Mbowe alisema kachanjwa chanjo ya Corona, mbona anaendelea kuvaa barakoa? Nchi walizochanja nao wanaendelea kuvaa barakoa

Mbowe alisema kachanjwa chanjo ya Corona, mbona anaendelea kuvaa barakoa? Nchi walizochanja nao wanaendelea kuvaa barakoa

Mbowe aliutangazia umma kuwa yeye keshachanja chanjo ya Corona lakini kila anapoenda barakoa haimtoki

Nimeangalia nchi za wenzetu pia kama ULAYA na Marekani wamechanja lakini kutwa wanavaa vibarakoa!! wana maintain social distance,kunawa maji tiririka nk

Sasa hiyo chanjo ina kazi gani kama sio utapeli
Wakina Uhuru Kenyata wakina Joe Biden wamechanjwa ila kitwa nzima wako na Barakoa

Umeona Mbowe pekee Dunia nzima ndo kachanjwa then anavaa Barakoa?
 
Wameshajikinga kwa kuchomwa sindano ya kinga ya Corona sasa barakoa za nini tena? social distance za nini tena?
Ni Mbowe pekee nazani Dunia nzima ndo kachanjwa then anavaa barakoa
 
Mbowe kapigwa chanjo kama fashion tu ila hata yeye haiamini kivileeee.
Nasikia ndani ya miaka miwili waliopigwa chanjo wote wanadanji sijui kama ni kweli
Vipi na wale wa kina Joe Biden wanao vaa na wechanjwa unawaelezea vipi?

Wakina Kagame si mbona kutwa nzima wako na Barakoa na wamechanjwa?

Akili za kuvukia barabara
 
Mbowe aliumwa Corona nilitarajia mwili wake umeshatengeneza kinga.
inashangaza kusikia anachanja kutafuta kinga.
Elimu kaka.hana elimu....mtu ukishaumwa..ukapona mwili tayar unauwezo wa kupambana na hao wadudu..tayar antibodies zishafanya yake...sasa unakuja ambiwa uchomwe tena wadudu wengne ..hiv inaingia akilin aisee
 
Mbowe aliutangazia umma kuwa yeye keshachanja chanjo ya Corona lakini kila anapoenda barakoa haimtoki

Nimeangalia nchi za wenzetu pia kama ULAYA na Marekani wamechanja lakini kutwa wanavaa vibarakoa!! wana maintain social distance,kunawa maji tiririka nk

Sasa hiyo chanjo ina kazi gani kama sio utapeli
Kuna siri kubwa nyuma ya pazia!
 
Una uhakika gani wamechanjwa?
Vipi na wale wa kina Joe Biden wanao vaa na wechanjwa unawaelezea vipi?

Wakina Kagame si mbona kutwa nzima wako na Barakoa na wamechanjwa?

Akili za kuvukia barabara
 
Hivi ina maana hujasikia sababu ni kwanini hata watu waliochanja wanaendelea kuvaa barakoa au unajitoa ufahamu? Kama hujasikia na hujui sababu mpaka sasa wakati maelezo yameshatolewa mara nyingi na hata kama uta-google dakika moja utakuwa umeshapata sababu basi wewe huna tofauti na kima kiakili.
Labda nia yako ni kumtusi, ila mimi naona umejitusi mwenyewe.
Wewe unaamini mpaka ukijue wewe, basi kalibia watu wote wanakijua, ndiyo maana badala ya kumuelezea, nini kimetokea unamwambia agugo.
 
mtoa mada hujielewi.
chanjo haisaidii wewe kutopata corona bali inakusaidia katika vulnerable group for those affected by corona.(vulnerable ni wale wanaoathirika zaidi na corona mpaka kushindwa hata kupumua (
 
Mbowe aliutangazia umma kuwa yeye keshachanja chanjo ya Corona lakini kila anapoenda barakoa haimtoki

Nimeangalia nchi za wenzetu pia kama ULAYA na Marekani wamechanja lakini kutwa wanavaa vibarakoa!! wana maintain social distance,kunawa maji tiririka nk

Sasa hiyo chanjo ina kazi gani kama sio utapeli
Ukichanjwa unaweza usiathiriwe, lakini unaweza kuwa na virusi vinavyoweza kuwadhuru wengine mfano ukiwa na watu wenye hivyo virusi. Kutovaa barakoa ni kwenye mazingira ambayo unaona huwezi kuwaambukiza wengine hata kama wewe uko salama.
 
... hebu Mataga muwe na akili; anayevaa barakoa anajali wengine kuliko anavyojijali mwenyewe kwani inasaidia kuzuia majimaji ya mwilini kuwafikia wengine. Ukichanjwa haimaanishi virus vya COVID haviwezi kukufikia; inamaansha madhara yake yanapungua. Ukiwa navyo hata kama umechanjwa vikiwafikia wengine unawaathiri.

So, Mbowe na wengine waliochanjwa kuvaa barakoa ni kwa faida ya wengine kuliko faida kwao binafsi. Na huo ndio UBINADAMU; kumthamini jirani yako kama nafsi yako! Hata maandiko si yanasema hivyo?

We endelea kusambaza Covid kisa legacy ni muuwaji kama wauwaji wengine!
Kwahiyo inawezekana Mama samia ana corona nini? maana tunaona mawaziri wake wanavaa barakoa akiwepo rais tu ila wakitoka hapo hawavai tena mpaka wakutane tema na rais, hivyo inawezakana Mama samia ana corona ndio maana anawakinga wengine kwa yeye kuvaa barakoa na kuwataka wengine pia wavae wakiwa karibu nae.
 
Ukichanjwa unaweza usiathiriwe, lakini unaweza kuwa na virusi vinavyoweza kuwadhuru wengine mfano ukiwa na watu wenye hivyo virusi. Kutovaa barakoa ni kwenye mazingira ambayo unaona huwezi kuwaambukiza wengine hata kama wewe uko salama.
Barakoa inaendana na social distance,kunawa mikono na mambo mengine yote ila huwezi kuvaa barakoa halafu mikusanyiko isiyo na lazima unaiendeleza hapo utakuwa hujui ni nini unafanya. Ndio maana wengine hupinga huu uvaaji wa barakoa public maana huwafanya watu kujiona wako safe na kusahau au kudharau social distance kunawa mikono na mambo mengine.
 
mtoa mada hujielewi.
chanjo haisaidii wewe kutopata corona bali inakusaidia katika vulnerable group for those affected by corona.(vulnerable ni wale wanaoathirika zaidi na corona mpaka kushindwa hata kupumua (
Na barakoa tu yenyewe haiwezi kuzuia maambukizi ikiwa tahadhari zengine hazifuatwi, hamuwezi mkawa mnakusanyana tu bila ulazima huo na mikono hamnawi wala hamjui matumizi sahihi ya jinsi ya kuvaa wala kuvua barakoa halafu mtegemee et barakoa ukivaa tu inazuia maambukizi.
 
Kikwazo kikubwa cha taifa hili ni ujinga wa kupindukia na wewe ni mmoja wao. Chanjo haizuii usiambukizwe, chanjo inaongeza kinga ya mwili ili usifikie kuumwa na hatimaye mauti!! Unaweza bado ku-test positive na ukiwa umechanjwa!!

Unaweza kumwambukiza vijidudu hivyo kidogo mtu ambaye hajachanjwa na asipate kuumwa lakini mwingine uliyemuambukiza akaumwa na labda hata mauti kumfika. Chanjo hii sio tiba ya corona. Inausaidia mwili kuishinda corona!!!

Hata kama tuna wasiwasi na chanjo, hatupaswi kuwa waongo kwa watu wengine. Kila aliyechanjwa anashauriwa kuendelea kujikinga kwa sababu pia kuna variants ambao hawapunguzwi makali na baadhi ya variants. Acha upotoshaji!!

Umeelezea vizuri Mkuu
Hata mimi nimepata chanjo ya kwanza na bado nikienda sehemu za watu navaa [emoji40]
Na hii ya India imeleta tafrani tena
 
Barakoa inaendana na social distance,kunawa mikono na mambo mengine yote ila huwezi kuvaa barakoa halafu mikusanyiko isiyo na lazima unaiendeleza hapo utakuwa hujui ni nini unafanya. Ndio maana wengine hupinga huu uvaaji wa barakoa public maana huwafanya watu kujiona wako safe na kusahau au kudharau social distance kunawa mikono na mambo mengine.
Sawa, lakini maisha lazima yaendelee - watu wanaendelea kukusanyika kwenye nyumba za ibada, mikutano ya hadhara, mafunzo, biashara au sehemu za kazi nk - lakini wanasisitizwa kuchukua tahadhari.
 
Labda nia yako ni kumtusi, ila mimi naona umejitusi mwenyewe.
Wewe unaamini mpaka ukijue wewe, basi kalibia watu wote wanakijua, ndiyo maana badala ya kumuelezea, nini kimetokea unamwambia agugo.
Siyo ''kalibia'' ni karibia. Kama mtu hujui kitu ukiambiwa nenda kasome sehemu fulani siyo msaada? Ulikwenda shule gani wewe?
 
Kwahiyo inawezekana Mama samia ana corona nini? maana tunaona mawaziri wake wanavaa barakoa akiwepo rais tu ila wakitoka hapo hawavai tena mpaka wakutane tema na rais, hivyo inawezakana Mama samia ana corona ndio maana anawakinga wengine kwa yeye kuvaa barakoa na kuwataka wengine pia wavae wakiwa karibu nae.
Mhu! Aina hii ya logic x and y, therefore, z ni hatari sana.
 
Back
Top Bottom