. Hawaelewi kuwa mbunge mtihani wake si wa darasani, ni wa kuwashawishi wananchi, ambao ni mgumu kuliko wa darasani.
Mnaliangalia tatizo kutoka upande mbaya. Hatuongezi ufanisi wa uongozi wa nchi kwa kudai vyeti fulani kutoka kwa viongozi. Tunaongeza ufanisi wa uongozi wa nchi kwa kuongeza elimu kwa wapiga kura wote.
Kwa sababu, ukiongeza vigezo vya elimu vya viongozi tu, wakati wapiga kura hawana elimu, viongozi wataona wananchi hawawezi kuwawajibisha. Watafanywa wanavyotaka.
Kwani baraza la mawaziri la sasa lina uhaba wa wasomi (kwa maana ya vyeti vikubwa)? Halina. Lakini kila ukisoma ripoti za CAG unaona madudu yanayotoka humo?
Hayo madudu ni kwa sababu viongozi hawana elimu ya vyeti?
La hasha. Ukiangalia elimu ya vyeti tuma ma Ph.D kibao, masters kibao. Wenye bachelor ndio wanaonekana hawajasoma.
Madudu hayo ni kwa sababu wananchi hawana elimu, hawana ufuatiliaji.
Ndiyo maana waliosoma sana hiyo elimu rasmi na kutupa mifumo ya elimu rasmi na demokrasia (nchi kama US na UK)hawana kigezo hicho.
Ukishaweka chujio la kwamba mtu asiye na cheti fulani hawezi kuwa rais, umeshavunja haki za msingi, za kidemokrasia za kikatiba za raia kupigiwa kura.
Wape wagombea wenye degeree na wasio na degree nafasi za kugombea urais, halafu wananchi wachague wenyewe wanamtaka nani.
Usijipe umuhimu wa kuwachagulia wananchi kuwa mwenye degree ndiye anawafaa.
Unaweza kutukosesha Lula da Silva wetu, John Major wetu au Harry Truman wetu.
Maana nzima ya demokrasia ni kuwaachia wananchi wachague kiongozi wao. Ukishaanza kuweka vigezo vigezo artificial kama vya vyeti ndiyo mwanzo wa kuwachagulia watu mgombea wako tu.
Yani unaweza kuweka vigezo kumuondoa mgomnea fulani wanayemtaka wananchi, ukamuweka mgombea wako unayemtaka wewe.
Ndiyo Kikwete alivyomtoa Sitta hivyo na kumuweka Anna Makinda Uspika kwa kigezo cha "safari hii tunamtaka mwanamke".
Ndiyo CCM walivyomkata Lowassa hivyo kwa kigwzo cha "safari hii tunataka wagombea vijana zaidi".