Mbowe: Bunge likipitisha Mkataba wa DP World, tutaamsha Nchi nzima

Mbowe: Bunge likipitisha Mkataba wa DP World, tutaamsha Nchi nzima

Ukombozi wanini wakati IQ yenyewe hafifu.
Bora maisha ya amani,upendo,mshikamano hata kama IQ yenyewe ni hafifu IQ ya Sudan,Iraq,Syria,Urusi,Somalia ya kupigana mabomu na kukatana mapanga hiyo haina faida.Babu zetu waliishi katika mapango lakini waliishi kwa upendo,mshikamano,udugu na amani,hawakuwa na njaa,njaa yao ilikuwa pesa lakini vingine walipambana kwa akili yao na wakatulea bila shida.Sasa hivi tuna Serikali,Bunge na Mahakama.Sasa hivi tuna Wafanyabiashara wakubwa wa Kitanzania,una wasomi wazuri wa Kitanzania,tuna viongozi wa Kitanzania,tuna hospitali za Watanzania,tuna shule za Watanzania,tuna barabara za lami karibia Tanzania yote,hiyo IQ yako ina faida gani zaidi ya kuhamasisha biashara ya Utumwa Tanzania.
 
Daah mkuu mbona umenivamia kwani mimi nilienda Dubai na wakina Msukuma au unataka nichambue nini ili uelewe...sihitaji kujisifia akili wakati Taifa linatapeliwa na wenye akili wapo Kimya tuu...

Kwa mantiki hio hauujui mkataba ila maneno ya mbowe yamekufanya uone tumepigwa
 
Wengi niliokutana nao hata hawaujui mkataba ila wanavoupinga na kulalamika [emoji23][emoji23]
 
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe ameitaka Serikali kuondoa Mkataba huo kwenye majadiliano Bungeni kwasababu unakwenda kuiingiza Nchi kwenye migogoro usio na faida.

Pia, amewataka Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Bandari, Plasduce Mikeli Mbossa kujitafakari kama wana hadi ya kuendelea kubaki kwenye ofisi za Umma kutokana na kuiingiza Nchi kwenye Mkataba huo.

Aidha, amesema ifike wakati sasa badala ya kutoa Kinga kwa Viongozi, wengine waanze kushtakiwa kwa makosa wanayofanya kwa kutumia Mamlaka yao vibaya na kuiingiza Nchi katika mikataba ya ovyo.
Ataamshaje
 
Biashara lazima iwe na faida kwa pande zote mbili.tuache kuona kila kitu ni kupigwaa tuh.mkataba uchambuliwe kwenye sehem tukiona hapafai tuombe pabadilishwe,sio kuleta ngojera za kusingizia kupigwa kupigwa [emoji53]
 
Tubadilishe mindset zetu.
Mindset za kuuza utu wetu na rasilamali zetu tulikataa tangu 09.12.1961 na hata hali ya utumwa ilipotaka kurudi 2016 hadi 2021 tulikataa tena tarehe 17.03.2021 kwa sala na maombi ya Watanzania na Mungu akatujibu.
 
Miungu yenyewe tunayoiabudu ni ya watu wa Sham sala gani itakayopokelewa.
 
Biashara lazima iwe na faida kwa pande zote mbili.tuache kuona kila kitu ni kupigwaa tuh.mkataba uchambuliwe kwenye sehem tukiona hapafai tuombe pabadilishwe,sio kuleta ngojera za kusingizia kupigwa kupigwa [emoji53]
Mkataba ulishasainiwa kitambo unataka uchambuwe nini yaani wewe upikiwe ugali uletewe mezani halafu uanze kutafuta unga na kuni inaingia akilini?
 
Back
Top Bottom