Mbowe: Hatutakubali Bunge lililopo litengeneze Katiba Mpya

Mbowe: Hatutakubali Bunge lililopo litengeneze Katiba Mpya

Unafikiri ndiyo amemaliza zamu yake na hawezi enda tena huko akitaka tena. Hizi ni dalili za kutaka kwenda huko. Nyie mcheeni tu Mama.
Kama atatenda kosa sawa ila kama hakutenda kosa lolote watampeleka kwa uonevu ?

Mungu atatenda kazi yake
 
Tatizo la Chadema siyo wanasiasa ni wanaharakati,hawajui kwamba kwenye siasa Kuna hitaji mchakato,majadiliano ya muda mrefu mpaka mnakubaliana na kwenye muafaka siyo lazima upate yote Kuna kupata na mengine kukosa.Wakiendelea na siasa za aina hii watakosa yote hawatapata katiba mpya Wala tume huru ya uchaguzi.
Unajadiliana vipi na watu ambao hawako tayari kujadiliana.?
 
Hivi ccm wanachoogopea katiba mpya ni nini?
Ikiandikwa katiba mpya nzuri ya kidemokrasia CCM itadhoofika.Nguvu kubwa ya CCM ni kuchangamana na dola na katiba hii iliundwa mahsusi kuipendelea CCM.Kwahiyo hata Chadema kingekuwa chama tawala isingekubali katiba mpya.
 
Mtajaa tu SI mnadhani kila mtu mnyanga akati wapo ma born town
 
Mbowe ni kiongozi mkubwa sana ila anafeli sehemu ndogo sana mara kwa mara

Kiongozi mkuu hatakiwi kutoa kauli kwa kukurupuka

Kwa mfano, anavyosema "...viongozi wa chadema wajiandae kufanya mikutano ya hadhara..." tafsiri yake ni nini?

Viongozi wake ni wakupokea order tu na kutekeleza bila kuwa na majadiliano?

Ikitokea viongozi kadhaa wakaja na hoja yenye mashiko (mfano kuepuka mikusanyiko kwa sababu ya corona) na hivyo kufifisha "agizo" lake haoni Kama inampunguzia credit yeye Kama top leader?

Halafu Mbowe alitakiwa asome upepo, kuja na matamko Kama haya watu wenye kudadisi sana watakuja na conclusion kuwa kumbe na yeye ni muoga Kama waoga wengine maana enzi za Magufuri hakutoa hivi vitisho, kwanini alishindwa wakati katiba inawaruhusu?

Hata hivyo, asome upepo vizuri wa wananchi maana ni "Kama" wanamuelewa elewa Rais huyu hivyo wanaweza kujikuta wanaandamana viongozi wao tu na boda hoda mtaani

..tamko la Rais Samia ni kuvunja KATIBA hivyo siyo busara tamko hilo lipite bila kulaaniwa na viongozi wa vyama vya upinzani, hususan Chadema.

..pia sioni kosa kwa Mbowe kuwaelekeza viongozi wa chama wajiandae kwa mikutano. Rais Samia amesema kuwe na subira, kwa hiyo hakuna ubaya Chadema wafanye maandalizi ili Rais atakapoamua kuruhusu mikutano agizo hilo liwakute wakiwa tayari.

..Mwisho, Mbowe hajavunja sheria yoyote ile ya nchi kwa kuwaelekeza viongozi wake wajiandae kufanya mikutano.
 
Patrick_Ole_Sosopi_on_Instagram:_“#UpdatesKatibaDay%0AHiki_ndicho_kinachoendelea_leo_July_Mosi...jpg
Joseph_O._Mbilinyi_on_Instagram:_“Kongamano_la_KATIBA_mpya_na_bora_DAR_leo...#KatibaMpya_#Tume...jpg


Taarifa zote zitakujia hapahapa
 
Unajadiliana vipi na watu ambao hawako tayari kujadiliana.?
Rais kakataa lini?Rais alisema ataonana na wapinzani,nafikiri Jambo la muhimu ni kumsisitizia/kumkumbusha aonane nao halafu mazungumzo yaanze.
 
Jamaa zangu wa CDM mnaona jamaa yenu alivyo mwehu???

..Raisi amehimiza lugha za staha.

..Sasa ndugu zangu kama mmeamua kumuunga mkono Raisi msiwe mnatumia lugha mbaya dhidi ya viongozi wa vyama vya upinzani.

..Mnapomuunga mkono Raisi kwa upande mmoja, halafu upande mwingine mkawa mnawatukana wapinzani, jamii inaweza ikadhani mmetumwa na Raisi kufanya hivyo.
 
Katiba inadaiwa na walevi? Mkutano umejaa walevi watupu kuanza mwenyekiti hadi wajumbe.
Wazee wa faru John, sipati picha baadae mtavyolewa
Jinga kabisa, kamuandalie chai ya jioni Nikki, ulisema igizo limekwama hakuna wajumbe sasa hivi unasema wajumbe walevi, utakuwa baamedi wewe ukitoroka kuosha vyombo kwa Nikki unakimbilia bar.
 
..Raisi amehimiza lugha za staha.

..Sasa ndugu zangu kama mmeamua kumuunga mkono Raisi msiwe mnatumia lugha mbaya dhidi ya viongozi wa vyama vya upinzani.

..Mnapomuunga Rais mkono kwa upande mmoja, halafu upande mwingine mkawa mnawatukana wapinzani, jamii inaweza ikadhani mmetumwa na Raisi kufanya hivyo.
Mkuu wewe ni miongoni mwa members ambao kwa kweli wakini-quote huwa nawaheshimu sana. Heshima yangu kwako ipo juu sana mkuu.

Unajua kinachopelekea haya mambo yatokee.

Hivi Mheshimiwa Mbowe kama kiongozi mkubwa tu, anaongeaje maneno aliyoyaongea kumjibu Rais wa nchi??? Ndio kweli tukae kimya tu????
 
Mwenyekiti wa kudumu wa CHADEMA amemuonya Rais Samia kuwa asikubali kuliruhusu bunge lililopo sasa hivi lianze mchakato wa katiba mpya.

Mbowe amesema Rais akiruhusu hilo wao kama chama cha upinzani nchini hawatakubali kamwe.

"Kwanza tuna amani mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa ni haki ya kikatiba kisheria na ni wajibu wetu, ombi la mama Samia kwamba tusubiri, tumpe muda hatuko tayari kumpa muda."Freeman Mbowe

====
wenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, amemwomba Rais Samia Suluhu Hassan, aunde Tume ya Katiba, itakayoshirikisha makundi yote kwa ajili ya kufufua mchakato wa katiba mpya “na hatutakubali Bunge hili lililopo, litutengenezee katiba mpya.”

Ombi la Mama Samia kwamba tumpe muda hatupo tayari kumpa muda na natoa agizo kwa Viongozi Nchi nzima wajiandae kwa mikutano ya hadhara siku ambayo tutaitangaza.

Tunapendekeza kuwe na Bunge la Katiba na lisiwe Bunge hili linaloendelea sasa wala wasituambie Bunge hili la sasa ndio liunde Katiba, ichukuliwe rasimu ya Warioba na Katiba na kisha iundwe rasimu ya Katiba mpya, sio gharama na tukiamua tutapata Katiba mpya mwaka huu.

Katiba ni mali ya Wananchi na sio mali ya Viongozi, miongoni mwa mambo ambayo Rasimu ya Katiba ya Warioba ilibainisha ni kupunguza majukumu ya Rais,Warioba alipendekeza tuwe na Tume Huru ya Uchaguzi, Tuwe na Mgombea Huru.


Huu ndiyo ubinadamu yaani "kusemezana."

Mama alitoa yake ya moyoni:


Haya sasa ni yetu ya moyoni.

Bandika bandua pole pole tutafika.
 
Back
Top Bottom