Mbowe: Hatutakubali Bunge lililopo litengeneze Katiba Mpya

Mbowe: Hatutakubali Bunge lililopo litengeneze Katiba Mpya

Moja ya sababu kubwa ya kushindwa kukamilika kwa mchakato wa katiba mpya ni wingi wa wabunge walio kuwemo. Muda mwingi ilitumika kulumbana, kweli mapanya wengi hawachimbi shimo likaenda.
Na kushupaza shingo
 
Yaani Mbowe anamtisha Rais wa nchi? Huyu mama awe makini, kipindi cha JPM hizi kauli kama za Mbowe hakuna aliethubutu kuongea, na Ikitokea umeongea lazima uchakae
Huyo JPM yuko wapi sasa, nyie mponzeni na mama ila mjue kuwa Mungu sio binadamu, kama mama hakujifunza kwa JPM basi atajifunza in hardway kama JPM anavyojifunza in hardway uko aliko.
 
Mbowe ni kiongozi mkubwa sana ila anafeli sehemu ndogo sana mara kwa mara

Kiongozi mkuu hatakiwi kutoa kauli kwa kukurupuka

Kwa mfano, anavyosema "...viongozi wa chadema wajiandae kufanya mikutano ya hadhara..." tafsiri yake ni nini?

Viongozi wake ni wakupokea order tu na kutekeleza bila kuwa na majadiliano?

Ikitokea viongozi kadhaa wakaja na hoja yenye mashiko (mfano kuepuka mikusanyiko kwa sababu ya corona) na hivyo kufifisha "agizo" lake haoni Kama inampunguzia credit yeye Kama top leader?

Halafu Mbowe alitakiwa asome upepo, kuja na matamko Kama haya watu wenye kudadisi sana watakuja na conclusion kuwa kumbe na yeye ni muoga Kama waoga wengine maana enzi za Magufuri hakutoa hivi vitisho, kwanini alishindwa wakati katiba inawaruhusu?

Hata hivyo, asome upepo vizuri wa wananchi maana ni "Kama" wanamuelewa elewa Rais huyu hivyo wanaweza kujikuta wanaandamana viongozi wao tu na boda hoda mtaani
Mtu mwenyewe anaogopa hadi kivuli chake anakimbilia ughaibuni huko, watulie sasa.
 
Haya sasa. Tulisema mama asicheke na nyani atakula mabua. Wanachotaka sasa jeshi la polisi liwape kipigo kwa kuweka mikutano yao kisha waseme wameuliwa kutekwa na kuteswa.

Mbona wanaofanya mihadhara ya kidini hawatekwi, kupigwa nk wakati mikusanyiko yake inafanana ni mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa? Au kwakuwa mikutano ya dini haina madhara na madaraka ya ccm?
 
Huyo JPM yuko wapi sasa, nyie mponzeni na mama ila mjue kuwa Mungu sio binadamu, kama mama hakujifunza kwa JPM basi atajifunza in hardway kama JPM anavyojifunza in hardway uko aliko.
Kwani Baregu, Karugendo wako wapi?
Nao walimpinga mbowe?

Wewe kwa kuwa bendera fuata upepo mbowe ndiyo hutakufa??
 
Mungu naye akawa sahihi zaidi kwa kumuondoa duniani!
Kwani Baregu, Karugendo wako wapi?
Nao walimpinga mbowe?

Wewe kwa kuwa bendera fuata upepo mbowe ndiyo hutakufa??
 
Huyo JPM yuko wapi sasa, nyie mponzeni na mama ila mjue kuwa Mungu sio binadamu, kama mama hakujifunza kwa JPM basi atajifunza in hardway kama JPM anavyojifunza in hardway uko aliko.
Ndesamburo nae yupo wapi? Maana inaonekana unajua sana wafu walipo
 
Mama anajua pia kuwa akizingua anazinguliwa.

Kwanini isiwe tusizinguane?

Maoni na mawazo ya mama si msahafu na hii ni kwa mwingine yeyote.
Hata wwe Mzee wa Corona pia hutaki social distance,unataka Mikutano ya kisiasa kisa Katiba!? Vp hamuogopi Corona tena!?
 
Kwani Baregu, Karugendo wako wapi?
Nao walimpinga mbowe?

Wewe kwa kuwa bendera fuata upepo mbowe ndiyo hutakufa??

Hao uliowataja walikuwa wanajifanya wacha Mungu na wazalendo, huku wakiongozwa na kiburi cha madaraka?
 
Mkuu wewe ni miongoni mwa members ambao kwa kweli wakini-quote huwa nawaheshimu sana. Heshima yangu kwako ipo juu sana mkuu.

Unajua kinachopelekea haya mambo yatokee.

Hivi Mheshimiwa Mbowe kama kiongozi mkubwa tu, anaongeaje maneno aliyoyaongea kumjibu Rais wa nchi??? Ndio kweli tukae kimya tu????

..Na mimi naheshimu sana maoni yako.

..Ningependa sana wanaomuunga mkono Rais Samia wawe na lugha nzuri tofauti na awamu iliyopita.

..Rais ametoa agizo ambalo linakiuka katiba. Pia agizo hilo linakipendelea chama chake na kuvionea vyama vya upinzani.

..Mbowe ameonyesha kutokukubaliana na msimamo wa Raisi. Sijaona mahali alipotumia lugha ya matusi au kumvunjia heshima Raisi.

..Mwisho, ningekuwa mshauri wa Raisi ningemshauri amtume msemaji wake aliweke suala hili vizuri, ili lifuate sheria na katiba.

..Suala kama hili lilitokea wakati wa Rais Magufuli. Lilituletea shida kubwa. Why is president Samia repeating the same mistake.? Kwanini washauri na wapambe wanamshangilia na kumhimiza Rais ktk jambo baya badala ya kumsaidia kurekebisha?
 
Hauwajui vizuri hawa aiseee yaani hawa ni kama watani zangu wakurya bila kula vibao hawaoni kama kuna mapenzi.

..Naomba mjizuie kuhamasisha violence dhidi ya wapinzani.

..Tutajenga utamaduni mbaya wa ukatili ktk siasa zetu.

..MUNGU ametupa nafasi ya kujirekebisha kwani tulifika pabaya. Tusipoteze nafasi hii adhimu.
 
Back
Top Bottom