Mbowe: Hatutakubali Bunge lililopo litengeneze Katiba Mpya

Mwenyekiti wa kudumu wa CHADEMA amemuonya Rais Samia kuwa asikubali kuliruhusu bunge lililopo sasa hivi lianze mchakato wa katiba mpya.

Mbowe amesema Rais akiruhusu hilo wao kama chama cha upinzani nchini hawatakubali kamwe.

"Kwanza tuna amani mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa ni haki ya kikatiba kisheria na ni wajibu wetu, ombi la mama Samia kwamba tusubiri, tumpe muda hatuko tayari kumpa muda."Freeman Mbowe

====
wenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, amemwomba Rais Samia Suluhu Hassan, aunde Tume ya Katiba, itakayoshirikisha makundi yote kwa ajili ya kufufua mchakato wa katiba mpya “na hatutakubali Bunge hili lililopo, litutengenezee katiba mpya.”

Ombi la Mama Samia kwamba tumpe muda hatupo tayari kumpa muda na natoa agizo kwa Viongozi Nchi nzima wajiandae kwa mikutano ya hadhara siku ambayo tutaitangaza.

Tunapendekeza kuwe na Bunge la Katiba na lisiwe Bunge hili linaloendelea sasa wala wasituambie Bunge hili la sasa ndio liunde Katiba, ichukuliwe rasimu ya Warioba na Katiba na kisha iundwe rasimu ya Katiba mpya, sio gharama na tukiamua tutapata Katiba mpya mwaka huu.

Katiba ni mali ya Wananchi na sio mali ya Viongozi, miongoni mwa mambo ambayo Rasimu ya Katiba ya Warioba ilibainisha ni kupunguza majukumu ya Rais,Warioba alipendekeza tuwe na Tume Huru ya Uchaguzi, Tuwe na Mgombea Huru.
Ila kiukweli hayo makundi yote anayoyasema vikiwemo vyama vya siasa wkt ule wa Kikwete.wengi wao walivyopewa nafac ya kila chama ama taasisi wapeleke wawakilishi wengi.wao.walipeleka ndugu michepuko na kunakiongozi mmoja alipeka mkewe.

Hivyo wabongo wengi hatupo makin kwenye mambo yetu ni kelele tu.
 
Moja ya sababu kubwa ya kushindwa kukamilika kwa mchakato wa katiba mpya ni wingi wa wabunge walio kuwemo. Muda mwingi ilitumika kulumbana, kweli mapanya wengi hawachimbi shimo likaenda.

Si kuwa kutokana na kutokuwapo kwa nia njema? Tatizo ni nia njema wala si idadi.
 
Rais kakataa lini?Rais alisema ataonana na wapinzani,nafikiri Jambo la muhimu ni kumsisitizia/kumkumbusha aonane nao halafu mazungumzo yaanze.

..Raisi amekataza mikutano ya hadhara, isipokuwa kwa wabunge.

..agizo hilo ni kinyume na sheria na katiba.

..vilevile agizo hilo linaipendelea ccm na kuviumiza vyama vya upinzani.

..Chama kama chadema kina mbunge mmoja tu ktk bunge la muungano, na vyama vingine vya upinzani havina wabunge kabisa.

..Raisi angeruhusu tu mikutano ya vyama vya siasa. Mikutano hiyo haimzuii yeye au serikali yake kurekebisha uchumi, au kuvutia wawekezaji.

..Kuna shughuli za michezo zinaendelea nchi nzima. Kuna mihadhara ya kidini inafanyika maeneo mbalimbali. Mikutano ya kisiasa haina madhara yoyote ile kwa ustawi wa nchi na ni halali kisheria.
 
Huyu Mbowe naona Sasa anatafuta kurudi Dubai! Hamjui Mama,asimuone mpole vile,anaweza akawa Mkali zaidi ya Magu hasa ukiingia mwenyewe kwenye angaa zake! Mama alisha sema "Ukinizinguwa,tunazinguwana'!!

Mama anajua pia kuwa akizingua anazinguliwa.

Kwanini isiwe tusizinguane?

Maoni na mawazo ya mama si msahafu na hii ni kwa mwingine yeyote.
 
Katiba inadaiwa na walevi? Mkutano umejaa walevi watupu kuanza mwenyekiti hadi wajumbe.
Wazee wa faru John, sipati picha baadae mtavyolewa
Hapa ndipo utawaona wapambe nuksi pangu pakavu tia mchuzi viherehere wakutupwa katiba huru ni kwa wote haichagui Mmesahau chizi aliapa kuwapiga shangazi zenu leo mnakenua
 
..Raisi amekataza mikutano ya hadhara, isipokuwa kwa wabunge.

..agizo hilo ni kinyume na sheria na katiba.

..vilevile agizo hilo linaipendelea ccm na kuviumiza vyama vya upinzani.

..Chama kama chadema kina mbunge mmoja tu ktk bunge la muungano, na vyama vingine vya upinzani havina wabunge kabisa.

..Raisi angeruhusu tu mikutano ya vyama vya siasa. Mikutano hiyo haimzuii yeye au serikali yake kurekebisha uchumi, au kuvutia wawekezaji.

..Kuna shughuli za michezo zinaendelea nchi nzima. Kuna mihadhara ya kidini inafanyika maeneo mbalimbali. Mikutano ya kisiasa haina madhara yoyote ile kwa ustawi wa nchi na ni halali kisheria.

Mkuu sasa kunaelekea chakula kuwiva. Katiba mpya yaja:

Maoni ya kila upande ni rasmi sasa.

Waungwana hawajawahi kushindwa kupata muafaka.
 
Yaani Mbowe anamtisha Rais wa nchi? Huyu mama awe makini, kipindi cha JPM hizi kauli kama za Mbowe hakuna aliethubutu kuongea, na Ikitokea umeongea lazima uchakae
Nini maana ya demokrasia?
 
Huyu Mbowe naona Sasa anatafuta kurudi Dubai! Hamjui Mama,asimuone mpole vile,anaweza akawa Mkali zaidi ya Magu hasa ukiingia mwenyewe kwenye angaa zake! Mama alisha sema "Ukinizinguwa,tunazinguwana'!!
Mbona watu wa CCM hampendi demokrasia?
 
Mwenyekiti wa kudumu wa CHADEMA amemuonya Rais Samia kuwa asikubali kuliruhusu bunge lililopo sasa hivi lianze mchakato wa katiba mpya.

Mbowe amesema Rais akiruhusu hilo wao kama chama cha upinzani nchini hawatakubali kamwe.

"Kwanza tuna amani mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa ni haki ya kikatiba kisheria na ni wajibu wetu, ombi la mama Samia kwamba tusubiri, tumpe muda hatuko tayari kumpa muda."Freeman Mbowe

====
wenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, amemwomba Rais Samia Suluhu Hassan, aunde Tume ya Katiba, itakayoshirikisha makundi yote kwa ajili ya kufufua mchakato wa katiba mpya “na hatutakubali Bunge hili lililopo, litutengenezee katiba mpya.”

Ombi la Mama Samia kwamba tumpe muda hatupo tayari kumpa muda na natoa agizo kwa Viongozi Nchi nzima wajiandae kwa mikutano ya hadhara siku ambayo tutaitangaza.

Tunapendekeza kuwe na Bunge la Katiba na lisiwe Bunge hili linaloendelea sasa wala wasituambie Bunge hili la sasa ndio liunde Katiba, ichukuliwe rasimu ya Warioba na Katiba na kisha iundwe rasimu ya Katiba mpya, sio gharama na tukiamua tutapata Katiba mpya mwaka huu.

Katiba ni mali ya Wananchi na sio mali ya Viongozi, miongoni mwa mambo ambayo Rasimu ya Katiba ya Warioba ilibainisha ni kupunguza majukumu ya Rais,Warioba alipendekeza tuwe na Tume Huru ya Uchaguzi, Tuwe na Mgombea Huru.
Haya sasa. Tulisema mama asicheke na nyani atakula mabua. Wanachotaka sasa jeshi la polisi liwape kipigo kwa kuweka mikutano yao kisha waseme wameuliwa kutekwa na kuteswa.
 
..Raisi amekataza mikutano ya hadhara, isipokuwa kwa wabunge.

..agizo hilo ni kinyume na sheria na katiba.

..vilevile agizo hilo linaipendelea ccm na kuviumiza vyama vya upinzani.

..Chama kama chadema kina mbunge mmoja tu ktk bunge la muungano, na vyama vingine vya upinzani havina wabunge kabisa.

..Raisi angeruhusu tu mikutano ya vyama vya siasa. Mikutano hiyo haimzuii yeye au serikali yake kurekebisha uchumi, au kuvutia wawekezaji.

..Kuna shughuli za michezo zinaendelea nchi nzima. Kuna mihadhara ya kidini inafanyika maeneo mbalimbali. Mikutano ya kisiasa haina madhara yoyote ile kwa ustawi wa nchi na ni halali kisheria.
Mwenye akili yenye ufaham ndoo atakuelewa lakini wengne humu ambao akili yao ya kilevi wanaendeshwa na mihemuko bila kutumia mantiki.Wanafikiri katuba mpya ni ya Mboe au Chadema.

Sent from my TECNO KA7O using JamiiForums mobile app
 
Jinga kabisa, kamuandalie chai ya jioni Nikki, ulisema igizo limekwama hakuna wajumbe sasa hivi unasema wajumbe walevi, utakuwa baamedi wewe ukitoroka kuosha vyombo kwa Nikki unakimbilia bar.
Naona una genye wewe
 
Back
Top Bottom