Uchaguzi 2020 Mbowe ashindwa kutetea Ubunge wake katika Jimbo la Hai

Uchaguzi 2020 Mbowe ashindwa kutetea Ubunge wake katika Jimbo la Hai

WanaJF,

Katika hali ambayo ilikuwa inatarajiwa na wengi ni kwamba Mgombea Ubunge wa Jimbo la Hai kupitia tiketi ya CHADEMA ambae pia ni Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa amegaragazwa vibaya sana kwa kuambulia kura 27,000 tu wakati mshindani wake Mgombea wa jimbo hilo kwa tiketi ya CCM amefanikiwa kujizolea kura zaidi ya 80,000.

View attachment 1615231
View attachment 1615230
Mgombea Ubunge kupitia CCM Saashisha Mafuwe, ameibuka mshindi katika Jimbo la Hai kwa kupata kura 89,786 huku mpinzani wake Freeman Mbowe wa CHADEMA akipata kura 27,684.

Hivyo ametangazwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Hai.


Kitendo cha Mbowe kukataliwa vibaya na wanaHai kwenye uchaguzi huru na haki kunatoa somo kwa wana CHADEMA na Watanzania kwa ujumla kuwa picha halisi ni kwamba Mbowe amechokwa na ushindi wake ndani ya chaguzi mbalimbali ndani ya CHADEMA unawezekana kwa sababu ya magumashi tu na sio vinginevyo.

Maamuzi ya wanaHai yamefanya Watanzania tuelewe kiundani kuwa bwana Mbowe bila shaka yoyote amekuwa akilazimisha kuendelea kuongoza CHADEMA na usanii wake wa kujifanya anakubalika umekuwa EXPOSED!

Kwa heshima kubwa nitumie nafasi hii kuwapongeza wana Hai kwa maamuzi sahihi na pia kuwapongeza CCM kwa kuukata mkorosho jimboni hai kwa kutumia Topaz tu.

Pole sana Bwana Mbowe.
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Amenuia Mbowe, Lema, Heche, Sugu, Msigwa, Mdee, Bulaya, Ruge, Peneza, Kishoka wasirudi mjengoni.
mkuu, inaumiza sana , yani mtu unaiba hadi inapitiliza ..dhuluma haiwezi kuwafikisha mahali popote
 
Tofauti ya kura elfu 60 ni kubwa Sana, hapa mbowe akiri kuwa muda umemtupa mkono,

Lakini si mara ya kwanza mbowe kushindwa vibaya,

Hata 2005 kwa kura za Urais alipata kura laki sita tu.

Kifupi ni kuwa Mbowe analazimisha kubakia madarakani Chadema.
 
Maskini Mbowe, wale body guard wake wenye miwani ya kuchomelea milango na v8 ya kambi ya upinzani bungeni ndio basi tena, sijuhi anarudi kwenye kazi yake awali? Siasa bwana,
Untitled.jpg
 
Kwa niliyoyaona katika uchaguzi huu kiukweli shetani ana nafuu ,mikakati iliyopangwa usiku wa kuamkia uchaguzi nilipoisikia masikio yaliwasha

1. Mawakala wasipewe nakala ya matokeo na ile nakala itakayobandikwa iwekwe gundi nyingi ili ichanwe haraka baada ya kubandika kabla raia hawajayaona matokeo.

2 Matokeo yakifika kituo cha kujumlishia yatapikwa upya kuwabeba jamaa bahasha zisifungwe.

Yaani itoshe tu kusema UCHAGUZI ULIKUWA NI KITUKO CHA KARNE


🤣🤣🤣
 
Miaka 5 iliopita kuna changamoto za APA na pale ila walijitahidi kwa namna moja, lakini nkiangalia upinzani ni bora ccm iendelee milele na milele,

Walahi tena na mimi nakwambia afadhali ccm ya Magufuli kuliko upinzani wa Lissu.

Yaani kama wabunge wa upinzani walishindwa kumpongeza magufuli kwa namana anavyodili na miradi ya maendeleo, basi hawatapata rais wa aina ya magufuli tena.
 
kufanya kosa sio kosa bali kurudia kosa ndo kosa....
2015 tulibelieve badala ya kufanya reasoning na yalikuwa maamuzi mazuri kwa kipind hicho maan tulipata positive impact
positive kwako kwangu huwezi mchukua fisadi ukamleta kwenye chama ilimradi ushinde uchaguzi. tunaichukia ccm kwasababu ya ufisadi alafu huyo fisadi mnamkaribisha tena. mimi uchaguzi huu sikupiga kura kwa kukataa upuuzi huu
 
Walahi tena na mimi nakwambia afadhali ccm ya Magufuli kuliko upinzani wa Lissu.

Yaani kama wabunge wa upinzani walishindwa kumpongeza magufuli kwa namana anavyodili na miradi ya maendeleo, basi hawatapata rais wa aina ya magufuli tena.

Ni bora tupate tu chama kipya cha upinzani, watu wenye akili
 
OKW BOBAN SUNZU nilimweleza kuwa ana mikosi, anashabikia simba inachapwa na sasa anashabikia Toto tundu nalo litachapwa asubuhi. 80,000 kwa 27,000 ati watu waandamane wakati watoto wake wapo ulaya. Huyu mbinafsi sana. Natafuta ile clip ya OCD niiweke alisema ukweli. 'Hivi mnadhani mnaweza kumshinda?" na 'wewe unategemea kushinda' . Anatakiwa awe IGP.
hakuna mkosi wowote. Iko wapi ushindani wa haki itoshe kusema nimeshindwa. Kwenye mpira ni mchezo wa wazi najua sikufanya poa. ila kwenye uchaguzi niko vizuri na imara
 
Back
Top Bottom