Mbowe audhibiti mdomo wa Tundu Lissu

Mbowe audhibiti mdomo wa Tundu Lissu

Ndugu zangu Watanzania,

Namshauri Mheshimiwa Mbowe achukue hatua za makusudi za kuudhibiti mdomo wa Lissu, maana kwa sasa umeshapoteza muelekeo na dira. Ndio sababu anaongea chochote kinachotua na kumjia katika mdomo wake. Hana breki wala nati za kuubana. Haelewi ni lipi azungumze na lipi asizungumze. Hana vikao wala makubaliano na akili yake kabla ya kuzungumza kitu.

Kwa sasa, Lissu anaona viongozi wenzake ndani ya chama hawana akili isipokuwa yeye tu. Anajiona yeye ndiye mwenye akili kuliko chama chake chote na wote waliosalia ni mambumbumbu tu. Anamuona Mwenyekiti wake kama mtu asiyejielewa, wala kujitambua, wala akili. Anamuona Mwenyekiti wake na viongozi wenzake kama mahayawani na makasuku tu.

Ndio maana, kwa dharau za kuwadharau viongozi wake wakiongozwa na Mwenyekiti wake, anadharau na kubeza jitihada zote zilizofanywa na Mwenyekiti wake pamoja na viongozi walioshirikiana na Mheshimiwa Mbowe. Anatamka hadharani kwa kiburi, kejeri, na dharau kubwa kuwa yote yaliyofanyika ni ujinga tu. Bila shaka moyoni mwake anamwita Mbowe ni mjinga na jinga. Kwa sasa hamheshimu wala hana cha Mwenyekiti, wala Katibu, wala Kamati Kuu, wala nani. Anajiona ni taasisi ndani ya taasisi, ni chama ndani ya chama. Anajiona ni mkubwa kuliko Mwenyekiti wake pamoja na chama chake. Anajiona anatakiwa kusikilizwa yeye tu na akili zake za kushikiwa na Wazungu. Anajiona ni mwanachama bora kuliko wengine wote, anaona wengine kama madodoki tu ya kunyonya kila kitu.

Ikumbukwe kuwa ni hekima za Mheshimiwa Mbowe kwa kushirikiana na viongozi imara, wazalendo, wakomavu, waungwana, na wenye mapenzi mema na taifa letu kutoka ndani ya CCM walioamua kukaa chini kwa pamoja na kufungua ukurasa mpya wa kisiasa hapa nchini. Ndio hao waliofanikisha Lissu anapata nafasi ya kuropoka majukwaani yote aropokayo na kumdharau Mwenyekiti wake. Ni hao ndio waliofanikisha kuondoa uhasama wa kisiasa. Ni hao waliofanikisha yeye kurejea nchini bila hofu. Ni hao waliofanya tusalimiane na kushirikiana katika shughuli za kijamii bila kujali itikadi zetu za kisiasa. Ni hao waliowezesha haki, amani, na demokrasia kushamiri katika taifa letu na kurejea katika kiti chake cha kikatiba. Na ni hao waliopelekea mpaka sasa kuona mchakato wa katiba mpya kuanza kuwekewa mikakati ya kufufuliwa upya, na ni hao waliorejesha hali ya kuaminiana na kupendana licha ya tofauti zetu za kisiasa.

Sasa Lissu, kwa akili yake inayotokana na kukosa hekima za uongozi na malezi mazuri kutoka utoto wake, anaona siyo kitu. Anaona ni ujinga, ni ushenzi, ni utahira, ni uwendawazimu, na ukasuku.

Watanzania hatupaswi kumsikiliza Lissu wala kumuunga mkono kwa kauli zake za kuwakatisha tamaa viongozi wetu wazalendo walioamua kuweka maslahi ya taifa letu mbele. Hatupaswi kumpa nafasi ya kutimiza ajenda zake.

Ajenda za Lissu ni kutaka kuvuruga maridhiano, ni kutaka kuleta uhasama wa kisiasa, ni kutaka kupandikiza mbegu za chuki na visasi mioyoni mwa Watanzania, ni kutaka siasa za visasi. Ni kutaka kukimbizana mitaani kama wakimbizi ili apate ya kwenda kuropoka huko kwa Wazungu anakopata misaada.

Kwa sasa Lissu hana raha maana anaona amepuuzwa na Watanzania, anaona amenyimwa ajenda ya kuisema vibaya nchi yetu na taifa letu, anaona amekosa hoja za kuishambulia serikali yetu na hivyo kukosa hoja mbele za watu, na ndio maana kila siku anarudia yale yale ambayo kama taifa tulishapita na kuvuka hatua hiyo kwa kushikana mikono na kuchora mistari ya kizalendo na kuamua kusonga mbele kama taifa.

Rai yangu kwa Mheshimiwa Mbowe ni kuwa usikate tamaa wala kukatishwa tamaa na maneno ya Lissu, simama imara na kishujaa, usihofu. Wengi wamekupongeza kwa kukubali kunyoosha mkono wa amani. Lissu ameshapuuzwa na Watanzania, usikubali avuruge maridhiano. Katu na kamwe usimpe nafasi hiyo.

Kazi iendelee. Mama ametufikia na kuwafikia Watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya Watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
Mrs Lucas jaribu muda mwingi kuficha upumbafu wako! Wewe unatoa ushauri kwa Mbowe ambaye ni Mwenyekiti wa Chama! Kwanini ushauri huo usingempa Lisu mwenyewe au ndio hulka yako ya kujiparata kwa Mbowe! Huna adabu!
 
Mrs Lucas jaribu muda mwingi kuficha upumbafu wako! Wewe unatoa ushauri kwa Mbowe ambaye ni Mwenyekiti wa Chama! Kwanini ushauri huo usingempa Lisu mwenyewe au ndio hulka yako ya kujiparata kwa Mbowe! Huna adabu!
Kichwa Cha Tundu lissu Hakishauriki na yeye anahisi ana akili kuliko wote ndio maana mdomo wake umejaa matusi tu na dharau kwa wengine
 
BAWACHA WATAKA KATIBA MPYA, WAPONGEZA POLISI KUWEKA ULINZI MAANDAMANO YA BAWACHA

View attachment 2618228
View attachment 2618229
View attachment 2618230
Wanapoteza muda wao tu na kujifurahisha tu,Kama wangekuwa wanajishauri vizuri ilitakiwa waende mahakamani kujuwa mwenendo wa kesi Yao, lakini pia wajiulize kwanini na vipi wake wa viongozi wao nao wapo Bungeni? Kweli asiyejuwa maana haambiwi maana, Siasa Ni sayansi na hao Bawacha inaoonekana wamevamia siasa tu kilimbukeni ndio maana wanachezeshwa ngoma wasiyoijuwa
 
Hiki kijamaa Mwanshambwa kinajifanya kinajua na mawazo yake ndio sawa tuu, inaonekana baba alikuwa dikteta, hakiamini kabisa kwenye uhuru wa kuongea au mawazo tofauti, yaani ni kusifia tuu na kuwaona wenye mawazo tofauti kama wasaliti, kinatia huruma sana kinahitaji msaada ili kiwe huru
 
Lissu kaongea point kubwa, Hakuna maridhiano na CCM hao ni matapeli.
Mbona miaka yote mlishindwa kufanya hiyo mikutano? Huoni maridhiano ndio yameleta mikutano ya hadhara ambayo lissu leo anatumia majukwaa hayo kutukana na kubeza juhudi za wenye akili,Unafikiri zingekiwa Ni akili za lisu angeweza kukaa katika mess ya mazungumzo na yakafanikiwa?
 
Hiki kijamaa Mwanshambwa kinajifanya kinajua na mawazo yake ndio sawa tuu, inaonekana baba alikuwa dikteta, hakiamini kabisa kwenye uhuru wa kuongea au mawazo tofauti, yaani ni kusifia tuu na kuwaona wenye mawazo tofauti kama wasaliti, kinatia huruma sana kinahitaji msaada ili kiwe huru
Hapana Mimi nachohitaji Ni ujenzi wa hoja zenye mashiko, nikosoe kwa hoja,nipinge kwa ushahidi ,nishambulie kwa hoja zenye mashiko na siyo kupuyanga tu Kama unavyofanya wewe na akili yako. Ukiona hoja zangu zinakuzidi kimo Tuliza kwanza kichwa chako kabla ya kuandika hapa
 
Kwani lini nimekwambia natafuta kitu fulani ambacho unasema nimekosa na sipati, Mimi nipo kwa ajili ya Taifa langu na siyo maslahi yangu Binafsi
Wewe piga brash viatu vya wakuu wako siasa huwezi, hata uchawa huwezi kichwani galoni yako ndogo haijai kikombe cha chai
 
Kwani maana ya neno mjinga ni nini? Mfano halisi ya mtu mjinga ni Lucas
 
Punguza ujuaji wewe chawa. Una ujasiri gani wa kusema Lissu hana hekima? Punguza Sana ujuaji na unafiki . Hekima unaijua. Lissu kaongea ukweli kwamba tushughulike na katiba mpya haya mambo yakusubiria huruma ya CCM ni ujinga.
Unafikiri hiyo katiba ingepatikana kirahisi bila kutanguliza na maridhiano yaliyoleta Hali ya kuaminiana na kuliweka Taifa mbele zidi ya maslahi ya vyama vyetu vya kisiasa
 
Back
Top Bottom