Mbowe: Hatutakubali Bunge lililopo litengeneze Katiba Mpya

Mbowe: Hatutakubali Bunge lililopo litengeneze Katiba Mpya

Huu ni sawa na mtego. Upinzani ukianza kumshambulia Rais SSH, wataonekana kama wanamdharau au wanamkejeli kwa sababu ya jinsia yake. Hiki ni kitu ambacho nchi za Ulaya, Amerika zitaanza kusita kuwapa support wapinzani maana kwao haki za kina mama ni kitu muhimu.

Upinzani ukishaonekana kama wana ubaguzi wa kijinsia kwenye dunia ya leo, wataanza kujipaka matope mbele ya watu wao wa nchi za magharibi.
 
Hehehe Mbowe Kwa mahesabu namkubali Sana,kaona bunge likitengeneza katiba yeye hatakuwepo,hivyo hatapata posho.

Anashinikiza iundwe tume anajua atakuwemo,hivyo uhakika wa posho upo.🤣🤣
 
Huu ni sawa na mtego. Upinzani ukianza kumshambulia Rais SSH, wataonekana kama wanamdharau au wanamkejeli kwa sababu ya jinsia yake. Hiki ni kitu ambacho nchi za Ulaya, Amerika zitaanza kusita kuwapa support wapinzani maana kwao haki za kina mama ni kitu muhimu. Upinzani ukishaonekana kama wana ubaguzi wa kijinsia kwenye dunia ya leo, wataanza kujipaka matope mbele ya watu wao wa nchi za magharibi.
Hivi na hao Waulaya na Wamarekani nao wanamawazo finyu kiasi cha kushindwa kutofautisha hoja inayowekwa mezani na mashambulizi ya haiba?
 
Fanyeni hiyo mikutano haramu mama awachape na kuwapa laana mitoto isiyokuwa na adabu.
 
Huu ni sawa na mtego. Upinzani ukianza kumshambulia Rais SSH, wataonekana kama wanamdharau au wanamkejeli kwa sababu ya jinsia yake. Hiki ni kitu ambacho nchi za Ulaya, Amerika zitaanza kusita kuwapa support wapinzani maana kwao haki za kina mama ni kitu muhimu. Upinzani ukishaonekana kama wana ubaguzi wa kijinsia kwenye dunia ya leo, wataanza kujipaka matope mbele ya watu wao wa nchi za magharibi.

..Na mama akianza kutumia mabavu na udikteta ataendelea kuheshimika?

..itakuwa ni jambo la aibu sana kuwa tuna raisi mwanamke halafu ana rekodi mbaya ya kuvunja haki za raia wake.

..itakuwa aibu kubwa kupita ile ya mwendazake. Hatutaeleweka kabisa huko nje.
 
Tuambie tu maana wewe unaonekana uko karibu nae sana mpaka unajua kuwa alienda Asia. Unaogopa nini kuitaja nchi uliokuwa nae?

Amandla...
Hiyo sio ajenda kubwa...mjadala mwambie awe na adabu kijana mdogo pale Hai alimlaza na viatu.

Tena tujue ni lini ataachia hatamu ya uongozi wa chama ajifunze kwa CCM? huyu akipewa nchi atakubali kuachia madaraka kweli?
 
Mwenyekiti wa kudumu wa CHADEMA amemuonya Rais Samia kuwa asikubali kuliruhusu bunge lililopo sasa hivi lianze mchakato wa katiba mpya.

Mbowe amesema Rais akiruhusu hilo wao kama chama cha upinzani nchini hawatakubali kamwe...
Mbowe awe makini asijejikuta akijitangaza kuwa ni kiongozi dhaifu anayedharau wanawake! Kwa nini hakujiima ubavu na saizi yake Dr JPM wakti ule hadi akakaimbia nchi kama leo ana ubavu wa kujipima na Mama SSH?
 
Huu ni sawa na mtego. Upinzani ukianza kumshambulia Rais SSH, wataonekana kama wanamdharau au wanamkejeli kwa sababu ya jinsia yake. Hiki ni kitu ambacho nchi za Ulaya, Amerika zitaanza kusita kuwapa support wapinzani maana kwao haki za kina mama ni kitu muhimu. Upinzani ukishaonekana kama wana ubaguzi wa kijinsia kwenye dunia ya leo, wataanza kujipaka matope mbele ya watu wao wa nchi za magharibi.

Usijidanganye. Kwani Aung San Sun Kyi ni mwanaume? Kiongozi wa kike akionekana anawanyima wananchi wake haki yao ya msingi ya kuwa na mawazo mbadala atashughulikiwa kama kiongozi mwingine yeyote. Ni nyie ambao mnataka atumie mabavu kuwashughulikia wapinzani ndio mnamchuuza. Naamini ana hekima na busara za kutosha kiasi cha kutowasikiliza.

Amandla...
 
Wafuasi wa chadema ni wapenda chuki,walipandikiza chuki kule Mtwara hadi vurugu za gesi zikatokea hadi watu wakauliwa.
Wakawahadaa wana arusha hadi wakapigwa na kuuwawa....
Mtwara waliuliwa na nani mkuu?

Aliyeua watu Arusha ni nani?

Ulimboka alitekwa na nani?

Aqulilina alipigwa risasi na nani?

Madhara ya mikutano anayasababisha nani? Katiba hairuhusu mikutano ya hadhara? Aliyeandika hiyo katiba akaruhusu mikutano ni nani? Duuh, umenikumbusha wala magaidi, wanaoua watu halafu wanasema ni kwa sababu wazungu wanatengeneza silaha. Hata wakikata watu vichwa kwa mapanga, wanasema ni wazungu!.
 
Mbowe awe makini asijejikuta akijitangaza kuwa ni kiongozi dhaifu anayedharau wanawake! Kwa nini hakujiima ubavu na saizi yake Dr JPM wakti ule hadi akakaimbia nchi kama leo ana ubavu wa kujipima na Mama SSH?

..Rais Samia naye awe makini asijejikuta anakuwa kiongozi MKATILI jambo ambalo halitegemewi kwa wanawake.
 
Back
Top Bottom