Mbowe ameingiwa na hofu. Nini kimempa Hofu na kukata tamaa?

Mbowe ameingiwa na hofu. Nini kimempa Hofu na kukata tamaa?

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
Habari za Sabato!

Nimeona Mbowe Akihojiwa na Kikeke. Kwa kweli hofu ipo dhahiri machoni mwake. Hata body language yake inamkataa akijaribu kuficha hofu yake. Ni kama amekata tamaa pakubwa.

Ingawaje wafuasi wake wanahangaika kupambana, na kumtia moyo lakini jitihada Zao zimefua dafu kuondoa Hofu ya Mbowe.

Mambo mawili yananifanya nifikiri sababu za Hofu yake;
1. Kura za Maoni za watu wengi mtandaoni zimemkatisha tamaa.
Unajua hakuna Jambo Baya kwenye siasa kama kugundua kuwa hukubaliki kuliko mshindani wako.
Yaani watu wengi hawakutaki. Tena wengi wakiwa ni wale unaowongoza.

Kura za JF na X zimerudisha nyuma majeshi ya ujasiri katika moyo wa Mbowe.
Sio Kazi ndogo KUKATALIWA na watu kwa zaidi ya asilimia 80% ni nyingi Sana hizo.

Kumaanisha, Mbowe Hana ushawishi.
Hivi Leo itamaanisha, kama Mbowe akiitisha Harambee watu wachangie Basi asilimia 80% hawatamuunga Mkono.

Kumaanisha Leo Mbowe akiwa kampeni Manager WA Urais wa CHADEMA zaidi ya 80% hawatamchagua.

Hilo pekee limemnyong'onyesha Mbowe. Ingawaje wapambe wake watampa moyo na wengine kumdanganya lakini tayari Mbowe picha Halisi ya vile watu wanavyomchukulia anayo.

2. Mbowe anajuta, MAJUTO.
Nachelea kusema, Mbowe anajuta Kutetea Kiti chake.
Ukimtazama Mbowe kwa umakini, mbali na hofu utagundua sio hofu pekee tuu inayomtafuna Bali Hofu yenye MAJUTO.

Mbowe anajuta kwa Mambo yafuatayo;
1. Kujivua nguo na heshima yake yote kudondoka.
Hii inamaanisha asilimia 80% ya wapiga Kura waliomkataa wengi wameona Mbowe kajidharau.

Kama Mbowe angestaafu kwa heshima angekuwa amecheza vizuri Sana

Heshima ya watu kutaka uendelee lakini wewe useme inatosha. Hiyo ndio heshima sio usubiri kuzomewa na kutukanwa.

2. Anajuta kuona chama kinaweza kumfia Mikononi.
Hatari ya chama kumfia Mikononi Ipo bayana Kabisa.
Watu wengi Makini ndani ya chama hawapo upande wake.

Na wale wanaotegemewa na kusubiriwa watoe tamko bado wako Kimya, hii kwake ni kama taa nyekundu ambayo inampa Hofu na kumfanya ajutie.

3. Anajuta kwa nini hakumteua mtu wake agombee ili yeye amuunge Mkono.
Mbowe hakutegemea kama Lisu angefanya shambulizi la kushtukiza namna hii. Hii ilimnyima nafasi ya KUFIKIRI vizuri na kupanga suluhu yenye Tija.
Anajuta hakuwa na sababu ya kuendelea yeye, Bora angeteua mtu mwingine alafu yeye amuunge Mkono.

4. Anajuta kupingana na Maneno yake, hasa kutetea Demokrasia.
Sio ubishi kwani ni dhahiri hata Mbowe anajua kuwa Mpaka mashinani wanachama wanamtaka LISU na sio yeye.
Demokrasia inahusu uongozi wa watu. Ikiwa watu wengi hawakutaki alafu wewe unalazimisha kuendelea kugombea uenyekiti tafsiri yake wewe ni Dikteta.

Wajumbe 1200 Vs Wanachama zaidi ya Milioni na kitu.
Wanachama wengi wanamuunga Lisu Mkono. Wajumbe bado ni Siri

Sijajua kwa nini CHADEMA hawakufanya Utafiti kujua wanachama wa kawaida wao wanataka Nani awe Mwenyekiti.

Acha nipumzike sasa.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Ni busara kuu kama angestaafu Kwa heshima kabla ya kutaka kustaafishwa na sanduku la kura

Ngoja tuone namna atakavyoutoboa mtumbwi wanaosafiria na ndo azma iliyo bayana unapomwamgalia kwenye macho na mwili wake ktk yale mahojiano
 
Ngoja tuwasubiri wajumbe wataamuaje siku ya uchaguzi, maana yeye ansema wengi wanamuomba aendelee.
 
Wapambe nuksi ndio wamempotosha mwamba!
Baada ya kuandaa lile igizo pale nyumbani kwake alipaswa ajipe muda mrefu wa angalau wiki 2 kupima kwanza upepo kama anakubalika kiukweli kabisa kwa wanachama wa kawaida kwa kiwango gani??
Sasa yeye akakurupuka akawajibu (ingawa aliwaita yeye!) Kwamba eti wampe siku 2 atawapa majibu kama atagombea ama lah
 
Wapambe nuksi ndio wamempotosha mwamba!
Baada ya kuandaa lile igizo pale nyumbani kwake alipaswa ajipe muda mrefu wa angalau wiki 2 kupima kwanza upepo kama anakubalika kiukweli kabisa kwa wanachama wa kawaida kwa kiwango gani??
Sasa yeye akakurupuka akawajibu (ingawa aliwaita yeye!) Kwamba eti wampe siku 2 atawapa majibu kama atagombea ama lah

Ni kweli kabisa
 
Back
Top Bottom