PreGE2025 Mbowe amjulia hali Tundu Lissu, Wateta kwa saa moja Gerezani

PreGE2025 Mbowe amjulia hali Tundu Lissu, Wateta kwa saa moja Gerezani

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Mbowe alitembelewa na Lissu wakati ule alipokaa mahabusu Kwa kesi ya Ugaidi

Vivyo hivyo ni uungwana Mbowe kumtembelea pia Lissu mahabusu wakati huu ambao naye ana kesi ya Uhaini

Baada ya kutembelewa na Mbowe gerezani, nategemea Chadema itaenda kushiriki Uchaguzi Mkuu 2025 kama wengi walivyoomba na ujumbe wake kupelekwa Kwa Mwenyekiti kupitia Mbowe hii leo
 
no reforms no election

retired chairman mbowe ,inabidi apewe majukumu yake ,heche awe na Dr slaa ,mbowe awe na lema

natamani kusikia mbowe akisema wamekamata mwenyekiti wa chama taiga,mdogo wangu TAL,hahaha
 
Wakuu!

Hawa G-55 watakuwa na hali gani huko waliko kama kweli Mbowe, anayedaiwa kuwa nyuma yao ameenda kumtembelea TAL?

===

Mwenyekiti Mstaafu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Freeman Mbowe akiambatana na Salum Mwalimu aliyekuwa Naibu katibu Mkuu wa Chama hicho Zanzibar pamoja na Daniel Naftal Ngogo, mwandani wa karibu wa kiongozi huyo Mstafu wa Chadema wamefika gereza la Keko Jijini Dar Es salaam na kumjulia hali Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Tundu Lissu leo Jumatano Aprili 16, 2025, majira ya saa sita Mchana.

View attachment 3306516
Kwa mujibu wa Jambo TV, wanadai waliwanasa viongozi hao wakiwa kwenye mazungumzo, kimeeleza kuwa wawili hao wamefanya mazungumzo kwa muda wa takribani saa moja, wakijadili na kuzungumza masuala mbalimbali.

Soma, Pia: Tundu Lissu ashtakiwa kwa Uhaini, arudishwa rumande, kesi yake kusikilizwa Aprili 24, 2025

Lissu Aprili 10, 2025 alirudishwa mahabusu baada ya kusomewa shitaka la uhaini katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kufuatia kushindwa kujitetea kutokana na kosa hilo kumnyima dhamana na nafasi ya kujitetea, akituhumiwa pia kuchapisha taarifa za uongo kwenye mtandao wa kijamii wa X akitarajia kupandishwa tena mahakamani Aprili 24 mwaka huu.

Chanzo: Jambo TV
Kufanya jambo la kiungwana Sana, lissu alishiriki Sana mbowe kuachiliwa akiwa gerezani.Mbowe asingeeleweka kutokwenda kumwona mwenyekiti wake wa chama...
 
Back
Top Bottom