Freeman Mbowe ni Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na maendeleo
CHADEMA akianza kuitumikia nafasi hiyo mwaka 2004 ambapo ameendelea kuishikilia mpaka sasa 2024
. Watu wengi wamekuwa na shauku ya kushuhudia uchaguzi ujao wa viongozi ndani ya Chama hicho ngazi ya taifa, jicho kubwa likiwa katika nafasi ya Mwenyekiti, nafasi ambayo imeshikiliwa kwa zaidi ya miaka 20 na Mbowe. Itakumbukwa pia Mbowe alikuwa ni moja kati ya waasisi wa chama hicho mwaka 1992.
Desemba 18, 2024 Wanachama wa CHADEMA walikusanyika Nyumbani kwa Freeman Mbowe kwenda kumshawishi agombee tena nafasi ya Uenyekiti CHADEMA kwa kipindi kingine ambapo inategewa uchaguzi wa kumchagua Mwenyekiti
utafanyika Januari 2025 kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na John Mnyika ambaye ni katibu wa chama hicho.
Kwa wakati huu wa Desemba tayari hatua za watia nia na uchukuaji wa Fomu pamoja na kurejesha fomu kwa wanaogombea nafasi Mbalimbali CHADEMA zimeanza ambapo miongoni mwa
waliochukua Fomu kugombea nafasi ya Uenyekiti ni pamoja na
Tundu Lissu ambaye kwa sasa ni Makamu Mwenyekiti Bara, CHADEMA.
Kumekuwa na machapisho yanayodaiwa kuchapishwa na JamiiForums, The Chanzo, Mwana Habari pamoja na Habari Digital huku yakiwa na jumbe zinazodaiwa kutolewa na Freeman Mbowe alipozungumza akiwa Nyumbani kwake baada ya wanachama wa CHADEMA kufika hapo mnamo 18, Desemba 2024 ili kumshawishi kuchukua fomu agombee tena nafasi ya uenyekiti, matamko dhidi ya Tundu Lissu, Rejea
hapa na hapa
Je, ni upi Uhalisia wa Machapisho hayo?
JamiiCheck imebaini kuwa machapisho yenye Nembo ya JamiiForums kama yanavyodaiwa Si ya kweli kwani hayajachapishwa na JamiiForums kwenye mitandao yake ya kijamii wala kutolewa na JamiiForums,
Chapisho moja lenye picha ya Mbowe, linasomeka kuwa "Lissu katunza fedha zake Ubelgiji, bado anawahadaa watu wamchangie gharama zake, huu ni unafiki wa kiwango cha juu" na lingine "Lissu na wenzake kama wamechoka Waondoke tu CHADEMA: Mbowe"
Maneno haya Si ya kweli kwani Mbowe
alipozungumza na Wanachama waliofika Nyumbani kwake tarehe 18, Desemba hakuzungumza kauli hizo mahali popote.
Aidha kwenye posta hizi kuna utofauti wa mambo kadhaa kutoka kwenye posta halisi za Jamiiforums
- Font zilizotumika hazitumiwi na JamiiForums,
-Uwepo wa Tag ya Habari kwenye posta ya Siasa ni tofauti na tag inayotumiwa na JamiiForums
-Rangi zilizopo kwenye posta hii hazitumiwi na Jamiiforums kwenye posta za Siasa
-Uwepowa neno Ziadi kwenye taarifa ambayo haina posta zaidi ya moja
-JamiiForums haitumii picha kwa mtindo kama uliotumiwa kukiwa na picha zaidi ya moja.
Je, Mbowe amesema anamuonya Lissu?
Kufuatia
Mkutano huo imeibuka posta inayoonekana kama ya The Chanzo, yenye picha ya Mbowe na Lissu ikiwa na ujumbe unaosomeka: Namuonya Lissu waziwazi - hana uwezo wa kifedha wa kupambana na mimi. Hii tabia ya kuombakuomba haitamfikisha popote.
JamiiCheck imebaini kuwa Taarifa hiyo Si ya kweli kwani kauli kama hiyo hakitolewa na Mbowe alipozungumza na wanachama wa CHADEMA waliofika Nyumani kwake, aidha Posta hiyo haikuwahi kuchapishwa kwenye mitandao ya kijamii ya The Chanzo.
Vile vile Mbowe alipokuwa akizungumza na wanachama waliofika kumshawishi agombee tena nafasi ya Uenyekiti alieleza kuwa: Nimeambiwa mimi ndiye ninaeleta mzigo peke yangu CHADEMA, na kama unataka tushindane kwa mizigo basi tushindane
Upi uhalisia wa Madai kuwa Mbowe asema ameijenga CHADEMA kwa jasho, fedha na damu, haiwezi kuiachia kwa wepesi?
Kupitia
ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck imebaini kuwa Posta inayodaiwa kuwa ya Mwanahabari Si ya kweli kwani haikuwahi kuchapishwa kwenye mitandao ya kijamii ya MwanaHabari,
Vilevile Freeman Mbowe, alipokuwa akizungumza na Wanachama wa CHADEMA waliofika nyumbani kwake kumshawishi agombee nafasi ya Mwekiti kwa mara nyingine hakutamka kauli kuwa chama hikinimekijenga kwa jasho, fedha na damu. Sihitaji huruma ya mtu, Siwezi kukiacha kwa wepesi namna hiyo hali inayofanya madai haya kuwa Si ya kweli.
Aidha, kumeibuka posta inayodaiwa kutolewa na Habari Digital yenye picha ya Mbowe huku ikiambatana na ujumbe unaosomeka kuwa, nina kila kinachohitajika- Fedha zipo, Watu wapo-uchaguzi Si mazungumzo ni Vita ya ushindani wa kweli.
JamiiCheck kupitia Ufuatiliaji wa Kimtandao umebaini kuwa Taarifa hiyo inayodaiwa kuchapishwa na Habari Digital Si ya kweli kwani haikuwa kusemwa na Mbowe nyumbani kwake alipozungumza na wanaCHADEMA walifika kumshawishi agombee, aidha haikuwahi kuchapishwa kwenye mitandao ya kijamii ya habari Didital.
Je, Mbowe alisema Lissu ni Muongo anatengeneza makundi katika chama?
Kupitia
ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck imebaini kuwa Posta inayodaiwa kuwa ya Jambo Tv Si ya kweli kwani haikuwahi kuchapishwa kwenye mitandao ya kijamii ya Jambo Tv
Freeman Mbowe, alipokuwa akizungumza na Wanachama wa CHADEMA waliofika nyumbani kwake kumshawishi agombee nafasi ya Uenyekiti kwa mara nyingine hakutamka kauli kuwa Lissu ni Muongo anatengeneza makundi ndani ya CHADEMA hali inayofanya madai haya kuwa Si ya kweli.