Mbowe anaungwa mkono na Wajumbe wapiga kura wengi ndani ya CHADEMA, Lissu anaungwa mkono na umati mkubwa wa wapiga kelele

Mbowe anaungwa mkono na Wajumbe wapiga kura wengi ndani ya CHADEMA, Lissu anaungwa mkono na umati mkubwa wa wapiga kelele

Machawa ya mzee Mbowe hayana hata aibu ,hivi jaribuni kuweka wasifu wa msomi Lissu na wasifu wa mzee Mbowe ndio mtajua kuwa makelele yote mnayorushia Lissu ni kwa ajili ya jambo moja tu, Lissu ni mkuwbwa mno kwa mzee Mbowe kwa Fikra ,mawazo na akili kwa ujumla .Acheni uwoga jamani ,kama mnavyojiita cham cha demokrasia ni wakati wa kuthitisheni hilo na si porojo.
LISU anaakiki lakini Hana sifa ya kuongoza taasisi
 
kumbe hili kombora la maana sana ni pilipili gentleman? :pedroP:

pole na samahani sana my friend, Lakini itabidi uzoeee tu maana hakuna namna nyingine sasa.

Freeman Aikaeli Mbowe anaenjoy kura nyingi zaidi za wajumbe wapiga kura kumchagua mwenyekiti wa Taifa chadema, huku Tundu Antipas Lisu akiinjoy makelele, mdomo na useless mass popularity, ambayo haitasaidia chochote kwenye harakati za kutafuata uongozi wa juu chadeama:BASED:
Kwani mbowe katangaza lini anagombea uwenyekiti wa chadema?
 
gentleman,
bado kuna zaidi ya hoja arobaini ziko tayari kubainishwa humu jukwaani, na una uhuru na haki ya kuzifuatilia au kupuuza,

lakini kiukweli zimejaa madini ya maana sana ya kitaifa na kimataifa, lakini pia mambo mengine ni pamoja na haya ambayo yanahusu chadema iliyogawanyika na uchaguzi wao wa ndani..

hata hivyo,
katika joto la uchaguzi wa ndani wa chadema, kati ya kanda 10 za kiutawala, kanda 4tayari zinamuunga mkono chairmani Mbowe waziwazi kabisa, kwenye azma yake ya kutaka kuingoza chadema kwa awamumu nyingine ya miaka mitano. kanda hizo ni pamoja na ile ya NYASA, PWANI, KASKAZINI NA VICTORIA.

Bado nafatilia kwa karibu ikiwa kuna kanda hata moja ina saporti azma ya Tundu Lisu kua mwenyekiti wa chadema taifa, zaida ya wanyanturu wachache ambao ninawafahamu, wanamuhadaa kiongozi huyo kwamba eti atashinda uchaguzi huo, hali yakua hana numbers:BASED:
Hahaha hizo ni ndoto, zinamuunga mkono kwa nafasi ipi? Mbowe hajatangaza kugombea kaka, kiherehere Cha nn? Wanachadema wataamua kupitia kura muda ukifika
 
Hivi kusini Lindi +Mtwara sio Kanda maana siwasikii viongozi wa chadema tokea huko.
Na wapo upande wa Mwamba VS Lissu.???
Wao wametulia wanasubiri wagombea watie Nia na kuchukua fomu kwanza.Hawataenda kama Kanda, Kila mmoja atampigia mgombea amtakaye, kura ni Siri na ndio demokrasia
 
Nani aliyekudanganya kuwa kanda zinapiga kura kama Block? Maana kuna mikoa Mbowe alivuruga uchaguzi mfano Nyasa unadhani wale wajumbe wata endorse Mbowe? Au wajumbe wa BAVICHA watampa mbowe wamuache reformist Lissu?

Pia wale wajumbe wanaangalia upepo ulivyo kwa wanachama, hata kama watakuwa ni machawa wa Mbowe lakini huko wanapotoka naamini wanachama watawapa maelekezo ya maoni yao hivyo wakimchagua mtu ambaye sio popular kisa tu ni machawa basi wajue huko wilayani wakirudi watakuta ofisi zimefungwa na makufuli.

Wasikilize maoni ya huko majimboni wasitumie utashi binafsi.
Haahaa umesema vyema, Kuna kiongozi mkubwa tu wa chadema anasema mtaani kwake alikuwa akipata maoni, wengi wanasema wanataka mabadiliko japo yeye anamuunga mkono mwenyekiti mbowe
 
Ni sawa na sababu kubwa ni kwamba mbowe ana uwezo kifedha wakati kiasi hana.lkn kuna haja gani kuendelea kukivuruga chama kisa mbowe abaki kwenye uenyekiti?kwa nini asiwaachie chama vijana yeye akawashauri.kwa mtaji hatutegemei cdm kuja kuwa chama mbadala hata siku.watanzania wa sasa si jana wanaelewa sana kilicho chini ya kapeti.rudisheni imani ya chama kwa wananchi.achaneni kuchaguana kisa fulani ana uwezo.kama ndivyo chama kitapoteza mwelekeo.
Shida kubwa kwa chadema hasa uchawa, Mbowe juzi aliropoka hovyo eti miaka 20 ya kukomaa, Ile ilikuwa hoja dhaifu, mtaani wananchi wanadai hivi mbowe akipata urais wa nchi atakubali kukaa miaka mitano?
 
Ana shinikiza tu wajumbe wamchague, so anaitisha uchaguzi fake ili kuonyesha chadema kuna democracy.

Uchaguzi huo ni kama wa Rais Mseven wa Uganda, unadhani Uganda ya Mseven hufanya genuine election? Au mseven huzuga tu kuwaonyesha donors kuwa tumefanya uchaguzi.
Haahaa umenikumbusha kwa kagame, ushindi 90%
 
Haahaa umesema vyema, Kuna kiongozi mkubwa tu wa chadema anasema mtaani kwake alikuwa akipata maoni, wengi wanasema wanataka mabadiliko japo yeye anamuunga mkono mwenyekiti mbowe
heading ya hoja kuu imebeba uzito mkubwa mno gentleman,

tofautisha actual votes na popularity votes, itakusaiadia sana gentleman ili usiumbuke na kuaibika 🐒
 
Shida kubwa kwa chadema hasa uchawa, Mbowe juzi aliropoka hovyo eti miaka 20 ya kukomaa, Ile ilikuwa hoja dhaifu, mtaani wananchi wanadai hivi mbowe akipata urais wa nchi atakubali kukaa miaka mitano?
chadema si kuna uhuru wa kutoa maoni gentleman, mbona kama unababaika na maoni ya kiongozi huyo wa mbozi, hali ya kua Hata lisu aliwahi kusema chaguzi za chadema zinanuka rushwa, ila hiyo haikua shida?

ni vizuri kuheshimu maoni na mitazamo ya wanachadema tofauti tofauti, hakuna haja ya makasiriko 🐒
 
Yes na Busara ya collective responsibility anapenda kujijengea ufalme wake binafsi ubinafsi
ni kwamba muungwana ni mbinafsi mno, right?

ni mgonjwa na dhaifu sana kwenye suala la collective responsibilities, na kwamba utawala bora kwake ni kama kituo cha polisi right?🐒
 
Friends, ladies and gentlemen.

Kwa kifupi kabisa, ukipima kwa jicho la rohoni kabisa, numbers of votes zinamfavor chairman Mbowe, huku useless mass popularity ikimfavor vice chairman Lisu, ikiwa uchaguzi wa ndani wa chadema utafanyika mwaka huu 2024 au 2025.

There is no way Lissu can beat Mbowe in the ballot box, because Mbowe has real numbers, than Lisu has.

Uchaguzi ni mchakato unaozingatia na kutegemea zaidi numbers kwa washindani ili kushinda.

Ni dhahiri kanda za Pwani, Nyasa, Victoria na Kaskazini ni ngome imara za mwenyekiti wa sasa wa chadema Taifa, na tayari katika ujumla wake zimejipambanua kumuunga mkono.

Kanda ya kati, nadhani sote tunafahamu uhasama kati ya Lissu na Kigaila. Ni majirani wasioelewana hawa.Tuchukulie kanda hiyo itakua imegawanyika.

Kanda ya Viktoria kwa kamanda Ezekia Wenje, kama kawaida Taifa zima linafahamu, huyo ndie makamu mwenyekiti wa chadema Taifa ajae, ambae pia anamuunga mkono Dr. Freeman Aikaeli Mbowe kua mwenyekiti wa chadema Taifa.

Nguvu ya Ezekia Wenje kisiasa ndani ya chadema, imemlazimisha na kumtoa mtu maarufu sana ulingoni kwenye kinyang'anyiro cha uongozi wa chama Taifa.

Kanda za Serengeti, Magharibi, Kusini n.k ni kama wanatafuta platforms na namna ya kujipambanua wako upande wa Mbowe au Lisu.

Kwa ujumla, mizizi ya mwenyekiti wa chadema Taifa wa sasa ni mirefu, imara na imejikita sana ndani ya chadema. Kuing’oa yahitajika mipango mikakati ya kisayansi, Lakini pia nguvu, bongo kali, ushawishi wa hali na mali na jitihada za ziada. Asilimia kubwa ya viongozi wa chadema wa kanda, mikoa na wilaya wanatokana na mapendekezo na baraka za mwenyekiti wa chadema wa sasa.

Kwa maoni na mtazamo wako kisiasa, kati ya kanda 10 za kiutawala zilizopo chadema, unadhani ni kanda zipi zinanaweza kuunga mkono azma ya Tundu Lisu kua mwenyekiti wa chadema Taifa badala ya Freeman Mbowe?🐒

Mungu Ibarki Tanzania
Mbowe asije jidanganya kubatle na lissu kwenye sanduku la kura, atapata aibu ambayo hajawahi kuipata maisha yake yote. Ushauri kwa mbowe aachie tu kiti ili astaafu kwa heshima ving'ang'anizi wa madaraka wanakuwaga na mwisho mbaya sana.
 
Wao wametulia wanasubiri wagombea watie Nia na kuchukua fomu kwanza.Hawataenda kama Kanda, Kila mmoja atampigia mgombea amtakaye, kura ni Siri na ndio demokrasia
Tutajie hata majina yao tuwajue as kanda zingine tuwajuavo
 
Back
Top Bottom