Uchaguzi 2020 Mbowe ashindwa kutetea Ubunge wake katika Jimbo la Hai

Uchaguzi 2020 Mbowe ashindwa kutetea Ubunge wake katika Jimbo la Hai

Yaani kwenye msimu wa Kampeni ulitaka aseme kuwa Lissu hajaifuta CCM?
Bado kinda yule, unajua ukizidisha uongo watu wanachukia. Hapa JF tunataka kupata taarifa za ukweli si ushabiki wa kitoto kama wa akina Erythrocyte na marafiki wake. Hata Yeriko Nyerere nilimsangaa kama si kumshangaa. Dada yangu Sky Eclat namjua hata kwa sura ila alichokuwa anaandika hapa, mungu anajua.

Hivi unaweza kumwacha mtu anayependa maendeleo ya Tanzania kidhati umchague Tundu Lissu mbinafsi na mtukanaji.

Imagine, watu wakaanza kumsifia JK aliyeuza nchi hii! Watanzania hatuna shukrani
 
WanaJF,

Katika hali ambayo ilikuwa inatarajiwa na wengi ni kwamba Mgombea Ubunge wa Jimbo la Hai kupitia tiketi ya CHADEMA ambae pia ni Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa amegaragazwa vibaya sana kwa kuambulia kura 27,000 tu wakati mshindani wake Mgombea wa jimbo hilo kwa tiketi ya CCM amefanikiwa kujizolea kura zaidi ya 80,000.

View attachment 1615231
View attachment 1615230
Mgombea Ubunge kupitia CCM Saashisha Mafuwe, ameibuka mshindi katika Jimbo la Hai kwa kupata kura 89,786 huku mpinzani wake Freeman Mbowe wa CHADEMA akipata kura 27,684.

Hivyo ametangazwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Hai.


Kitendo cha Mbowe kukataliwa vibaya na wanaHai kwenye uchaguzi huru na haki kunatoa somo kwa wana CHADEMA na Watanzania kwa ujumla kuwa picha halisi ni kwamba Mbowe amechokwa na ushindi wake ndani ya chaguzi mbalimbali ndani ya CHADEMA unawezekana kwa sababu ya magumashi tu na sio vinginevyo.

Maamuzi ya wanaHai yamefanya Watanzania tuelewe kiundani kuwa bwana Mbowe bila shaka yoyote amekuwa akilazimisha kuendelea kuongoza CHADEMA na usanii wake wa kujifanya anakubalika umekuwa EXPOSED!

Kwa heshima kubwa nitumie nafasi hii kuwapongeza wana Hai kwa maamuzi sahihi na pia kuwapongeza CCM kwa kuukata mkorosho jimboni hai kwa kutumia Topaz tu.

Pole sana Bwana Mbowe.
Wazee wa kimila walishasema kitambo kuwa huyu Mbowe hawatamchagua tena na hata yeye mwenyewe Mbowe alikuwa anajuwa hilo. Aachane na siasa sasa, watanzania hawataki chama cha kihuni kisicho na msimamo zaidi ya kutaka watanzania kuwa mashoga kama baadhi ya viongozi wao.
 
Dah tumekwisha aisee
Wazee wa escrow wa uamsho na wengine wasio na chapa wanaosubiria ushahidi kukamilika,waandike tu wosia maana kutoka jela ni majaliwa.
Tumekwiishaa,ni mwendo wa kushughulikiwa wapinzani,wanaharakati,wakosoaji.
 
Wazee wa kimila walishasema kitambo kuwa huyu Mbowe hawatamchagua tena na hata yeye mwenyewe Mbowe alikuwa anajuwa hilo. Aachane na siasa sasa, watanzania hawataki chama cha kihuni kisicho na msimamo zaidi ya kutaka watanzania kuwa mashoga kama baadhi ya viongozi wao.
But dikteta hana rafiki watulie tu zamu yao ya kulia ikifika
 
But dikteta hana rafiki watulie tu zamu yao ya kulia ikifika
Of course dikteta Mbowe hana rafiki na ndiyo maana wachagga wenzake walimkataa kitambo. Sasa kwa hasira ndiyo ataibomoa Chadema kwa kuiba mali za chama zaidi.
 
Kwa mwenye wasifu wa kijana huyu machachari aliyeweza kupambana na figisu za ndani ya chama cha mapinduzi na hatimaye kuja kumtoa Freeman Mbowe(mkongwe).
Kijana huyu ameweza kufurukuta dhidi ya kina jerry Muro,Mallya na wanaccm wengine wakiwemo madaktari.

Mwenye CV Yake aitupie humu tumtambue.
 
Tulipowaambia mtakuja na maneno mapya hamkuamini,,tuliwaambia nyomi sio la wapiga kura hamkuamini,tuliwaambia ni mchaga akishika jani la Msale ni kuomba msamaha hamkuamini,ss leo mnakuja na maneno mapya mmenywea kama kakimba cha mwisho,wote chali,mmelegea kama mlenda,na subirini tena matokeo mengine yenye maumivu zaid ya hayo
Kama unagongeka hivi
 
Mwaka 2025 Wapinzani msiingie kamwe kwenye uchaguzi kama muundo wa NEC na baadhi ya vifungu vya KATIBA havitabadilishwa. Mtaendelea kupigwa tu

NEC na ZEC hawatowapa Nchi Wapinzani kamwe. Lissu ajiandae tu “kushindwa” vibaya mno
 
Ujinga mtupu, eti uchaguzi huru na haki!. umejaribu kutengeneza mazingira ili Mbowe aonekane hafai.

Kumbe mmeshinda kwa kujaza kura feki kila kona, Mbowe ni mwamba kawasumbua hamna hamu nae mpaka mmesaidiwa na tume.

Wametangaza matokeo haraka haraka usiku mnene kuogopa reaction ya wapiga kura, then asubuhi mapema defender zitaanza kuzunguka jimbo zima la Hai kuwatisha wapiga kura.

Ndio maana Ndugai alikuwa anachekelea bungeni wapinzani hawatarudi, kumbe huu mpango wa kujaza kura feki ndio ulikuwa kwenye vichwa vyao.

Mngeweza kumtoa hata roho, bora mmemuachia roho yake.
" Mngeweza Kumtoa hata roho, bora mmemuachia roho yake " - DenooJ 2020.
 
Yes, wametengeneza pengo la kura feki karibia elfu sitini ili kudanganya watu kashindwa kihalali!
Inawezekana, lakini pia lazima kuwepo ushahidi.

Mfano ni jimbo la Moshi mjini ambako waliojiandikisha ni 130,000 plus, lakini waliopiga kura ni 54,000 plus. Zaidi ya wapiga kura 70,000 hawakupiga kura.

Nilitegemea kama kuna kura feki basi kura zilizopigwa zingekuwa 100,000 plus.

Bado kuna maeneo mengi watu hawakujitokeza kwa wingi kupiga kura, ikiwemo Mbeya mjini
 
Back
Top Bottom