Kinuju
JF-Expert Member
- Mar 20, 2021
- 2,386
- 5,325
Mwenyekiti wa kudumu wa CHADEMA amemuonya Rais Samia kuwa asikubali kuliruhusu bunge lililopo sasa hivi lianze mchakato wa katiba mpya.
Mbowe amesema Rais akiruhusu hilo wao kama chama cha upinzani nchini hawatakubali kamwe.
"Kwanza tuna amani mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa ni haki ya kikatiba kisheria na ni wajibu wetu, ombi la mama Samia kwamba tusubiri, tumpe muda hatuko tayari kumpa muda."Freeman Mbowe
====
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, amemwomba Rais Samia Suluhu Hassan, aunde Tume ya Katiba, itakayoshirikisha makundi yote kwa ajili ya kufufua mchakato wa katiba mpya “na hatutakubali Bunge hili lililopo, litutengenezee katiba mpya.”
Ombi la Mama Samia kwamba tumpe muda hatupo tayari kumpa muda na natoa agizo kwa Viongozi Nchi nzima wajiandae kwa mikutano ya hadhara siku ambayo tutaitangaza.
Tunapendekeza kuwe na Bunge la Katiba na lisiwe Bunge hili linaloendelea sasa wala wasituambie Bunge hili la sasa ndio liunde Katiba, ichukuliwe rasimu ya Warioba na Katiba na kisha iundwe rasimu ya Katiba mpya, sio gharama na tukiamua tutapata Katiba mpya mwaka huu.
Katiba ni mali ya Wananchi na sio mali ya Viongozi, miongoni mwa mambo ambayo Rasimu ya Katiba ya Warioba ilibainisha ni kupunguza majukumu ya Rais,Warioba alipendekeza tuwe na Tume Huru ya Uchaguzi, Tuwe na Mgombea Huru.
Madai ya Katiba tutadai asubuhi, mchana hadi usiku, kama wanataka tukae mezani turidhie kama wasiporidhia tutakutana Barabarani, hatutoridhia kushiriki Uchaguzi wowote bila kuwa na Katiba au Tume ya Uchaguzi