Mbowe audhibiti mdomo wa Tundu Lissu

Mbowe audhibiti mdomo wa Tundu Lissu

Kwani lini nimekwambia natafuta kitu fulani ambacho unasema nimekosa na sipati, Mimi nipo kwa ajili ya Taifa langu na siyo maslahi yangu Binafsi
Maslahi yako binafsi unayataka sana ndg Lucas Mwashimba, ndo maana kwa kila mada unayoiweka hapa jamvini ni lazima uweke namba yako ya simu. Kama ingekuwa ni kwa maslahi ya Taifa usingekuwa unaweka namba ya simu kwenye mada zako.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Namshauri Mheshimiwa Mbowe achukue hatua za makusudi za kuudhibiti mdomo wa Lissu, maana kwa sasa umeshapoteza muelekeo na dira. Ndio sababu anaongea chochote kinachotua na kumjia katika mdomo wake. Hana breki wala nati za kuubana. Haelewi ni lipi azungumze na lipi asizungumze. Hana vikao wala makubaliano na akili yake kabla ya kuzungumza kitu.

Kwa sasa, Lissu anaona viongozi wenzake ndani ya chama hawana akili isipokuwa yeye tu. Anajiona yeye ndiye mwenye akili kuliko chama chake chote na wote waliosalia ni mambumbumbu tu. Anamuona Mwenyekiti wake kama mtu asiyejielewa, wala kujitambua, wala akili. Anamuona Mwenyekiti wake na viongozi wenzake kama mahayawani na makasuku tu.

Ndio maana, kwa dharau za kuwadharau viongozi wake wakiongozwa na Mwenyekiti wake, anadharau na kubeza jitihada zote zilizofanywa na Mwenyekiti wake pamoja na viongozi walioshirikiana na Mheshimiwa Mbowe. Anatamka hadharani kwa kiburi, kejeri, na dharau kubwa kuwa yote yaliyofanyika ni ujinga tu. Bila shaka moyoni mwake anamwita Mbowe ni mjinga na jinga. Kwa sasa hamheshimu wala hana cha Mwenyekiti, wala Katibu, wala Kamati Kuu, wala nani. Anajiona ni taasisi ndani ya taasisi, ni chama ndani ya chama. Anajiona ni mkubwa kuliko Mwenyekiti wake pamoja na chama chake. Anajiona anatakiwa kusikilizwa yeye tu na akili zake za kushikiwa na Wazungu. Anajiona ni mwanachama bora kuliko wengine wote, anaona wengine kama madodoki tu ya kunyonya kila kitu.

Ikumbukwe kuwa ni hekima za Mheshimiwa Mbowe kwa kushirikiana na viongozi imara, wazalendo, wakomavu, waungwana, na wenye mapenzi mema na taifa letu kutoka ndani ya CCM walioamua kukaa chini kwa pamoja na kufungua ukurasa mpya wa kisiasa hapa nchini. Ndio hao waliofanikisha Lissu anapata nafasi ya kuropoka majukwaani yote aropokayo na kumdharau Mwenyekiti wake. Ni hao ndio waliofanikisha kuondoa uhasama wa kisiasa. Ni hao waliofanikisha yeye kurejea nchini bila hofu. Ni hao waliofanya tusalimiane na kushirikiana katika shughuli za kijamii bila kujali itikadi zetu za kisiasa. Ni hao waliowezesha haki, amani, na demokrasia kushamiri katika taifa letu na kurejea katika kiti chake cha kikatiba. Na ni hao waliopelekea mpaka sasa kuona mchakato wa katiba mpya kuanza kuwekewa mikakati ya kufufuliwa upya, na ni hao waliorejesha hali ya kuaminiana na kupendana licha ya tofauti zetu za kisiasa.

Sasa Lissu, kwa akili yake inayotokana na kukosa hekima za uongozi na malezi mazuri kutoka utoto wake, anaona siyo kitu. Anaona ni ujinga, ni ushenzi, ni utahira, ni uwendawazimu, na ukasuku.

Watanzania hatupaswi kumsikiliza Lissu wala kumuunga mkono kwa kauli zake za kuwakatisha tamaa viongozi wetu wazalendo walioamua kuweka maslahi ya taifa letu mbele. Hatupaswi kumpa nafasi ya kutimiza ajenda zake.

Ajenda za Lissu ni kutaka kuvuruga maridhiano, ni kutaka kuleta uhasama wa kisiasa, ni kutaka kupandikiza mbegu za chuki na visasi mioyoni mwa Watanzania, ni kutaka siasa za visasi. Ni kutaka kukimbizana mitaani kama wakimbizi ili apate ya kwenda kuropoka huko kwa Wazungu anakopata misaada.

Kwa sasa Lissu hana raha maana anaona amepuuzwa na Watanzania, anaona amenyimwa ajenda ya kuisema vibaya nchi yetu na taifa letu, anaona amekosa hoja za kuishambulia serikali yetu na hivyo kukosa hoja mbele za watu, na ndio maana kila siku anarudia yale yale ambayo kama taifa tulishapita na kuvuka hatua hiyo kwa kushikana mikono na kuchora mistari ya kizalendo na kuamua kusonga mbele kama taifa.

Rai yangu kwa Mheshimiwa Mbowe ni kuwa usikate tamaa wala kukatishwa tamaa na maneno ya Lissu, simama imara na kishujaa, usihofu. Wengi wamekupongeza kwa kukubali kunyoosha mkono wa amani. Lissu ameshapuuzwa na Watanzania, usikubali avuruge maridhiano. Katu na kamwe usimpe nafasi hiyo.

Kazi iendelee. Mama ametufikia na kuwafikia Watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya Watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
Hichi ndicho mlichojadili kwenye kikao chenu mlichofanya au ni maoni yako binafsi mkuu ?
 
Nawafahamu wote hao

Walimu olevo
1) tobby ,mwl lakini ni polisi na kwasasa mkuu washule ya wazazi pale chimala
2) mwabugusi
3) mwashamba (kaka)
Hawa walikuwa ofisi ya nidhamu

Walimu Aleval
Albert ,mwl geog 1

Kisenene ,geog 1 na genera study
Yasini geog 2

Madam masail eng 1

Mwangosi ,kiswahili ,nakwasasa mkufunzi chuo kikuu RUCU iringa

Wote hao na walimu wengine shule zawazazi mbeya ,wannifahamu

Nilikufatilia Sana hojazako nikaona hapana wewe lazima unaundugu na mwashamba na wewe niyule mdogo wake....kwahiyo punguza mbwembwe mkuu,ccm inawenyewe
Najuwa hunifahamu Bali unafanya kazi ya kubuni buni tu, lakini pia napenda kukwambia ya kuwa Wana CCM ndio wenye chama,Hakuna aliye na hati miliki ndani ya CCM yetu, hakuna aliye mkubwa ndani ya CCM ,sote tuna haki sawa na nafaso sawa,sote tunaheshimiana na kuheshimu mchango wa kila mtu, ndioa maana ukitaja CCM unataja chama wakati vyama vya upinzani ukitaja chama unataja kwanza mtu,maana huko mtu ndio chama na chama ndio yeye.

Ndio maana ndani ya CCM mtu yeyote anaweza kugombea uongozi au kupewa uongozi bila kujali Hali ya kipato Cha familia aliyotokea ,kinachoangaliwa ndani ya CCM ni sifa na uwezo wa mtu kiuongozi katika kuweza kumudu majukumu ya nafasi fulani, uadilifu,uzalendo wa mtu kwa chama na Taifa. Hakuna ubaguzi Wala kubaguliwa au kubaguana ndani ya CCM ,Hakuna habari za wale au sisi ndani ya CCM , sisi sote Ni ndugu ndani ya CCM na tuna nafasi na sauti sawa.

Tunawaheshimu viongozi wetu na kutoa ushauri kwa kufuata utaratibu rasmi wa kichama , siyo mikurupuko Kama wafanyavyo akina lissu na watu wa Aina yake ndani ya chama chake
 
Maslahi yako binafsi unayataka sana ndg Lucas Mwashimba, ndo maana kwa kila mada unayoiweka hapa jamvini ni lazima uweke namba yako ya simu. Kama ingekuwa ni kwa maslahi ya Taifa usingekuwa unaweka namba ya simu kwenye mada zako.
Hapana mkuu Mimi sitafuti maslahi yangu Binafsi,Napigania maslahi ya Taifa langu,Nahitaji kuona Taifa letu likiwa lenye amani , utulivu na upendo. Napenda kuona Hali ya mshikamano miongoni mwetu watanzania ikishamiri na kunawili
 
Nyie visonoko wa lumumba hii staili huku Chadema tunaiita twanga kotekote,mtatuelewa tu.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Namshauri Mheshimiwa Mbowe achukue hatua za makusudi za kuudhibiti mdomo wa Lissu, maana kwa sasa umeshapoteza muelekeo na dira. Ndio sababu anaongea chochote kinachotua na kumjia katika mdomo wake. Hana breki wala nati za kuubana. Haelewi ni lipi azungumze na lipi asizungumze. Hana vikao wala makubaliano na akili yake kabla ya kuzungumza kitu.

Kwa sasa, Lissu anaona viongozi wenzake ndani ya chama hawana akili isipokuwa yeye tu. Anajiona yeye ndiye mwenye akili kuliko chama chake chote na wote waliosalia ni mambumbumbu tu. Anamuona Mwenyekiti wake kama mtu asiyejielewa, wala kujitambua, wala akili. Anamuona Mwenyekiti wake na viongozi wenzake kama mahayawani na makasuku tu.

Ndio maana, kwa dharau za kuwadharau viongozi wake wakiongozwa na Mwenyekiti wake, anadharau na kubeza jitihada zote zilizofanywa na Mwenyekiti wake pamoja na viongozi walioshirikiana na Mheshimiwa Mbowe. Anatamka hadharani kwa kiburi, kejeri, na dharau kubwa kuwa yote yaliyofanyika ni ujinga tu. Bila shaka moyoni mwake anamwita Mbowe ni mjinga na jinga. Kwa sasa hamheshimu wala hana cha Mwenyekiti, wala Katibu, wala Kamati Kuu, wala nani. Anajiona ni taasisi ndani ya taasisi, ni chama ndani ya chama. Anajiona ni mkubwa kuliko Mwenyekiti wake pamoja na chama chake. Anajiona anatakiwa kusikilizwa yeye tu na akili zake za kushikiwa na Wazungu. Anajiona ni mwanachama bora kuliko wengine wote, anaona wengine kama madodoki tu ya kunyonya kila kitu.

Ikumbukwe kuwa ni hekima za Mheshimiwa Mbowe kwa kushirikiana na viongozi imara, wazalendo, wakomavu, waungwana, na wenye mapenzi mema na taifa letu kutoka ndani ya CCM walioamua kukaa chini kwa pamoja na kufungua ukurasa mpya wa kisiasa hapa nchini. Ndio hao waliofanikisha Lissu anapata nafasi ya kuropoka majukwaani yote aropokayo na kumdharau Mwenyekiti wake. Ni hao ndio waliofanikisha kuondoa uhasama wa kisiasa. Ni hao waliofanikisha yeye kurejea nchini bila hofu. Ni hao waliofanya tusalimiane na kushirikiana katika shughuli za kijamii bila kujali itikadi zetu za kisiasa. Ni hao waliowezesha haki, amani, na demokrasia kushamiri katika taifa letu na kurejea katika kiti chake cha kikatiba. Na ni hao waliopelekea mpaka sasa kuona mchakato wa katiba mpya kuanza kuwekewa mikakati ya kufufuliwa upya, na ni hao waliorejesha hali ya kuaminiana na kupendana licha ya tofauti zetu za kisiasa.

Sasa Lissu, kwa akili yake inayotokana na kukosa hekima za uongozi na malezi mazuri kutoka utoto wake, anaona siyo kitu. Anaona ni ujinga, ni ushenzi, ni utahira, ni uwendawazimu, na ukasuku.

Watanzania hatupaswi kumsikiliza Lissu wala kumuunga mkono kwa kauli zake za kuwakatisha tamaa viongozi wetu wazalendo walioamua kuweka maslahi ya taifa letu mbele. Hatupaswi kumpa nafasi ya kutimiza ajenda zake.

Ajenda za Lissu ni kutaka kuvuruga maridhiano, ni kutaka kuleta uhasama wa kisiasa, ni kutaka kupandikiza mbegu za chuki na visasi mioyoni mwa Watanzania, ni kutaka siasa za visasi. Ni kutaka kukimbizana mitaani kama wakimbizi ili apate ya kwenda kuropoka huko kwa Wazungu anakopata misaada.

Kwa sasa Lissu hana raha maana anaona amepuuzwa na Watanzania, anaona amenyimwa ajenda ya kuisema vibaya nchi yetu na taifa letu, anaona amekosa hoja za kuishambulia serikali yetu na hivyo kukosa hoja mbele za watu, na ndio maana kila siku anarudia yale yale ambayo kama taifa tulishapita na kuvuka hatua hiyo kwa kushikana mikono na kuchora mistari ya kizalendo na kuamua kusonga mbele kama taifa.

Rai yangu kwa Mheshimiwa Mbowe ni kuwa usikate tamaa wala kukatishwa tamaa na maneno ya Lissu, simama imara na kishujaa, usihofu. Wengi wamekupongeza kwa kukubali kunyoosha mkono wa amani. Lissu ameshapuuzwa na Watanzania, usikubali avuruge maridhiano. Katu na kamwe usimpe nafasi hiyo.

Kazi iendelee. Mama ametufikia na kuwafikia Watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya Watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.

Mnapenda sana kuanika namba zenu mitandaoni, hamuogopi kutekwa na kufanyiwa chochote kibaya!!

Bhujiku ng'waka bhabhaa
 
Nyie visonoko wa lumumba hii staili huku Chadema tunaiita twanga kotekote,mtatuelewa tu.
Wewe na lissu hamna tofauti yoyote Ile maana wote Ni waropokaji tu ,Bora hata Erythrocyte anajitahidi kidogo kujizuia mihemuko na kuandika vitu kwa hekima na busara bila kumshambulia mtu
 
Lissu yupo Sahihi kabisa Mtu yeyote ambaye anategemea mabadiliko kutoka kwa kiongozi ambaye anatokana na CCM basi mtu huyo ndio mwenye MATATIZO.Hamidu Rubawa
20230118_144819.jpg
 
Hapana mkuu Mimi sitafuti maslahi yangu Binafsi,Napigania maslahi ya Taifa langu,Nahitaji kuona Taifa letu likiwa lenye amani , utulivu na upendo. Napenda kuona Hali ya mshikamano miongoni mwetu watanzania ikishamiri na kunawili
Kama lengo lako ndo hilo, basi usiwe unaweka namba ya simu. Ni ushauri tu, hii dunia ni duara, leo uliye muanzishia uzi kuwa ni mropokaji, kesho unaweza kuta ndo kashika mpini
 
Katu na kamwe Tundu lissu hawezi kuwa Rais wa Taifa letu
 
Najuwa hunifahamu Bali unafanya kazi ya kubuni buni tu, lakini pia napenda kukwambia ya kuwa Wana CCM ndio wenye chama,Hakuna aliye na hati miliki ndani ya CCM yetu, hakuna aliye mkubwa ndani ya CCM ,sote tuna haki sawa na nafaso sawa,sote tunaheshimiana na kuheshimu mchango wa kila mtu, ndioa maana ukitaja CCM unataja chama wakati vyama vya upinzani ukitaja chama unataja kwanza mtu,maana huko mtu ndio chama na chama ndio yeye.

Ndio maana ndani ya CCM mtu yeyote anaweza kugombea uongozi au kupewa uongozi bila kujali Hali ya kipato Cha familia aliyotokea ,kinachoangaliwa ndani ya CCM ni sifa na uwezo wa mtu kiuongozi katika kuweza kumudu majukumu ya nafasi fulani, uadilifu,uzalendo wa mtu kwa chama na Taifa. Hakuna ubaguzi Wala kubaguliwa au kubaguana ndani ya CCM ,Hakuna habari za wale au sisi ndani ya CCM , sisi sote Ni ndugu ndani ya CCM na tuna nafasi na sauti sawa.

Tunawaheshimu viongozi wetu na kutoa ushauri kwa kufuata utaratibu rasmi wa kichama , siyo mikurupuko Kama wafanyavyo akina lissu na watu wa Aina yake ndani ya chama chake
Imeisha hiyo
 
Kama hajavunja sheria acha aropoke. Kwa nini mudhibiti mtu. Mdhibiti kwa hoja mbadala.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Namshauri Mheshimiwa Mbowe achukue hatua za makusudi za kuudhibiti mdomo wa Lissu, maana kwa sasa umeshapoteza muelekeo na dira. Ndio sababu anaongea chochote kinachotua na kumjia katika mdomo wake. Hana breki wala nati za kuubana. Haelewi ni lipi azungumze na lipi asizungumze. Hana vikao wala makubaliano na akili yake kabla ya kuzungumza kitu.

Kwa sasa, Lissu anaona viongozi wenzake ndani ya chama hawana akili isipokuwa yeye tu. Anajiona yeye ndiye mwenye akili kuliko chama chake chote na wote waliosalia ni mambumbumbu tu. Anamuona Mwenyekiti wake kama mtu asiyejielewa, wala kujitambua, wala akili. Anamuona Mwenyekiti wake na viongozi wenzake kama mahayawani na makasuku tu.

Ndio maana, kwa dharau za kuwadharau viongozi wake wakiongozwa na Mwenyekiti wake, anadharau na kubeza jitihada zote zilizofanywa na Mwenyekiti wake pamoja na viongozi walioshirikiana na Mheshimiwa Mbowe. Anatamka hadharani kwa kiburi, kejeri, na dharau kubwa kuwa yote yaliyofanyika ni ujinga tu. Bila shaka moyoni mwake anamwita Mbowe ni mjinga na jinga. Kwa sasa hamheshimu wala hana cha Mwenyekiti, wala Katibu, wala Kamati Kuu, wala nani. Anajiona ni taasisi ndani ya taasisi, ni chama ndani ya chama. Anajiona ni mkubwa kuliko Mwenyekiti wake pamoja na chama chake. Anajiona anatakiwa kusikilizwa yeye tu na akili zake za kushikiwa na Wazungu. Anajiona ni mwanachama bora kuliko wengine wote, anaona wengine kama madodoki tu ya kunyonya kila kitu.

Ikumbukwe kuwa ni hekima za Mheshimiwa Mbowe kwa kushirikiana na viongozi imara, wazalendo, wakomavu, waungwana, na wenye mapenzi mema na taifa letu kutoka ndani ya CCM walioamua kukaa chini kwa pamoja na kufungua ukurasa mpya wa kisiasa hapa nchini. Ndio hao waliofanikisha Lissu anapata nafasi ya kuropoka majukwaani yote aropokayo na kumdharau Mwenyekiti wake. Ni hao ndio waliofanikisha kuondoa uhasama wa kisiasa. Ni hao waliofanikisha yeye kurejea nchini bila hofu. Ni hao waliofanya tusalimiane na kushirikiana katika shughuli za kijamii bila kujali itikadi zetu za kisiasa. Ni hao waliowezesha haki, amani, na demokrasia kushamiri katika taifa letu na kurejea katika kiti chake cha kikatiba. Na ni hao waliopelekea mpaka sasa kuona mchakato wa katiba mpya kuanza kuwekewa mikakati ya kufufuliwa upya, na ni hao waliorejesha hali ya kuaminiana na kupendana licha ya tofauti zetu za kisiasa.

Sasa Lissu, kwa akili yake inayotokana na kukosa hekima za uongozi na malezi mazuri kutoka utoto wake, anaona siyo kitu. Anaona ni ujinga, ni ushenzi, ni utahira, ni uwendawazimu, na ukasuku.

Watanzania hatupaswi kumsikiliza Lissu wala kumuunga mkono kwa kauli zake za kuwakatisha tamaa viongozi wetu wazalendo walioamua kuweka maslahi ya taifa letu mbele. Hatupaswi kumpa nafasi ya kutimiza ajenda zake.

Ajenda za Lissu ni kutaka kuvuruga maridhiano, ni kutaka kuleta uhasama wa kisiasa, ni kutaka kupandikiza mbegu za chuki na visasi mioyoni mwa Watanzania, ni kutaka siasa za visasi. Ni kutaka kukimbizana mitaani kama wakimbizi ili apate ya kwenda kuropoka huko kwa Wazungu anakopata misaada.

Kwa sasa Lissu hana raha maana anaona amepuuzwa na Watanzania, anaona amenyimwa ajenda ya kuisema vibaya nchi yetu na taifa letu, anaona amekosa hoja za kuishambulia serikali yetu na hivyo kukosa hoja mbele za watu, na ndio maana kila siku anarudia yale yale ambayo kama taifa tulishapita na kuvuka hatua hiyo kwa kushikana mikono na kuchora mistari ya kizalendo na kuamua kusonga mbele kama taifa.

Rai yangu kwa Mheshimiwa Mbowe ni kuwa usikate tamaa wala kukatishwa tamaa na maneno ya Lissu, simama imara na kishujaa, usihofu. Wengi wamekupongeza kwa kukubali kunyoosha mkono wa amani. Lissu ameshapuuzwa na Watanzania, usikubali avuruge maridhiano. Katu na kamwe usimpe nafasi hiyo.

Kazi iendelee. Mama ametufikia na kuwafikia Watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya Watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
Hakuna anachokisema Lissu ambacho Chadema inakipinga

Sent from my SM-J500H using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom