Uchaguzi 2020 Mbowe anavyomfitini Tundu Lissu, Nyalandu ashinda kura za maoni

Hii habari kama ni kweli na hao uliwataja asilimia 100 nasadiki maana hata kujitoa Mbowe ni mkakati ili lisu hasipenye ila wanachezea shilingi chooni kama watampitisha Nyarandu nafikiri Lissu atakwenda ACT kushirikiana Membe na ndio itakuwa mwisho chadema
 
Hakuna kitu Kama hicho mkuu ...lazuma majina yatoke matatu kwenda mkutano mkuu...huko ndo utajua kuwa alikuwa anapewa moyo tu ...yaani kipigo atakachopewa nyarandu huenda asibakie chadema...ngoja waje wajumbe kutoka mikoani
 
ujio wa Lissu naona watu wame panick kinyama yaani.

juice ya pilipili kichaa yaja, kaeni tu mkao wa kukimbilia Comoro (sijui kwa mtumbwi au kupiga mbizi mtajaza wenyewe).

habari ni.... Lissu anatinga timu Jumatatu ijayo na ndiye mgombea urais wa coalition ya upinzani kupitia chama chake cha Chadema.

habari ndiyo hiyo!
 
Mbna mie sijaelewa huo muenendo wa upigaji kura, khaaaaah
 
Sasa mleta mada hufikirii kama huyu mtu wakati hayupo kapitwa kwa kura 4 tu. Jee akiwepo mwenyewe itakuwaje?
 
Mchakato ndani ya kamati kuu ndani ya Chadema umekamilika ambapo kamati kuu ya Chama hicho imechagua watu watatu kwenda kwenye baraza kuu la Chama.
Katika kura zilizopigwa ndani ya kamati kuu, Ndugu Nyalandu amepata kura nyingi zaidi kuliko Lissu.

Hata hivyo tafsiri ya kura hizi ni kuwa Kamati kuu ya Chadema ambayo ndiyo uongozi wa Chadema hauamini kuwa Lissu ni mgombea bora kuliko Nyalandu.

Yaani kamati kuu ya Chadema kiufupi haiamini kuwa Ndugu Tundu Lissu anaweza kuwa rais mzuri kuliko ndugu Lazaro Nyalandu.

Hii maana yake ni kwamba Uongozi wa Chadema, umetuma Meseji kwa Wanachadema na Watanzania kuwa, Uongozi huo ungependa ndugu Nyalandu ndiye awe mpeperusha bendera ya chama hicho dhidi ya Rais Magufuli.

Sasa ni jukumu letu sisi wananchi kuanza kujiuliza, kuwa Uongozi wa Chadema umeona kasoro gani kwa Tundu Lissu hadi usiamini kuwa yeye ndiye anayefaa zaidi kuwa mgombea kuliko mwanachama yeyote wa CHADEMA katika waliotia nia?

Huenda uongozi wa Chadema una kitu ulichokiona kwa ndugu Lissu kiasi kwamba kupitia kura zao unatuma meseji kwetu kuwa Lissu si bora kuliko Nyalandu. Je ni kitu gani hicho?

Mimi nafikiri kuwa yule aliyeko jikoni ndiye anayejua joto lililoko huko, Sasa kama Uongozi wa juu wa Chadema haumuoni Lissu kama namba moja, je ni sahihi sisi kuanza kumuona kuwa ni mtu sahihi?

Nadhani maamuzi haya ya kamati kuu ni mawazo ya kutufikirisha sana sisi wapiga kura. Hii ni. meseji ya dhahiri kwetu kutoka kwa uongozi wa CHADEMA kuwa, kwenye uchaguzi huu ujao, miongoni mwa wagombea, uongozi huo unaamini kuwa kuna mtu ndani ya Chadema na nchi hii mwenye sifa zaidi kuliko Lissu anayepaswa kuwa raisi La sivyo kwa nini haukumpa kura nyingi zaidi Lissu kushinda wengine?

Tutafakari!
 
Reactions: UCD
Ngoja waje wenye Sacco's na mapovu yao!
 
Misile nilikiwa nakuheshimu sana lakini leo umeonesha uwezo mdogo wa kung'amua Mambo. Kilichofanywa na Chadema ni camouflage. Yaani Diversion. Ktk maswala ya inteligensia ni aina fulani ya kumpoteza mwelekeo adui adhani A ni B kumbe A ni A tu .
Nadhani umenielewa.
 
Kwa hiyo mgombea wa saccos lazima afichwe kwanza?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…