Moja ya sababu kubwa ya kushindwa kukamilika kwa mchakato wa katiba mpya ni wingi wa wabunge walio kuwemo. Muda mwingi ilitumika kulumbana, kweli mapanya wengi hawachimbi shimo likaenda.
Kwenye nia njema ya uwakilishi sawia, huwezi kutumia bunge la jamhuri kuwa bunge la katiba kwa sababu halina uwiano wowote. Linakuwa ni bunge la siasa lenye kundi moja kubwa lililo na mrengo, itikadi na kauli moja na hivyo ni rahisi sana ku compromise hata masuala ya msingi kitaifa, ili kulinda maslahi ya kundi hilo lililokubwa kwenye bunge.
Bunge la katiba linapashw a kuwa na uwakilishi usio na asili ya ititkadi za kisiasa. Ni chombo kinachopashwa kuundwa na makundi yote muhimu katika taifa vikiwemo vyama vya siasa, vyama vya wafanyakazi, taasisi za umma na zile za binafsi, vyama vya kijamii, makundi mbali mblai ya watu kama wazee, vijana, wakulima, wafugaji, n.k.
Kugeuza bunge la wanasiasa ndilo liwe bunge la katiba, na kutupia tupia watu wengine wachache humo, ni kutaka kuhalalisha maslahi ya chama chenye wabunge wengi kuwa katiba ya nchi, wakati vyama vya siasa vina katiba zake.
Naunga mkono hoja ya Mbowe kwamba bunge la siasa halipashwi kubadilishwa na kuitwa bunge la katiba kwa kuwa tayari lina kundi kubwa la watu aina moja na hivyo kufanya uwiano wa uwaklishi kukosa mashiko kitu ambacho kama hakitakuwepo, basi itakuwa ni katiba inayolind amaslahi ya kundi lenye watu wengi ambacho ni chama cha siasa.