Mkuu BAK, uchaguzi ukiruhusiwa kufanyika sehemu yoyote nchini, hata wapiga kura asili mia moja tu (1%) wakijitokeza, CCM watadai uchaguzi huru umefanyika na kujitangazia ushindi, kama ule wa serikali za mitaa na uchafuzi uliofuata wakati wa uchaguzi mkuu.
Lengo liwe kuzuia uchaguzi usiwepo kabisa, watu wasifike kwenye vituo vya kupigia kura kabisa. Hata hao waCCM wasithubutu kwenda huko vituoni.
Ni hivi: CHADEMA na wengine wasiofurahishwa na haya mambo ya CCM hawawezi kukosa watu angalao 50 katika vituo vyote vya kupigia kura nchi nzima.
Hakuna polisi wa kuweza kusimamia kila kituo na kupambana na hao watu 50 wanaosimamia kazi ya kuzuia uchafuzi usitokee. Kama kuna watu wa CCM watakaotaka mapambano kwenye hivyo vituo, basi hiyo itakuwa ni habari tofauti.
Maana yake huo ndio utakuwa mwanzo wa mapambano nchi nzima.
Kama hayo ndiyo wanayoyataka CCM kwa kukaza shingo hivi, basi waambiwe wazi kwamba nchi itachafuka.