Mbowe aliiweka Chadema rehani kwa Samia. Sisi tulimuuliza kwani kuna shida gani mzee? Mbona uwezo tunao huku ukituweka rehani?

Mbowe toka aseme CCM oyeeee nilijua Tu mambo yameshaharibika , nikajua Yuko chadema lakini anawaza Sana ccm yake
 
Toka 2022 ndio watu wanajitokeza leo kuanika "dhambi" za Mbowe? Hayo mapendekezo yalitoka kwa nani? Kama ni kutoka kwa CCM, alifanya kosa gani kuwashirikisha wenzake? Hayo yalikuwa ni mapendekezo ambayo Kamati Kuu ilikuwa na mamlaka ya kuyakataa na nadhani ndivyo ilivyokuwa. Sidhani kama Mbowe angekubali kupewa majimbo 20 maana kwa experience yake ni lazima alijua kuwa kuna uwezekano mkubwa wa CCM kumgeuka kwa ama kutoruhusu CDM washinde kama walivyo ahidi ( mfano ni NCCR Mageuzi) ama watatoa nje makubaliano hayo ili wakimalize kabisa chama chake. Mbowe sio mjinga kiasi hicho.

Mimi ninavyojua ni kuwa Lissu alitangaza nia ya kugombea urais kama chama chake kitampa idhini. Sijamsikia Mbowe akisema lolote kuhusu hilo. Kama angekuwa hataki angeweza kusema kuwa ametangaza nia mapema mno. Na mpaka hivi karibuni Lissu alikuwa anasisitiza kuwa yeye nia yake ni kugombea umakamu Mwenyekiti na urais tu. Kama alifanya hivyo huku akijua kuhusu usaliti mkubwa wa Mbowe basi tatizo litakuwa lake. Wenje amezungumzia tuhuma zilizotolewa dhidi ya Mbowe za kuhongwa magari mawili ambayo kiukweli aliyanunua katika mnada. Mpaka sasa hivi hatujaelezwa kama ni kweli tuhuma zilitolewa na kama zilikuwa za kweli.

Ninavyojua mimi ni kuwa strategists wengi wa vyama vya siasa huwa wanaangalia ni sehemu gani ndiko wana uhakika zaidi wa kushinda, na huko ndiko wanaweka nguvu kubwa. K.m. sio rahisi kwa Chadema kushinda Pemba na Mafia kwa hiyo itakuwa busara zaidi kuwekeza zaidi kwenye majimbo ya Mbeya, Mara n.k.

Hivi karibuni pamejitokeza tuhuma za ajabu ajabu kutoka kwa watu wanaodai wako jikoni. Kuna wanaodai walizuiwa na watu wa Mbowe kugawa kompyuta na kadhalika. Humu ndani wamejaa watu ambao wanaamini wakimchafua Mbowe ndio mtu wao atashinda na chama chao kitaingia kwenye era mpya ya mafanikio.

Nashauri wanyamaze. Kama wana ushahidi wa tuhuma hizo wazikabidhi kwa Kamati Kuu. Kama hawana imani nayo basi wamfanyie kampeni safi mgombea wao ili ashinde bila kukivuruga chama zaidi. Akishinda, wataweza kuzifuatilia na kuzichukulia hatua stahiki. Haya wanayofanya ni kwa faida ya wapinzani wao na sio chama chao.

Amandla...
 
Hakuna kitu Lisu atafanya,atapoa kama Mwabukusi wa TLS.

Unajua Kwa nini? Atalazimika ajijenge kimaisha Kwa hela za chama ili kuondoa aibu ambazo Mbowe amezitaja kumhusu Lisu.
 
Sio wewe tu, wapinzani wa kweli tutamwachia saccos yake na machawa wake
Kumbe ndio maana alipoitisha maandamano, wewe na mashujaa wenzako mlimkatalia?
Hamjawahi kuwa wapinzani wa dhati isipokuwa mkiwa nyuma ya keyboard.

Amandla...
 
Kadri siku zinavyoenda ninaanza kuamini zile tetesi toka Twitter/X kuwa kuna mtu kalambishwa asali ya 12B+ 🤣 G Sam
 
Mbowe akae tu pemben bhana

Hatutaki kubembelezana sisi hapa
 

Hakika unajua kuandika lete habari
 
Mbowe alifanya mengi sana, hatutaki kusema ila ikibidi tutasema yote
 
Huenda mwenyekiti alichangia pakubwa kuenguliwa kwa wagombea
 
Mbowe ameyatafta mwenyewe, saaa hivi hakuna jiwe litaachwa juu ya jiwe lingine.
Duru zinasema
  1. Kuna panguapangua ya Makatibu matawini ili kumlinda mwenyekiti
  2. Makamu anakwenda kufukuzwa uanachama muda si mrefu
 
Mkuu Mag3 , hoja isiwe ni wapi ninapata hoja zangu, hoja iwe jee hoja zangu zina logic?, zina mashiko?, zitaisaidia Chadema?.
p
 
Hoja zozote zikikabidhiwa kwa hii sekretarieti ya hawa makatibu wakuu ndio mwisho wake huo na hutosikia zikijadiliwa.
Mwenyekiti wa kikao anao uwezo wa kuzima hoja yoyote isijadiliwe na ndio umekuwa utaratibu wake kuendesha chama kibabe.
Huu ubabe sio wa leo, toka enzi za Chacha Wangwe umesemwa sana.
 
Kumbe ndio maana alipoitisha maandamano, wewe na mashujaa wenzako mlimkatalia?
Hamjawahi kuwa wapinzani wa dhati isipokuwa mkiwa nyuma ya keyboard.

Amandla...
Maandamani yaongozwe na tapeli anayekula nao maccm?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…