Uchaguzi 2020 Mbowe anavyomfitini Tundu Lissu, Nyalandu ashinda kura za maoni

Uchaguzi 2020 Mbowe anavyomfitini Tundu Lissu, Nyalandu ashinda kura za maoni

Hivi siku hizi JF imekuwa kijiwe au niseme nini? Is this still a reputable forum? Hii thread ni ya uongo na mbaya zaidi hizo asilimia zimewekwa hapo hata mbwa koko hawezi shindwa hesabu hiyo. Wapiga kura 29 moja iharibike halafu eti kila mmoja apate hizo asilimia zilizowekwa hapo? Ama kweli nilijisemea kuwa IF niliyojiunga 2008 just after kufuata kwa Jambo Forum siyo hi ya leo. Kitendo cha kutangaza kaxi waziwazi na kujaza watu wenye utata ndiyo ilikuwa mwisho wa ubora wa Forum hii.
Achana na huyu mbwa koko
 
*Lazaro S. Nyalandu - 28* ( 100%)
*Tundu Antipasi Lissu - 24* (86%)
*Dr. Mayrose K. Majinge - 23* ( 82%)

Kura 28. Then hizi asimilia mbona haziadd up?
 
*Lazaro S. Nyalandu - 28* ( 100%)
*Tundu Antipasi Lissu - 24* (86%)
*Dr. Mayrose K. Majinge - 23* ( 82%)

Kura 28. Then hizi asimilia mbona haziadd up?
Walikuwa watu 28. Walipiga kura kila mtu kura anaandika majina ya watu watatu anaaoona wanafaa. Hivyo Nyalandu alipata kura za wajumbe wote. Skiliza hayo mahojiano wameelezea vizuri. Ila nimegundua Nyalandu yupo kwa kazi maalum. Si bure.
 
kura halali 28..
nyalandu 28
lissu 24
mwingne 23

hio hesabu iko sawa kweli? au mim ndio sielewi
Hizo percentage umeziweka vibaya, siku nyingine hakikisha ukiweka percentage jumla yake isizidi 100%.

Inshort umeandika uongo mtupu.

Inategemea na voting system inyotumiwa na CHADEMA. Iwapo wanatumia approval voting system ambapo kila mpiga kura anaweza kuchaguwa watu wawili au watatu, basi idadi ya percentages za wagombea zitazidi 100, ila kama wanatumia one person-one vote, lazima percentages ziwe ni 100.
 
Hizi clip zako kwangu hazichezi, seems your file format is not supported in my Android file format.
Nimefungua hio link ya youtube kwenye simu yangu. Nimeona kweli Nyalandu anasema kuwa alipata kura zote, asilimia 100. Akifuatiwa na Lisu then Myrose. Na Kasema pia wajumbe walipiga kura tatu kila mmoja.

Jamaa anaongea ukweli.
 
Kwenye mgawo wa percentage ndio sijaelewa, huenda nilikimbia hesabu

Ni mwongo tu huyo...

Anasema;

å Idadi ya wapiga kura jumla 29
å Matokeo anasema;
¶ Nyalandu 28
¶ Lisuu 24
¶ MayRose 21

Yaani, kajikamatisha mwenyewe kwa uongo!!
 
Ndugu wana bodi.

Kupitia vyanzo vyangu makini vya kimtandao nimepokea taarifa kuwa kamati kuu ya CHADEMA imefanya uamuzi kwa kupiga kura. Uamuzi wa kupendekeza nani awe mpeperusha bendera mkuu wa CHADEMA katika uchaguzi wa mwaka huu 2020. Yaani mgombea Urais.

Ukweli ni kwamba kati ya watu 8 waliorudisha fomu ni watu wawili tu wenye ushindani.
1. Mh Tundu Lissu
2. Mh Lazaro Nyalandu.

Hawa wote ni wenyeji wa mkoa wa Singida na wote ni wajumbe wa kamati kuu ya chadema taifa.

Binafsi nilishitushwa sana kiasi cha kubadilisha mapigo ya moyo wangu baada ya kuona matokeo ya kura za maoni za kamati kuu ya CHADEMA.

Kilichonishitua ni kuona ``think tank`` ya CHADEMA inaamini Mhe Lazaro Nyalandu ni bora kuliko Mhe Tundu Lissu aliyekinga chama kwa damu yake na risasi 16 ambazo mpaka sasa hatujajua Kama kweli zilikuwa zinampiga au malaika walitega migongo yao ndio ikapigwa lisasi kwa niaba yake? Kwasababu mpaka sasa watanzania na wanachadema bado wanajiuliza huyu jamaa aliponaje!!

Bila kutia chumvi yafuatayo ni matokeo ya tatu bora za maoni ya kamati kuu ya CHADEMA

KURA ZA WAGOMBEA URAIS JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

KAMA ZILIVYOPIGWA NA KAMATI KUU YA CHADEMA, DAR ES SALAAM, JULY 22, 2020

*IDADI YA KURA ZILIZOPIGWA - 29*
*KURA ILIYOHARIBIKA - 1*
*IDADI YA KURA HALALI -28*

*Lazaro S. Nyalandu - 28* ( 100%)
*Tundu Antipasi Lissu - 24* (86%)
*Dr. Mayrose K. Majinge - 23* ( 82%)

Haya ndiyo majina yatakayo kwenda Baraza Kuu la CHADEMA.

Baada ya matokeo haya nikaanza upelelezi kujua nini kimejiri Kaka Tundu Lissu azidiwe kura na mh Lazaro Nyalandu.

Uchunguzi wangu umebaini kuwa Mhe Aikael Mbowe na Nduguye Mhe Godbless Lema ndiyo walikua nyuma kuhakikisha kuwa Lazaro Nyalandu anamzidi kura za maoni Mhe Tundu Lissu katika maoni ya Kamati kuu.

Kwa ufupi naambatanisha chat za Whatsapp kati ya Mhe Lema na Mhe Mbowe baada ya matokeo ya kura hizo.

Na nina ushahidi thabiti watu wanne waliomnyima kura Lissu ni wafuatao.

1. Freeman Mbowe.
2. Godbless Lema.
3. Halima Mdee.
4. Esther Bulaya.

Pia nichukue wasaa huu kuwajulisha Mhe Esther Matiko na kaka Patrick Ole Sosopi kuwa makini katika siasa zao ndani ya chadema Mwamba hawatazami kwa jicho rafiki.

Wajumbe wa baraza kuu na mkutano mkuu wa chadema taifa wanaopinga mpango wa Mwamba kumuunga mkono Lazaro Nyarandu na ambao wanamuunga mkono mh Tundu lissu,mjiandae pia kisaikolojia yajayo yanafurahisha.

Sasa nimeanza kuamini kwanini wanachama wa chadema na viongozi wengi walikuwa wanatimkia vyama vya Nccr mageuzi na ccm wakisema Kuna tatizo naona sasa linaanza kuwa dhahiri machoni kwa watanzania na wanachama wa chadema.

Ni wenu.
hivi kwa mfano lisu amekuwa raisi, mdee atakuwa nani?? bulayo naye atakuwa nani ?? fikiria mnyika mbowe ,huoni ni kituko?? Nyalandu kazi anaiweza na imekamilika akishindwa membe yupo, kuhusu lisu ........
 
Dah, maisha yanaenda kasi sana! Yaani Lissu apitwe kura na Nyarandu tena ndani ya Chadema! Ndio maana sitaki unafiki wa kisiasa.
Kama ni kweli basi hawajitambui. Kusubiri mtu atoke CCM wamsimamishe Urais ni kichekesho, means wenyewe hawajiamini
 
Huu ni uzushi kama huu
Screenshot_20200616-151745.png
 
Duuu....yajayo yanafurahisha....

huu unaweza kuwa uchangonishi.....umetaja majina ya wachaga tu, Bulaya umemweka ili kufukia dhamira yako ovu ya ukabila.


hizo kura zilipigwajepigwaje, maana wajumbe 29, mara mwingine 28, mwingine 24, sijaelewa kabisaaa...
Mleta uzi atakuwa libashite fulani hivi linajiharishia kusikia Mwanasheria msomi Tundu Lissu anarejea Bongo land.
 
Mkubwa thread ni ya kweli. Walipiga kura tatu tatu kila mtu. Sikiliza mahojiano Nyalandu anakiri mwenyewe wakati anahojiwa na Jenerali Ulimwengu.
Mkuu. KAMA ni kweli ni serious matter. Na hakika mark my Words Nyalandu yuko kazini. Time will tell. Not far
 
Mpaka muda huu hao Chadema bado hawajakanusha huenda basi ni kweli. Mungu nisaidie Siasa niwe Mshabiki tu wa kupita na si zaidi.
 
Back
Top Bottom