Mbowe: CHADEMA hatutashiriki Uchaguzi Mkuu wa 2025 (bila Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi)

Raha ya mbowe ni kutawala nyumbu kama wewe.

Kwa hiyo aliyewazuia kushiriki uchaguzi mkuu wa 2025 ni mwendazake?
Mkuu, ukiongoza wafuasi wa Mbowe ni raha tupu.
 
Hii mbinu haijawahi kuwasaidia CDM zaidi ya kuipa ahueni CCM na kuendelea kuiparasite TZ, Let him think big!!!
 
Sasa isiposhiriki uchaguzi wa kidemokrasia inategemea kufanya mapinduzi ya kibabe? ifike wakati CHADEMA muache hizi siasa maji taka fanyeni sisa zenye dira kwa maslahi mapana ya taifa. mmeshindwa kumpelekea spika uthibitisho wa vikao vilivyowafukuza Covid 19 wananchi tunawaangalia tu mnavyocheza na akili zetu tunaomba mjibu swali kwanza la rufaa za wale Covid 19 ndio tuwasikilize kwa haya mengine. kusudi la kusema hayo ni kuonyesha kuwa tunahangaika na adui wa nje wakati tunamwacha adui tuliekaa naye mezani shida ya CHADEMA inaanzia ndani ya chama najua katika hili watanielewa wachache kwa sasa lakini wengi watanielewa baadae
 
Mbona bado mapema sana kuanza kulalamika wazee kama hamtashiriki uchaguzi wa 2025 si basi sasa mnataka tufanyeje
 
Nenda kamuulize Ndugai kwanini anawang'ang'ania wabunge wa COVID 19 pale bungeni wakati CHADEMA haiwatambui?

Akikupa jibu ndio utaelewa kwanini CHADEMA ni nguvu ya umma wa watanzania.
Mbowe amewasamehe hao unaowaita covid 19 na amewaomba warudi kujenga chama
 
kaka kuna magezeti sasa hivi ? Tanzanite na Habari leo wapo ni kusifu na kuabudu tu.
Tanzania daima liko wapi? Kazi yao ni kupinga kila kitu
 
Kuna haja gani ya kushiriki kama unajua hutatendewa haki? ni bora hizo pesa wakazitumia kuwaelimisha watu ili wajue haki na wajibu wao wa kuchagua viongozi, kujiletea maendeleo na Serikali kuwajibika kwa wananchi
 
Tanzania daima liko wapi? Kazi yao ni kupinga kila kitu
dawa huwa si kufunga watu midomo, dawa ni kutekeleza kinachotakiwa ili wananchi wakose cha kusema !! kufungia watu kongoea ni kuficha uozo ambao leo tunaushuhdia wote kwa macho.
 

Mataga kazi mnayo!

Katiba mpya/tume huru ndiyo kipaumbele cha waungwana wote ndani na nje ya CCM. Hakuna katiba

Kwa wasio waungwana wala hainyimi kunywa maji.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Katiba Mpya na Tume Huru ya uchaguzi lazima vipatikane, kushiriki uchaguzi wakati tume kila mara inaipendelea CCM na wagombea wake ni ujinga, itafutwe njia yoyote mbadala ya kuidai Katiba Mpya.
Watanzania wote kwenye akili timamu tusimame na kupaza sauti zetu kudai Katiba Mpya ya Wananchi kwa ajili ya Wananchi bila kujali kuwa CCM na serikali yake wanapenda na kukubali ama la.Hilo ndilo jukumu tunalotakiwa kulitekeleza before it's too late.Tutumie fursa ya kuondoka yule aliyesema Katiba siyo kipaumbele chake.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Mbowe ana wahadaa wafuasi wake wasiojielewa
Kudai Katiba siyo agenda ya Mh.Mbowe wala CHADEMA pekee Bali ya Watanzania wengi kwa faida yetu sote.
Mnaotetea Katiba iliyopo mna maslahi gani nayo kiasi cha kuhamasisha Wananchi kuwa isipatikane Mpya?
Katiba za nchi zinatakiwa ziendane na mahitaji ya wakati husika,inakuwaje Watanzania wa leo wanaong'ang'ania Katiba iliyoandikwa miaka zaidi ya 40 ilyopita tena wakati ule chini ya chama kimoja na watu wachache walioelimika kulikoni sasa?Mazingira na mahitaji ya nchi hii ya mwaka 1977 ni sawa na 2021? Tujiulize,kwa nini CCM wanaogopa Katiba hii kubadilishwa?Je,katiba za nchi ni kwa faida ya vyama vilivyopo madarakani?
Wenye nchi wanapohitaji kujitengenezea utaratibu bora wa kuiongoza nchi yao ni nani mwenye Haki ya kuwazuia?
 
Kenya kila siku wanabadilisha katiba utafikiri wananchi wanashiba katiba
 
Watanzania wengi Wala hawaitaji katiba. Huu ni ukweli, katiba inahitajiwa Sana na wanasiasa
 
dawa huwa si kufunga watu midomo, dawa ni kutekeleza kinachotakiwa ili wananchi wakose cha kusema !! kufungia watu kongoea ni kuficha uozo ambao leo tunaushuhdia wote kwa macho.
Kama kupinga kila kitu ni sawa kwa nini kusifia kila kitu iwe nongwa?
 


Umenena ukweli mtupu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…