Mbowe: Hatutakubali Bunge lililopo litengeneze Katiba Mpya

Mbowe: Hatutakubali Bunge lililopo litengeneze Katiba Mpya

Kwa kauli hii ya Mbowe mama hana option zaidi ya kuwa dikteta.....
otherwise watampelekesha sana hawa....
mama inaonekana ni mpenda haki na utu
lkn naona wanamforce awe dikteta.....
wanasema hakuna mchawi mbaya kama mwanamke....
Hapa sasa Mbowe ndiye anaye dictate, kwa maana hiyo yeye sasa atakuwa dikteta, tatizo mama kasema subirini katiba mpya itakuja, kama kuna kitu cha kulazimisha kwanza itafutwe tume huru ya uchaguzi, Mutungi na timu yake wakae pembeni, tukishapata wawakilishi halali wa wananchi ndiyo katiba mpya ianze hivyo kwa ushauri wapinzani kaeni na mama mmwambiye ushauri wenu katika kuipeleka nchi katika maendeleo.

Mbowe ukifanya hivyo hutajenga bali utakuwa unabomoa, uchafuzi wa uchaguzi ni vigumu sana kuusafisha unataka akili kubwa na ustahamilivu na ustaarabu na kamwe usicheze na dola, siyo mkamuona ni mama mkaleta hoja za vitisho, huyo ni taasisi na neno lake ni sheria. Chondechonde stahamilini na mfuate utaratbu ikiwa mnataka kuingia kwenye nchi ile ya ahadi.
 
Hili neno amandla unalitumia kizembe sana....
issue ipo hv CCM hawawezi kubali mabadiliko ya katiba.....huo ni uamuzi wa CCM sio mama....
JK mwenyewe analijua hili fika....
siku katiba ikiwekwa sawa fisiemu wanapotea...
usisahau kwamba sheria zinatungwa na watawala....
Inakuuma sana ninavyotumia Amandla?

Iko hivi, Katiba sio prerogative ya Chama Tawala. Mwenyekiti ndio sura ya chama chake kwa hiyo hawezi kujitoa katika maamuzi yeyote yanayofanywa na chama chake. Histori inaonyesha kuwa hakuna chama kinachotawala milele kwa hiyo iko siku CCM hakitakuwa chama tawala. Na kisipokuwa makini basi siku hiyo ikifika ndio kitapotea jumla kama ilivyokuwa kwa KANU, UNIP, na wengine. PRI ya Mexico kilitawala kwa miaka 71 (kuanzia 1929 mpaka 2000) na kilipoondolewa hakijarudi tena. Congress party cha India hivyo hivyo. Sasa hivi kipo kipo tu ingawa ndio chama cha wakina Mahatma Gandhi, Nehru na Indira Gandhi.

Amandla...
 
..Rais Samia naye awe makini asijejikuta anakuwa kiongozi MKATILI jambo ambalo halitegemewi kwa wanawake.
neno MKATILI ni relative sana kwani linaweza kuchanganya kusimaia sheria za nchi (ambazo ni za kimabavu naturally) na kuonea raia (ambalo ndyo watu hatutaki). kwani Golda Meir alipokuwa anawapiga na kuwaua waarabu, au Margareth Thatcher alipokuwa akiwabana Labour party kisiasa walikuwa MAKATILI?
 
Mpaka hapa mama ameonesha utofauti mkubwa ,kipindi kile mabomu yangekuwa yashangurumaaa ila mkutano umerushwa online
 
Mkuu wewe ni miongoni mwa members ambao kwa kweli wakini-quote huwa nawaheshimu sana. Heshima yangu kwako ipo juu sana mkuu.

Unajua kinachopelekea haya mambo yatokee.

Hivi Mheshimiwa Mbowe kama kiongozi mkubwa tu, anaongeaje maneno aliyoyaongea kumjibu Rais wa nchi??? Ndio kweli tukae kimya tu????
Kuimba zile pambio kama za enzi zile unaruhusiwa bora tonge linafika kinywani.
 
Mwenyekiti wa kudumu wa CHADEMA amemuonya Rais Samia kuwa asikubali kuliruhusu bunge lililopo sasa hivi lianze mchakato wa katiba mpya.

Mbowe amesema Rais akiruhusu hilo wao kama chama cha upinzani nchini hawatakubali kamwe.

"Kwanza tuna amani mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa ni haki ya kikatiba kisheria na ni wajibu wetu, ombi la mama Samia kwamba tusubiri, tumpe muda hatuko tayari kumpa muda."Freeman Mbowe

====
wenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, amemwomba Rais Samia Suluhu Hassan, aunde Tume ya Katiba, itakayoshirikisha makundi yote kwa ajili ya kufufua mchakato wa katiba mpya “na hatutakubali Bunge hili lililopo, litutengenezee katiba mpya.”

Ombi la Mama Samia kwamba tumpe muda hatupo tayari kumpa muda na natoa agizo kwa Viongozi Nchi nzima wajiandae kwa mikutano ya hadhara siku ambayo tutaitangaza.

Tunapendekeza kuwe na Bunge la Katiba na lisiwe Bunge hili linaloendelea sasa wala wasituambie Bunge hili la sasa ndio liunde Katiba, ichukuliwe rasimu ya Warioba na Katiba na kisha iundwe rasimu ya Katiba mpya, sio gharama na tukiamua tutapata Katiba mpya mwaka huu.

Katiba ni mali ya Wananchi na sio mali ya Viongozi, miongoni mwa mambo ambayo Rasimu ya Katiba ya Warioba ilibainisha ni kupunguza majukumu ya Rais,Warioba alipendekeza tuwe na Tume Huru ya Uchaguzi, Tuwe na Mgombea Huru.
Yake yale ya siku zote. Nyie ni wengi sana msitushinde. My mind is made up, don't confuse me with facts. Sasa tutapate wapi wabunge, ahera?
 
Kwa kauli hii ya Mbowe mama hana option zaidi ya kuwa dikteta.....
otherwise watampelekesha sana hawa....
mama inaonekana ni mpenda haki na utu
lkn naona wanamforce awe dikteta.....
wanasema hakuna mchawi mbaya kama mwanamke....
Akiamua kuwa dikteta kwa sababu watu wanadai haki, na awe. Hatuna cha kupoteza, zaidi ya kongwa zetu za kuonewa na kunyanyaswa.

Marehemu alikuwa dikteta, aliwapoteza baadhi uetu, aliwaua, aliwabbikia kesi, aliwateka, lakini hakutumaliza wote. Hata huyu, japo hatutarajii awe hivyo, akiamua kuwaonea watu wanaodai haki, hatawamaliza. Marehemu hakuwamaliza, naye akawafuata aliowatanguliza.

Duniani ni kituo wakati tukiwa safarini. Tenda wema, itumikie haki, usitumikie chama wala magenge ya waonezi.
 
Hatutakubali hatutakubali, mara Never Never !

Utafikiri tunao huo uwezo wa kufanya chochote kitu[emoji1787]
Uwezo upo. Hakuna kitu kibaya duniani kama kuongoza/kutawala "kondoo". Siku wakijua kuwa hawana cha kupoteza,inakuwa kama Eswatini.
 
neno MKATILI ni relative sana kwani linaweza kuchanganya kusimaia sheria za nchi (ambazo ni za kimabavu naturally) na kuonea raia (ambalo ndyo watu hatutaki). kwani Golda Meir alipokuwa anawapiga na kuwaua waarabu, au Margareth Thatcher alipokuwa akiwabana Labour party kisiasa walikuwa MAKATILI?

..Uko sahihi.

..Mh.Mbowe awe makini.

..Rais Samia naye awe makini.

..Binafsi naona Rais Samia na Mh.Mbowe wanaweza kutekeleza majukumu yao bila kukwaruzana.

..Sanasana namshauri Rais Samia awe mgumu kupeleka msaada wa DOLA kila inapoonekana CCM haina uwezo wa kujibu hoja za wapinzani.
 
Akiamua kuwa dikteta kwa sababu watu wanadai haki, na awe. Hatuna cha kupoteza, zaidi ya kongwa zetu za kuonewa na kunyanyaswa.

Marehemu alikuwa dikteta, aliwapoteza baadhi uetu, aliwaua, aliwabbikia kesi, aliwateka, lakini hakutumaliza wote. Hata huyu, japo hatutarajii awe hivyo, akiamua kuwaonea watu wanaodai haki, hatawamaliza. Marehemu hakuwamaliza, naye akawafuata aliowatanguliza.

Duniani ni kituo wakati tukiwa safarini. Tenda wema, itumikie haki, usitumikie chama wala magenge ya waonezi.
Sasa ndio muache ukaidi wakati dunia inapambana na Uviko 19 nyie mpo busy kuhamasisha maandamano.

Na Mwenyekiti wa kudumu janja janja sana achelewi kubadili gear angani huyu.
 
Back
Top Bottom