Mbowe alivyokimbiwa na wafuasi wake ni kama Yesu alivyoachwa solemba na wanafunzi wake akakamatwa na jeshi la Rumi

Mbowe alivyokimbiwa na wafuasi wake ni kama Yesu alivyoachwa solemba na wanafunzi wake akakamatwa na jeshi la Rumi

Mimi acha nipumzike, leo nitakula ugali, mlenda na Samaki wa kuchoma.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa Sasa Dar es salaam
Sijakusoma hadi mwisho mkuu 'Robert Heriel'; nimesoma tu kipande cha juu hadi huko kwa Yesu na akina Musa ,Daud na wengineo, halafu nikaona nije huku chini niandike haya kwa sasa.
Nashukuru kwamba sasa ninakuelewa vizuri zaidi wewe ni mtu wa aina gani.
Nitakusoma andiko hili zima kwa uangalifu zaidi nitakapo pata muda. Nikiona kuna la kuongeza nitafanya hivyo; usipo nisoma tena elewa nimejiridhisha iwe hivyo.
 
POLISI MNAWEKA KAMBI KANISA KATOLIKI HAPO MSIMBAZI MNATAFUTA NINI??SAMIA UNATAFUTA KWA WAKATOLIKI?SAMIA ULIKWENDA VATICAN KUFANYA NINI?JE NCHI INAENDESHWA KIDINI?
 
Watanzania ni watu. Usiwa underestimate.
Polisi sio wajinga kufanya wiki nzima HIKI walichokifanya.

Mtu ni mtu Mkuu.
Ukipuuza kidogo mambo huweza kubadilika kwa namna itakayokushangaza
Na ukizangitia kuwa misukule wa mzee Mbowe ni mabomu yasiyo na mwelekeo misguided
 
Sijakusoma hadi mwisho mkuu 'Robert Heriel'; nimesoma tu kipande cha juu hadi huko kwa Yesu na akina Musa ,Daud na wengineo, halafu nikaona nije huku chini niandike haya kwa sasa.
Nashukuru kwamba sasa ninakuelewa vizuri zaidi wewe ni mtu wa aina gani.
Nitakusoma andiko hili zima kwa uangalifu zaidi nitakapo pata muda. Nikiona kuna la kuongeza nitafanya hivyo; usipo nisoma tena elewa nimejiridhisha iwe hivyo.

Uwe na utulivu tuu
Akili yako isiingiliwe na ushabiki na hisia. Tumia akili na Mantiki
 
Huyu mleta uzi hua nasoma aya zake tatu za mwanzo, mbili za kati na mbili za mwisho.

Na mara zote hua nakutana na misinformed paragraphs (labda ambazo sizisomi hua na taarifa sahihi)

Ila dah 😂😂😂
 
Siamini kama utawala wa kidikteta unaweza kutolewa kwa njia ya ballot box au maandamano ya amani.. hata elimu tu ya kawaida ya novel za wakina Chinua achebe zinakataa.

Chadema fikirieni njia mpya na hopefull mnaijua…
 
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

Kuna watu wanauliza Wafuasi wa Mbowe(Wanachadema) walikuwa wapi wakati kiongozi wao anakamatwa na Askari pale kwenye Magomeni.

Wapo wapi anaowapigania?

Wapo wapi waliopatwa na madhila, majanga ambao Mbowe na viongozi wenzake anawasemea na kuwapigania?

Yesu naye alikuwa mwenyekiti kama alivyo Mbowe, Yesu aliwatendea watu wengi miujiza na kufanya makubwa sana ambayo yalivuma na kuwa maarufu katika Judea, Samaria, mama nchi jirani.

Lakini siku alipokutana na Mkono wa Dola, watu wote walimkimbia.
Sio wanafunzi wake.
Sio wale aliowaponya,
Sio wale ambao aliwafufua,
Sio wale aliowalisha chakula.
Wote walimkimbia, zaidi ya yote alisulubishwa.

Kuna mambo ya kujifunza katika mambo haya. Hasa unapoingia katika mambo Ya kisiasa;

1. Usitegemee watu walionyuma yako, hakikisha unajiweza.
Elewa kuwa walionyuma na chini yako wewe ndiye kiongozi wao hivyo endapo utapoteana basi hata wafuasi wako watapoteana.

Kiongozi hategemei Waliochini yake. Kiongozi anategemewa.

2. Kiongozi lazima uwe na Way forward ya namna ya kukabiliana na adui zako..
Maandamano hayawezi kufanikiwa kwa sababu wanaoyaratibu na viongozi wao huruhusu kukamatwa mapema kabla picha halijaanza.

3. Kiongozi wa kisiasa ni muhimu kuwa na Mafunzo ya kijeshi na elimu ya Kijasusi.

Yesu hakufanikiwa kufanya jambo lolote la maana kisiasa na alishindwa kukomboa taifa la Kiyahudi kwa sababu hakuwa na mafunzo ya kivita, kijeshi na mambo ya Kijasusi. Ingawaje washabiki na wafuasi wake humtetea kwa kusema ilimbidi auawe ili wakombolewe kiroho lakini kisiasa hizo tunaita porojo au propaganda za kuwapa moyo mashabiki wake.

Hii ni tofauti na Ma legend wengine kama Musa, Daudi, Ibrahim, Yusufu, Yakobo n.k. hawa wote walikuwa viongozi na walikuwa wanamafunzo ya kivita, kijeshi, na intellijensia.

Na wote misheni zao zilifanikiwa.

Kwa sababu Jeshi, ujasusi, mapigano ni sehemu ya field katika Utawala na Mamlaka.

Ni rahisi kwa mwanajeshi, mwanasheria, jasusi, Polisi, au jeshi kwa aina zake kufanikiwa kutawala au kuchukua Utawala kuliko mtu ambaye wa fani kama Ualimu, udaktari, uinjinia, n.k.

Daudi kabla hajawa Mfalme alikuwa naye na wafuasi wake. Yaani Daudi alikuwa Mwenyekiti katika genge ambalo lilikuwa linamuamini.

Daudi kitaaluma alikuwa mchungaji wa mifugo, mwanamuziki lakini kumbe kwa Siri huko porini alikuwa anajifunza mapigano ya kivita.

Hii ni kusema hata siku anakutana na Goliath hakuwa amekurupuka, alijua kuwa anauwezo wa kupigana na Goliath na Mungu angemsaidia.

Ukitaka ujue kuwa Daudi pia alikuwa Jasusi na kapteni sio tuu tukio la kumuangusha Goliath bali hata harakati za kukabiliana na Mfalme Sauli ambaye hakutaka kumuachia Ufalme kwa njia ya Amani. Daudi alijiepusha sana na Dola, alikimbia na kuepuka mitego yote ya Dola ambapo kwa mtu wa kawaida angekuwa ameshapigwa mapema.

Tundu Lisu na Mbowe wanachokosea ni kudhani kuwa siasa wanazozifanya ni sahihi wakati sio sahihi.
Siasa za Mbowe na Lisu ni sahihi katika ulimwengu wa Dunia ya kwanza huko kwa Wazungu wenye mambo ya Demokrasia. Lakini kwa Afrika sio sahihi kabisa kwa sababu;

Mosi, Afrika Bado ipo nyuma kwa karibu Karne mbili nyuma ya Wazungu. Yaani tupo nyuma ya Wakati.

Pili, Waafrika pia akili, mitazamo, na Mila zetu Bado ipo nyuma.

Sio ajabu Watanzania wengi hawawezi kuelewa kile wanachokifanya Mbowe na Lissu.

Watanzania na Waafrika wengi hawaelewi Uhuru ni kitu gani, Haki ni nini, Mila potofu ni zipo,
Lakini tumaini ni kuwa kidogokidogo mambo yatabadilika.

Kwa hiyo njia pekee ambayo Watanzania na Waafrika huilewa ni njia ya mabavu na maguvu.

Watu wasiotambia Haki zao, uhuru wao, kipi kizuri na kipi kibaya huwezi kuwaongoza kwa njia za kidemokrasia. Ubabe, udikteta, maguvu ndio njia sahihi.

Huwezi kuleta Demokrasia kwa ulimwengu ambao Bado unaamini katika Mwanamke anatakiwa kutolewa Mahari. Alafu ukiwaambia wakupe hoja hakuna hata Moja ya maana.

Huwezi leta Demokrasia kwenye jamii ya watu ambao wanaaminj hawafanikiwi kwa sababu wamelogwa au Kuna mtu kamtupia Jini. Hiyo Demokrasia ya kazi gani?

Huwezi leta Demokrasia au kuwapa watu uhuru wanaoamini kuwa Mzazi anaweza kukutamkia maneno mabaya(Laana) Ati yakashika au baraka ikashika jambo ambalo ni uongo wa mchana Kabisa.

Huwezi leta au kupigania Demokrasia kwenye jamii ambayo Albino wanauliwa kisa mambo ya kishirikina.

Huwezi leta Demokrasia kwa watu ambao wanaamini kiongozi wa dini akiwapa mafuta au kitu Fulani watafanikiwa. Hizi ni akili za wakati wa Yesu, zama za zamani sana.

Ambapo miaka hiyo Wafalme walidanganya wanaowatawala kuwa wao ni miungu na wanauwezo wa kimungu.

Huwezi leta Demokrasia kwa watu ambao huona mzazi au mkubwa Hakosei. Hiyo jamii Bado ipo gizani.

Huwezi leta Demokrasia kwa watu wanaoamini mwanamke ni kumbe cha kukaa nyumbani. Kiumbe kisicho na Haki kama Mtu.
Na wanawake wenyewe wanaoamini vivyohivyo. Huwezi peleka Demokrasia huko.

Huwezi kupeleka Demokrasia kwa watu hao kwa Sababu zifuatazo:
1. Wataitumia vibaya Demokrasia na uhuru utakaowapa.

Waafrika tunashuhudia wakilalamika Kila pembe ya Afrika kuwa mbona walipigania uhuru lakini mambo ni kama yamewashinda. Uhuru unapiganiwa na watu waliojiandaa na waliokomaa.

Hata mtoto mdogo ukimpa uhuru kabla ya Wakati wake sio ajabu ukamkuta anavuta mibangi, madawa ya kulevya na kufanya mambo ndivyosivyo.

2. Kundi dogo kukandamiza kundi Kubwa.
Demokrasia ni watu wengi ndio husikilizwa na kunufaishwa. Lakini watu ambao hawajaandaliwa kupata Demokrasia huwa kinyume chake, kwamba kundi dogo kusikilizwa na kuneemeka dhidi ya kundi Kubwa.

3. Kutokueleweka.
Unamwambia Mtu wewe ni mtu lazima ufanye kazi ili uwe Huru, unahaki ya kuchagua au kuchaguliwa kiongozi, hakuelewi.

Unamwambia Mtu hutakiwi kutolewa Mahari, hawezi kukuelewa na hana Makosa kwa sababu amefungwa macho yake. Anaona kiza mbele.

4. Machafuko.
Uhuru, Demokrasia na Haki haiwafai watu ambao hawajajiandaa kwa Sababu huweza kusababisha machafuko.

Sio ajabu watu wanaona mbona ndoa siku hizi zinapasuka vipandevipande, wanasema mwanamke kapewa Uhuru au suala la HAKI Sawa.

Mtu anapopewa uhuru kabla hajaandaliwa kinachofuata ni machafuko.

Lazima mtu aandaliwe kuwa Huru.

Kumpa mtu uhuru kabla hujamuandaa ni sawa na Ndama aliyekata Kamba.

Katika Level ya Familia,
Wazazi Bora hujua kabisa Uhuru na Demokrasia ni muhimu sana kwa mtu. Hivyo huwaandaa watoto wao hatua kwa hatua namna ya kuwa watu Huru na watu wa Haki na Demokrasia.

Mtoto akipewa uhuru bila kuandaliwa sio ajabu akifika chuo kikuu anaanza kuparangana huko kwenye ma-club na makasino bila AKILI. Kuparamia wanawake hovyo, kunywa mapombe na mavyakula pasipo AKILI.
Mwishowe mtoto huweza kudhurika na wakati mwingine kufa kabla ya Wakati

Uhuru unaenda kwa Hatua. Uhuru unaenda sambamba na AKILI.

Uhuru bila AKILI yaani uhuru ambao haujaandaliwa huleta machafuko na anguko.

Zipo hatua za watu kupigania au kupewa Uhuru. Hilo litakuwa Somo jingine. Kwa sababu uhuru nao ukicheleweshwa huleta machafuko na maanguko.

Taikon nimeandika mpaka nimepotea njia lakini naamini nilichoandika ukitulia kitatusaidia wote.
Lakini kama hakijakusaidia au hakitakusaidia nakupa Pole sana.

Mimi acha nipumzike, leo nitakula ugali, mlenda na Samaki wa kuchoma.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa Sasa Dar es salaam

Siku ya Kiyama, mahakimu na wote wenye mamlaka watasimama mbele ya Mwenyezi Mungu kwa ajili ya hukumu.

Katika Uislamu, Qur'an na Hadithi zinatufundisha kuwa yeyote aliyepewa jukumu la kuhukumu wengine anawajibika kutumia uadilifu. Mahakimu ambao hawakuwa waadilifu au walitumia madaraka yao vibaya watawajibishwa mbele ya Mwenyezi Mungu kwa makosa yao.

Katika Qur'an, Surat Al-Baqarah (2:284), Mwenyezi Mungu anasema:“Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye ufalme wa mbingu na ardhi. Na kama mtaonyesha yaliomo ndani ya nafsi zenu au mtaficha, Mwenyezi Mungu atawatoza hisabu kwa hayo.
Kisha atamsamehe amtakaye na atamwadhibu amtakaye; na Mwenyezi Mungu ni Mwenye uweza wa kila kitu.
”Hii inamaanisha kuwa hakuna kitakachofichika mbele ya Mwenyezi Mungu, hata matendo yaliyofanywa kwa siri. Mahakimu waliohukumu bila haki watahukumiwa kwa matendo yao yote, ya ndani na ya nje.
Pia, Hadithi nyingi za Mtume Muhammad (SAW) zinatilia mkazo hatari ya kutokuwa na uadilifu katika kutoa hukumu. Katika Hadithi iliyopokewa na Imam Muslim, Mtume (SAW) alisema:

“Hakika waamuzi ni wa aina tatu: mmoja atakuwa Peponi na wawili watakuwa Motoni. Yule aliyehukumu kwa haki na kwa ujuzi atakuwa Peponi. Yule aliyehukumu bila ujuzi, na akaonea katika hukumu, atakuwa Motoni.”
(Sunan Abu Dawood, Hadithi 3573)

Hadithi hii inaonyesha kwamba mahakimu ambao hawakufuata haki wataadhibiwa vikali kwa dhuluma zao. Mwenyezi Mungu atahukumu kwa haki kamili, na wale ambao walikiuka haki duniani wataadhibiwa vikali kwa makosa yao.Kwa hivyo, katika Siku ya Kiyama, mahakimu na wale wenye mamlaka watapata hukumu ya haki kwa mujibu wa matendo yao, na wasio waadilifu watawajibishwa kwa dhuluma zao.
 
Siku ya Kiyama, mahakimu na wote wenye mamlaka watasimama mbele ya Mwenyezi Mungu kwa ajili ya hukumu.

Katika Uislamu, Qur'an na Hadithi zinatufundisha kuwa yeyote aliyepewa jukumu la kuhukumu wengine anawajibika kutumia uadilifu. Mahakimu ambao hawakuwa waadilifu au walitumia madaraka yao vibaya watawajibishwa mbele ya Mwenyezi Mungu kwa makosa yao.

Katika Qur'an, Surat Al-Baqarah (2:284), Mwenyezi Mungu anasema:“Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye ufalme wa mbingu na ardhi. Na kama mtaonyesha yaliomo ndani ya nafsi zenu au mtaficha, Mwenyezi Mungu atawatoza hisabu kwa hayo.
Kisha atamsamehe amtakaye na atamwadhibu amtakaye; na Mwenyezi Mungu ni Mwenye uweza wa kila kitu.”Hii inamaanisha kuwa hakuna kitakachofichika mbele ya Mwenyezi Mungu, hata matendo yaliyofanywa kwa siri. Mahakimu waliohukumu bila haki watahukumiwa kwa matendo yao yote, ya ndani na ya nje.
Pia, Hadithi nyingi za Mtume Muhammad (SAW) zinatilia mkazo hatari ya kutokuwa na uadilifu katika kutoa hukumu. Katika Hadithi iliyopokewa na Imam Muslim, Mtume (SAW) alisema:
“Hakika waamuzi ni wa aina tatu: mmoja atakuwa Peponi na wawili watakuwa Motoni. Yule aliyehukumu kwa haki na kwa ujuzi atakuwa Peponi. Yule aliyehukumu bila ujuzi, na akaonea katika hukumu, atakuwa Motoni.”
(Sunan Abu Dawood, Hadithi 3573)

Hadithi hii inaonyesha kwamba mahakimu ambao hawakufuata haki wataadhibiwa vikali kwa dhuluma zao. Mwenyezi Mungu atahukumu kwa haki kamili, na wale ambao walikiuka haki duniani wataadhibiwa vikali kwa makosa yao.Kwa hivyo, katika Siku ya Kiyama, mahakimu na wale wenye mamlaka watapata hukumu ya haki kwa mujibu wa matendo yao, na wasio waadilifu watawajibishwa kwa dhuluma zao.

Kila mtu atawajibishwa kwa alichofanya.
 
Back
Top Bottom