Mbowe audhibiti mdomo wa Tundu Lissu

Mbowe audhibiti mdomo wa Tundu Lissu

Ndugu zangu Watanzania,

Namshauri Mheshimiwa Mbowe achukue hatua za makusudi za kuudhibiti mdomo wa Lissu, maana kwa sasa umeshapoteza muelekeo na dira. Ndio sababu anaongea chochote kinachotua na kumjia katika mdomo wake. Hana breki wala nati za kuubana. Haelewi ni lipi azungumze na lipi asizungumze. Hana vikao wala makubaliano na akili yake kabla ya kuzungumza kitu.

Kwa sasa, Lissu anaona viongozi wenzake ndani ya chama hawana akili isipokuwa yeye tu. Anajiona yeye ndiye mwenye akili kuliko chama chake chote na wote waliosalia ni mambumbumbu tu. Anamuona Mwenyekiti wake kama mtu asiyejielewa, wala kujitambua, wala akili. Anamuona Mwenyekiti wake na viongozi wenzake kama mahayawani na makasuku tu.

Ndio maana, kwa dharau za kuwadharau viongozi wake wakiongozwa na Mwenyekiti wake, anadharau na kubeza jitihada zote zilizofanywa na Mwenyekiti wake pamoja na viongozi walioshirikiana na Mheshimiwa Mbowe. Anatamka hadharani kwa kiburi, kejeri, na dharau kubwa kuwa yote yaliyofanyika ni ujinga tu. Bila shaka moyoni mwake anamwita Mbowe ni mjinga na jinga. Kwa sasa hamheshimu wala hana cha Mwenyekiti, wala Katibu, wala Kamati Kuu, wala nani. Anajiona ni taasisi ndani ya taasisi, ni chama ndani ya chama. Anajiona ni mkubwa kuliko Mwenyekiti wake pamoja na chama chake. Anajiona anatakiwa kusikilizwa yeye tu na akili zake za kushikiwa na Wazungu. Anajiona ni mwanachama bora kuliko wengine wote, anaona wengine kama madodoki tu ya kunyonya kila kitu.

Ikumbukwe kuwa ni hekima za Mheshimiwa Mbowe kwa kushirikiana na viongozi imara, wazalendo, wakomavu, waungwana, na wenye mapenzi mema na taifa letu kutoka ndani ya CCM walioamua kukaa chini kwa pamoja na kufungua ukurasa mpya wa kisiasa hapa nchini. Ndio hao waliofanikisha Lissu anapata nafasi ya kuropoka majukwaani yote aropokayo na kumdharau Mwenyekiti wake. Ni hao ndio waliofanikisha kuondoa uhasama wa kisiasa. Ni hao waliofanikisha yeye kurejea nchini bila hofu. Ni hao waliofanya tusalimiane na kushirikiana katika shughuli za kijamii bila kujali itikadi zetu za kisiasa. Ni hao waliowezesha haki, amani, na demokrasia kushamiri katika taifa letu na kurejea katika kiti chake cha kikatiba. Na ni hao waliopelekea mpaka sasa kuona mchakato wa katiba mpya kuanza kuwekewa mikakati ya kufufuliwa upya, na ni hao waliorejesha hali ya kuaminiana na kupendana licha ya tofauti zetu za kisiasa.

Sasa Lissu, kwa akili yake inayotokana na kukosa hekima za uongozi na malezi mazuri kutoka utoto wake, anaona siyo kitu. Anaona ni ujinga, ni ushenzi, ni utahira, ni uwendawazimu, na ukasuku.

Watanzania hatupaswi kumsikiliza Lissu wala kumuunga mkono kwa kauli zake za kuwakatisha tamaa viongozi wetu wazalendo walioamua kuweka maslahi ya taifa letu mbele. Hatupaswi kumpa nafasi ya kutimiza ajenda zake.

Ajenda za Lissu ni kutaka kuvuruga maridhiano, ni kutaka kuleta uhasama wa kisiasa, ni kutaka kupandikiza mbegu za chuki na visasi mioyoni mwa Watanzania, ni kutaka siasa za visasi. Ni kutaka kukimbizana mitaani kama wakimbizi ili apate ya kwenda kuropoka huko kwa Wazungu anakopata misaada.

Kwa sasa Lissu hana raha maana anaona amepuuzwa na Watanzania, anaona amenyimwa ajenda ya kuisema vibaya nchi yetu na taifa letu, anaona amekosa hoja za kuishambulia serikali yetu na hivyo kukosa hoja mbele za watu, na ndio maana kila siku anarudia yale yale ambayo kama taifa tulishapita na kuvuka hatua hiyo kwa kushikana mikono na kuchora mistari ya kizalendo na kuamua kusonga mbele kama taifa.

Rai yangu kwa Mheshimiwa Mbowe ni kuwa usikate tamaa wala kukatishwa tamaa na maneno ya Lissu, simama imara na kishujaa, usihofu. Wengi wamekupongeza kwa kukubali kunyoosha mkono wa amani. Lissu ameshapuuzwa na Watanzania, usikubali avuruge maridhiano. Katu na kamwe usimpe nafasi hiyo.

Kazi iendelee. Mama ametufikia na kuwafikia Watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya Watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
Lissu kaongea point kubwa, Hakuna maridhiano na CCM hao ni matapeli.
 
Lissu Ni Mropokaji Sana ,Ni mtu aliyekosa hekima za kiuongozi ,Ni mtu ambaye malezi yake utotoni yanatia mashaka Kama aliyapata vizuri, Hana breki Wala busara azungumzapo mbele ya watu,Ni mkurupukaji Sana,anajiona yeye ndiye mwenye Akili kuliko watanzania wote.
Punguza ujuaji wewe chawa. Una ujasiri gani wa kusema Lissu hana hekima? Punguza Sana ujuaji na unafiki . Hekima unaijua. Lissu kaongea ukweli kwamba tushughulike na katiba mpya haya mambo yakusubiria huruma ya CCM ni ujinga.
 
Kila kitu kina utaratibu wake,chama kina uongozi na masuala yote Yana taratibu zake katika kuyatatua hata Kama huridhiki na hatua fulani,lissu Kama anaona alikuwa na maridhiano waliyofanya wenzake mpaka akaweza kurejea nchini Basi angezungumza kwenye vikao rasmi vya chama chake na siyo kuja kuropoka majukwaani
Peleka taratibu zako CCM.
 
Ujinga wake hauwezi kuvumiliwa,Kama Anataka aondoke chadema akaunde chama chake Cha kwenda kuropoka huko aone Kama Kuna mtu atamfuata huko,Ndio atajuwa maana ya kujenga chama imara maana yeye anafikiri chama kinajengwa kwa kuropoka ropoka tu
Usiifananishe Chadema na CCM ambayo ilimuondoa spika ndugai kisa kauli yake ya madeni ya nje. Baki na ujinga wa CCM na uchawa wako iache chadema Kama ilivyo.
 
Maridhiano yetu tulitaka mikutano ya hadhara ifunguliwe tuanze kuwajambisha CCM tu
Hatutaki Maridhiano tena, tunataka Katiba mpya tu
 
Kwani unataka mpaka uwaambie watu ndo wakujue? Ujinga, unafiki, werevu na uungwana wa mtu uko kwenye maneno ya midomo au kalamu yake..!!

Haiba yako na uandishi wako tu unajieleza mwenyewe unatafuta kitu kwa wenye madaraka ya kiserikali kama cheo au uteuzi wa nafasi fulani na au pesa kabisa. Kwani nani asiyezijua siasa za kiafrika na hususani za kitanzania bro..??

Tabia na mwenendo wako ni kama ya iliyokuwa ya Cyprian Musiba. Lakini yuko wapi sasa?

Yaani huyu bwana (Cyprian Musiba) alikuwa anazushia na kutukana watu hovyo kwa maandishi na mdomo wake kwa kivuli cha "uzalendo wa nchi" au "maslahi ya Taifa" kama unavyodai wewe hapa ili tu kuwafurahisha watawala aidha kwa malipo ya pesa cash au Kwa matarajio ya kupata upendeleo fulani wa uteuzi wa nafasi ya madaraka serikalini...

Hutapata chochote ndugu!!

Utashangaa majira na nyakati za kutafuta ubora wa maisha yako Kwa njia hii yanapita ukiwa mtupu kabisa..

You better use your precious time to do something profitable. Kutaka ule au utoke kimaisha kwa kutumia siasa ni sawa na kufanya betting. Utashangaa unajituma weeeeee kumtetea mwanasiasa fulani, lakini akawa hata hatambui uwepo wako...

Fanya uchangiaji wako ktk mijadala ya kisiasa ukiwa neutral na siyo uelekeo wako huo ulionao..!!
Hapana ndugu yangu ,Mimi sitafuti uteuzi katika kuandika kwangu hapa,Naandika kwa hiyari yangu
 
Maridhiano yetu tulitaka mikutano ya hadhara ifunguliwe tuanze kuwajambisha CCM tu
Hatutaki Maridhiano tena, tunataka Katiba mpya tu
Sasa unafikiri bila maridhiano hiyo mikutano ya hadhara ingetokea wapi? Kwa akili yako unafikiri mngeanza mikutano bila watu wenye akili zao kukaa chini na kuumiza vichwa juu ya mstakabali mwema wa Taifa letu
 
Demokrasia iliyopo ndani ya CCM Ni kubwa Sana na ndio maana CCm inaendelea kuwepo madarakani,kwa kuwa watu wanajisikia amani kuwepo ndani ya CCM

BAWACHA WATAKA KATIBA MPYA, WAPONGEZA POLISI KUWEKA ULINZI MAANDAMANO YA BAWACHA

1683825948273.png

1683826076657.png

1683826178068.png
 
Back
Top Bottom