Uchaguzi 2020 Mbowe anavyomfitini Tundu Lissu, Nyalandu ashinda kura za maoni

Yaani wamemnyima Lissu kugombea?
Hahaha CDM hameni chama tu muacheni mbowe na genge lake, hiki chama kina mambo ya kijinga sana, who the f***k is Nyalandu? hakuna hata mtu anamjua mnataka aende kushindana na Jiwe na Membe? hampo serious. Nilijua CDM ina washenzi sikujua ni level hii.
 
Hizi taarifa mnazipata wapi?
Najua wewe alshabaab wa Act unajua unachokifanya
 
ninaona dalili kwamba ndani ya kamati kuu ya cdm mna watu wenye busara za hali ya juu sana
wanayaangalia masuala hadi nyuma ya pazia.
TL anafaa kabisa kuwa kiongozi tena mzuri tu but not to the presidential level.
ndg zangu urais ni zaidi ya kujenga hoja na kuwa na misimamo mikali kutetea hoja zako.
ndio maana tunamkumbuka sana mhe. Kikwete, ndio maana baba wa taifa mwl.J.K.Nyerere
alikiri "NINGEAMUA KUWA DICTATOR KWA KATIBA HII NINGEKUWA
rais ni top decision maker wa masuala yote muhimu yanayohusu nchi,
watz wenzangu tusiongozwe na ushabiki, tusiongozwe na kuangalia nani anaikosoa sana serikali,
wala tusiongozwe na sympathy bali tuwe makini kupata mtu anayeyajua matatizo ya watz, ambaye atakuwa
tayari kuwasikiliza watz bila kujali misimamo yake na asiyekuwa jazba. kwa bahati nzuri tumekuwa na marais
watano sasa na wote tunawajua sifa zao tutumie hiyo kama ubao wetu wa kujifunzia tupate jibu nani anafaa kuwa rais wetu
NGWABEJA SANA
 
Mtu unaandika uongo kwa kutumia namba harafu mbaya zaidi hata hesabu haujui, Mtihani huo.Idadi ya wapiga kura ni 28, Nyarandu alipata 28,Tundu Lisu 24 na magige 23.Kama nyarandu tuu alipata kura 28, je hizo za akina Lisu na Magige zilitoka waapi??.
 
Ni bora ungeandika habari za Membe wenu Lissu tuachie sisi wanachama wa CHADEMA
 
Umejuaje mkuu 'ikipendaroho'?

Wewe utakuwa una akili kali sana ya kutambua vitu.

Hilo ndilo lengo la mleta mada hii hapa.
Na hilo ndiyo lengo lake kuu hata kama hajui kura zilizopigwa huko chamani
 
Aliyeonyesha uwezo mdogo ni wewe, kama huoni yote hayo yanayotendeka ili Lissu asipeperushe Bendera ya chadema, na wakishamkata wanajitahidi tatizo la lissi lisikigawe chama
 
Kama sasa tuna amiri Jeshi !! Lissu ashindwe kuwa amiri Jeshi ?!. Haya ni maneno ya kejeli.

Inatakiwa mtu ambaye ukimtaja hata kwa wazee vinijini , anapata kura za bila kujihoji huyu ni nani ?!. Na Lissu ni candidate mzuri kwa sasa ndani ya Cdm .
 
Boss usiseme yote, waache wasigundue lolote mpaka muda ufike
 
Hii habari ya kusema mpango wa Mungu sio nzuri.......,mnamfanyaga kuwa Mungu ni mwongo....hata Lowasa mlidai mpango wa Mungu......kiko wapi....yuko wapi? Mungu gani labda?
Kila kitu kinapotokea ni mpango wa Mungu hivyo Lowasa alipokuja Chadema ulikuwa mpango wa Mungu ndiyo maana tulipata wabunge wengi sana,Na baada ya yeye kushindwa zile njama zake aliamua kurudi kwao yeye pamoja na rafiki yake Sumaye hivyo ilikuwa mpango wa Mungu kukinusuru chama toka mikono michafu ya ccm.
 
kura halali 28..
nyalandu 28
lissu 24
mwingne 23

hio hesabu iko sawa kweli? au mim ndio sielewi
Hizo hesabu ni za fantasy. Ni hesabu za kizazi kijacho cha mwaka 2100. Kwa Leo hatutazielewa.

Över.
 
wewe ndiye mshenzi unayedhani kuhama chama ndiyo suruhisho!!!!!
 
Hizo percentage umeziweka vibaya, siku nyingine hakikisha ukiweka percentage jumla yake isizidi 100%.

Inshort umeandika uongo mtupu.
Mi nikajua ni style mpya ya upigaji kura wa chadema kuwa labda kila mgombea anapigiwa ndiyo na hapana. Hivi chamani bado kuna viroba ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…